JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GARI LAGONGA TRENI NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA

> Mtu mmoja amefariki na wanafunzi 19 kati ya 30 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mpira kuligonga Treni eneo la Gofu jijini Tanga

> Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, SACP Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

Soma - https://jamii.app/AjaliTreniGari
#JFLeo
INADAIWA MWANAMKE AKIFANYA HAYA NDOA YAKE HUVUNJIKA

> Ndani ya JamiiForums unaendelea mjadala unaotaja mambo ambayo mwanamke akifanya husababisha ndoa kuvunjika

> Mwanamke kuchelewa kuamka kabla ya mume, kushindwa kumuhudumia mumewe kimwili (tendo la ndoa) kwasababu za kutojisikia au kisingizio cha kuumwa

> Kutomsikiliza mume pindi anapozungumza na kuwaambia marafiki adhaifu wa mume wako

Maoni yako ni yapi?
Soma - https://jamii.app/KeNdoaKuvunjika
#JFMahusiano
JE, MAFANIKIO HULETWA NA BAHATI AU JUHUDI

> Hoja hii imechambuliwa na wanaJamiiForums katika dhana kuu tatu ambazo ni mafanikio ni zao la bahati, mafanikio hutokana na juhudi na dhana ya 3 ikiwa ni juhudi na bahati huleta mafanikio

Soma > https://jamii.app/DhanaZaMafanikio

#JFMaisha
JESHI LA POLISI LAKIRI KUMBAMBIKIA KESI MFANYABIASHARA TABORA

> Jeshi la Polisi nchini, limekiri kuwa taarifa za awali walizopata kutoka Mkoani Tabora zimeonesha kwamba askari wake walimbambikia kesi mfanyabiashara, Mussa Sadiki

> Alibambikiziwa kesi ya kuvunja na kuiba na alikaa kituoni kwa wiki 1 na alipopelekwa Mahakamani, alisomewa shtaka la mauaji

Soma - https://jamii.app/PolisiKubambikaKesi
#JFLeo
MWENDOKASI KUWEKEWA DALADALA ILI KUPUNGUZA ADHA YA USAFIRI

> Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ameagiza kuongezwa kwa mabasi 10 ya kawaida ktk Usafiri wa Mwendokasi jijini Dar es Salaam ili kupunguza changamoto ya usafiri

Soma - https://jamii.app/DaladalaNjiaUDART
#JFLeo
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

> Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Wajibu Institute katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

> Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

#JFLeo
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA NEW ZEALAND AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Mshukiwa wa shambulio lililotokea jana jijini Christchurch, na kuua watu 49, Brenton Terrant (28) tayari amefikishwa Mahakamani

> Wengine wawili bado wanahojiwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/MosqueShootingSuspect
#JFInternational
WALEMAVU WA MIGUU KUPEWA VIUNGO VYA BANDIA BURE

> Walemavu wa viungo vya miguu 600 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa miguu bandia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)

> Uchunguzi kwa wagonjwa utafanyika mwezi Aprili na wale watakaotakiwa kutumia viungo hivyo watapewa mwezi Mei

Soma - https://jamii.app/MiguuBandiaBure
#JFLeo
WAZAZI NA JAMII WATAJWA KUWA CHACHU YA ONGEZEKO LA RUSHWA

> Watajwa kupokea fedha nyingi toka kwa watoto wao bila maelezo na kuwa kichocheo cha kuendelea kwa ulaji rushwa miongoni mwa watumishi wa umma

> Pia tabia ya kumuona kijana wao asiyetajirika haraka kama mjinga na asiyejituma imekuwa ikiwafanya watumishi kujikita katika vitendo vya rushwa

Soma - https://jamii.app/WazaziJamiiRushwa
PROF. LIPUMBA ATANGAZA MAKATIBU WAKUU WA CUF TAIFA

> Amemtangaza ndugu Khalifa Suleiman Khalifa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho

> Pia amtangaza Magdalena Sakaya Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara

Soma => https://jamii.app/MakatibuCUFTaifa

#JFLeo
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu uwezekano wa Rais Mstaafu kushtakiwa
Maoni ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta kuhusu “Mahakama ya Mafisadi”
RAIS MAGUFULI AITAKA TBA KUTOA MAELEZO YA MATUMIZI YA BILIONI 10

> Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza wa Gereza la Ukonga, Dar

> Ameagiza mradi huo ukabidhiwe kwa JWTZ

Soma > https://jamii.app/RaisMagufuliVsTBA

#JFLeo
SENETA APIGWA KWA UBAGUZI WA DINI

> Seneta Fraser Anning wa Queensland, Australia amepigwa na yai na kijana mmoja baada ya kudai Waislamu wanaohamia New Zealand ndio chanzo cha shambulio lililotokea Msikini na kuua watu 49

Soma > https://jamii.app/NZSenator

#JFInternational
SHAMBULIO LA KIGAIDI, NEW ZEALAND: IDADI YA WALIOFARIKI YAFIKIA 50

- Idadi hiyo inafikiwa huku majeruhi wawili wakiwa katika hali mbaya

- Aidha, waliojeruhiwa pia ni 50 huku 36 miongoni mwao wakiwa bado wamelazwa hospitalini

Zaidi, soma https://jamii.app/DeathTollRises50-NWZLND
PAPUA, INDONESIA: TAKRIBANI WATU 50 WAMEFARIKI KWA MAFURIKO

- Maafisa wa Serikali wamesema idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati uokoaji ukiendelea

- Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa na maporomoko ya ardhi yamejeruhi watu wengine 50

Zaidi, soma https://jamii.app/FloodsIndonesia-Machi2019
ARDHI KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI KWA SHILINGI 5,000

- Wizara ya Ardhi imezindua mpango wa kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni au hati ya kieletroniki itakayodumu miaka mitano

- Kuanza Dar es Salaam na kisha kuendelea mikoa yote

Zaidi, soma https://jamii.app/ElectronicLandLicence
MARA: MALIGHAFI ZISIZO NA KIBALI ZA KUTENGENEZEA POMBE ZAKAMATWA

- Kituo cha Forodha Sirari kimekamata mapipa 386 ya lita za ujazo 96,500 yenye malighafi ya thamani ya Tsh. Milioni 246.6

- Yalikuwa yakisafirishwa kinyemela kwenda Kenya

Zaidi, soma https://jamii.app/MalighafiZakamatwaSirari