JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ILALA, DAR: ALIYESHTAKIWA KWA SHERIA ZA NJE AACHIWA HURU

Mahakama imemuachia huru, Isidory Karume (57) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kukutwa akimiliki risasi mbili za bastola

> Alishtakiwa kwa sheria isiyokuwepo Tanzania

Soma > https://jamii.app/AachiwaHuruRisasi

#JFLeo
SHERIA YA HALI YA HATARI NCHINI SUDAN YAPUNGUZWA MUDA

> Muda wa kutekelezwa sheria ya hali ya hatari nchini Sudan umepunguzwa kutoka mwaka mmoja na kuwa miezi sita

> Tangazo la kupunguza muda wa sheria hiyo limetolewa na Bunge

Soma - https://jamii.app/MudaSheriaHatari
#JFInternational
UINGEREZA: BUNGE LAUKATAA MPANGO WA BREXIT

> Bunge la Uingereza laukata mpango wa nchi hiyo kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya uliowasilishwa na Waziri Mkuu, Theresa May

> Kura 391 zaukataa mpango huo huku Wabunge 242 wauukiunga mkono

Soma => https://jamii.app/MayBrexit

#JFLeo
MAREKANI KUWAONDOA WANADIPLOMASIA WAKE VENEZUELA

> Itawaondoa wafanyakazi wake wote wa ubalozi waliobakia nchini Venezuela kwasababu hali imezidi kuwa mbaya nchini humo

> Uwepo wao unazuia Marekani kuchukua hatua juu ya Venezuela

Soma - https://jamii.app/UsVenezuelaCrisis
#JFInternational
SINGIDA: MWENYEKITI WA HALMASHAURI ASHAURI 'UCHANGUDOA' UHALALISHWE

- Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba, Simon Tyosela amesema biashara hiyo itasaidia kuinua mapato

- Ni baada ya Mkuu wa Mkoa kusema madada poa na machangudoa watakamatwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwnyktIrambaUchangudoa
BAJAJI YAMGONGA ASKARI WA BARABARANI AKIWA KAZINI

- Askari Jenipher, WP.10492PC aligongwa jana katika barabara ya Kahama-Kiinza huko Kahama Mjini, Shinyanga

- Amelazwa katika hospitali ya Wilaya baada ya kupata majeraha na anaendelea vizuri

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariAjaliKazini
EAC KUUNDA TAASISI YA KUTEKELEZA SARAFU MOJA

> Kamati ya sheria ya Afrika Mashariki imepitisha rasimu ya kuanzisha taasisi ya fedha ambayo pia ni taasisi ya takwimu ya Jumuiya, ikiwa ni sehemu muhimu ya mkataba wa umoja wa kifedha wa EAC

Zaidi, soma https://jamii.app/EACIstitute1Coin
TSH. TRILIONI 20.85 KUTUMIKA KWENYE MATUMIZI YA KAWAIDA NA UCHAGUZI

- Ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020

- Fedha hizo ni kati ya Tsh. Trilioni 33.1 ambazo Serikali inatarajia kukusanya kwa mwaka wa fedha ujao

Zaidi, soma https://jamii.app/GharamaUchaguzi2019-20
ITALIA: WABAKAJI WAACHIWA KWA KUWA SURA YA ALIYEBAKWA HAIVUTII

> Waliachiwa baada ya Majaji kuamua kuwa mlalamikaji ana ‘uanaume wa kimaumbile’ na hivyo hamvutii mbakaji

> Hata hivyo, wameshtakiwa tena kwa amri ya Mahakama ya rufaa

Zaidi, soma https://jamii.app/MvutoSuraUbakaji
UCHAGUZI NCHINI ALGERIA WAAHIRISHWA

> Uchaguzi wa urais nchini humo uliotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi ujao umeahirishwa baada ya Rais Abdelazi Bouteflika kutoa uamuzi huo jana na kusababisha maelfu ya wananchi kuandamana

Zaidi, soma https://jamii.app/AlgeriaElectionDelay
UN: SERIKALI YA RAIS PIERRE NKURUNZIZA YAZIDI KUWA KANDAMIZI

- Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi

- Tume hiyo imeeleza kusikitishwa kwa kufungwa ofisi ya UN ya haki za binadamu nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliYatajwaKandamizi-BRND
AUSTRALIA: KADINALI GEORGE PELL AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 6

- Mahakama imemuhukumu kwa kumkuta na hatia ya kuwanyanyasa kingono Wavulana 2

- Pell, aliyekuwa Waziri wa uchumi wa Vatican, anaelezwa kufanya hivyo zaidi ya miaka 20 iliyopita

Zaidi, soma https://jamii.app/CardinalSentenced6Yrs-AUST
PROFESSA LIPUMBA APITISHWA KUGOMBEA UENYEKITI CUF

- Prof. Ibrahimu Lipumba ni miongoni mwa Wanachama watatu waliopitishwa na Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF)

- Wengine waliopitishwa ni Diana Daudi Simba na Zuberi Mwinyi Hamisi

Zaidi, soma https://jamii.app/LipumbaKugombeaUenyekiti-2019
WATUMISHI MBARONI KWA WIZI WA DAWA

> Watumishi watatu wa idara ya afya Wilayani Chato mkoani Geita wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa dawa mbalimbali zinazodaiwa kuwa mali ya Serikali

> Wapo waganga wafawidhi 2 na mtunza stoo

Zaidi, soma https://jamii.app/WatumishiWiziDawa
WATAALAMU WA ATOMIKI WAKUTANA, TANZANIA NI MMOJA WA WANUFAIKA

> Wamekutana Arusha kujadili utekelezaji miradi ya matumizi salama ya Sayansi na Teknolojia ya nyuklia Afrika

> Tanzania ilipata Tsh. Bilioni 9 na kununua vifaa tiba vya Saratani

Zaidi, soma https://jamii.app/MatumiziTeknolojiaAtomiki
NIGERIA: JENGO LENYE SHULE LAANGUKA, WENGI WAHOFIWA KUFA

- Jengo la ghorofa 3 lililokuwa na shule ya msingi na makazi limeanguka leo saa nne asubuhi(saa za huko)

- Uokoaji unaendelea na Watu kadhaa wametolewa kwenye vifusi wakiwa na majeraha

Zaidi, soma https://jamii.app/BuildingCollapseNGR-2019
HARRY KITILYA NA WENZAKE WAANZA KUJIBU KESI DHIDI YAO

- Kamishna huyo Mkuu mstaafu wa TRA na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wameanza kujibu

- Ni katika Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiUfisadiKitilyaYaanza
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WATAALAMU WA UJENZI WA UWANJA WA MICHEZO DODOMA

- Utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma-Morogoro na utachukua Watazamaji 85,000 hadi 100,005

- Unajengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco, Mtukufu Mohammed VI

Zaidi, soma https://jamii.app/RamaniUwanjaDodoma
MOSHI: MAGARI MADOGO YA ABIRIA YAGOMA KUTOA HUDUMA

- Hiace zitoazo huduma katika maeneo ya KCMC, Soweto, Majengo na Bonite zimegoma kuanzia leo saa 5 asubuhi

- Madereva wanapinga kukamatwa na Polisi kwa kutolipa ushuru wa Tsh. 1000 kila siku

Zaidