JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LAGOS: TAKRIBANI WATU 9 WAMEFARIKI NA 40 KUOKOLEWA BAADA YA JENGO KUANGUKA

- Ni kwa mujibu wa Mratibu wa Mamlaka ya Taifa ya Kushughulikia Majanga ya Dharura, Ibrahim Farinloye

- Hata hivyo, watu wapatao 100 wanahofiwa kufunikwa na kifusi

Zaidi, soma https://jamii.app/BuildingCollapseNGR-2019
NDUGAI: SINA TAARIFA KUHUSU KUSITISHWA KWA MSHAHARA WA LISSU

- Amemtaka Mbunge huyo kuandika barua kwenda ofisi ya Spika kueleza madai yake

- Amesema Bunge linataratibu zake na Mbunge ni Mtumishi wa Umma kama walivyo wengine anapaswa kufuata taratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/MshaharaLissu-Ndugai
WAFUNGWA 700 WAPATA MSAMAHA DRC

> Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC), Felix Tshisekedi amewasamehe wafungwa 700 wa kisiasa waliokuwa jela kwa makosa mbalimbali

> Wafungwa hao walifungwa katika utawala wa mtangulizi wake, Joseph Kabila

Zaidi, soma https://jamii.app/700PrisonersFree
JOSHUA NASSARI(CHADEMA) AVULIWA UBUNGE

- Spika Job Ndugai amemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi

- Spika amesema Nassari amepoteza sifa kwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAvuliwaUbunge
NASSARI ADAI ALIWASILIANA NA OFISI YA SPIKA

- Mbunge huyo ameieleza JamiiForums kuwa hana taarifa rasmi naye ameona taarifa zikisambaa mitandaoni

- Pia, ameeleza kuwa Januari 29, 2019 aliwasiliana na Ofisi ya Spika na kueleza juu ya kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAvuliwaUbunge
WASHTAKIWA WA MAUAJI WAFUTIWA KESI BAADA YA RAIS MAGUFULI KUAGIZA UCHUNGUZI

- DPP Biswalo Mganga amesema Rais aliagiza uchunguzi baada ya kusoma barua ya Mshtakiwa mmoja kwenye gazeti

- Aliandika barua kuonesha Polisi walivyombambikia kesi

Zaidi, soma https://jamii.app/WafutiwaKesiMauaji
TATIZO LA UMEME NCHINI VENEZUELA KUMALIZIKA POLEPOLE

> Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo ametangaza kuwa tatizo la kukatika kwa umeme linashughulikiwa haraka

> Katika kero nyingine, bado kuna baadhi ya maeneo mabomba ya maji yanatoa maji mazito meusi

Zaidi, soma https://jamii.app/PowerOutbrakeVenez
KILIMANJARO: DC WA HAI AVUNJA MABARAZA YA ARDHI YA KATA

- DC Lengai Ole Sabaya ameagiza kuvunjwa kwa mabaraza ya ardhi ya Kata 3 ndani ya saa 24

- Ameagiza hivyo kutokana na kulalamikiwa na Wananchi kuhujumu haki zao katika kumiliki ardhi

Zaidi, soma https://jamii.app/MabarazaArdhiYavunjwaHai
SHAMBULIO MSIKITINI NEW ZEALAND: BAADHI YA WATU WAHOFIWA KUFARIKI

> Mtu aliyevalia kijeshi akiwa na silaha aliingia ndani ya Msikiti wa Masjid Al Noor na kuanza kufyatua rusasi

> Ndani ya Msikiti kulikuwa na Waumini 300

Soma > https://jamii.app/NewZealand

#NewZealandMosqueShooting
WANAWAKE WATUMIA UGORO KUPANGA UZAZI NA KUMALIZA ASHKI ZAO

> Baadhi ya wanawake wa Urambo wanatumia ugoro (tumbaku iliyosagwa) kama njia ya kupanga uzazi na kupunguza hamu ya kufanya mapenzi. Huweka sehemu ya siri kisha kuutoa baada ya muda

> Tabia hiyo imezoeleka sana miongoni mwa wanawake wasio na wenza, ikiwemo wajane na wanawake wasio katika uhusiano na wanaume ama kuolewa hutumia kama njia kumaliza hamu zao

Zaidi, soma - https://jamii.app/UgoroUzaziMpango
#JFLeo
POLISI AFARIKI AKIWA BAA BAADA YA KULEWA SANA

> Askari Polisi, PC Donald Motoulaya (29) wa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, amekutwa amefariki akiwa kwenye baa iitwayo Friends Pub iliyopo Manispaa ya Songea mkoani humo

Soma - https://jamii.app/PolisiKifoBaa
#JFLeo
ISRAEL YAFANYA KIKAO CHA DHARURA BAADA YA SHAMBULIZI TEL AVIV

> Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu jana usiku aliitisha majadiliano ya dharura ya kijeshi na makamanda wa Jeshi baada ya shambulizi la maroketi dhidi ya Tel Aviv kutoka Gaza

> Habari mpya zinasema leo alfajiri ndege za kivita za Israel nazo zimefanya mashambulizi ya kujibu

Soma - https://jamii.app/TelAvivAttack
#JFInternational
POLISI AMUUA MKEWE KWA MADAI YA KUZAA NJE YA NDOA

> KENYA: Patrick Nyapara amemuua mkewe, Christine Maonga (28) kwa kumpiga risasi mara tatu kichwani kwa madai kuwa mkewe alipata ujazito nje ya ndoa na kumsingizia kuwa yeye ndiye baba wa mtoto huyo baada ya kujifungua

> Afisa huyo alitoweka baada ya kutenda kitendo hicho

Soma - https://jamii.app/MumeAuaMkeRisasi
#JFInternational
MSUMBIJI HATARINI KUKUMBWA NA KIMBUNGA HATARI

> Watu wanaoishi katika Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo wameonywa juu ya kutokea kwa hali mbaya zaidi kutokana na Kimbunga kikali kitakachosababishwa na tufani iliyopewa jina la Idai

> Mpaka sasa Tufani hiyo imeshasababisha vifo vya watu 66 na safari nyingi za ndege zimesitishwa

Soma - https://jamii.app/HatariKimbungaMaputo
#JFInternational
WALAJI WA DONA BILA KUOSHA HATARINI KUPATA SARATANI YA INI

> Ni kutokana na kuwa ni kiasi kikubwa cha sumukuvu ambayo hupatikana kwenye mazao ya nafaka hasa mahindi na karanga, hivyo walaji wa ugali wa dona wapo hatarini zaidi ikiwa hatua za uandaaji wa chakula hicho hautazingatiwa

> Ni lazima mahindi yaoshwe kwa umakini na usahihi kwani wengi huyahifadhi kwa kutumia dawa

Soma - https://jamii.app/OshaDonaSaratani
#JFLeo
MICHEZO: DROO LIGI YA MABINGWA ULAYA

> Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limetangaza timu zitakazochuana kwenye hatua ya robo fainali
UPDATE: Baada ya UEFA kutangaza michezo ya hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, hivi ndivyo safari ya kuchukua Ubingwa itakavyokuwa

Je, unadhani nani ataibuka kidedea?

#JFSports | #JFMichezo
MICHEZO: DROO YA ROBO FAINALI LIGI YA EUROPA
-
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limetangaza timu zitakazochuana kwenye hatua ya robo fainali katika Ligi ya EUROPA
MWILI WA MWANAFUNZI WAKUTWA KWENYE ENEO LA KICHAKA

> Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Yungwe Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuawa kichakani na sababu za kifo bado hazijajulikana

> Alipotea tangu Machi 1

Soma - https://jamii.app/MwiliMwanafunziKichakani
#JFLeo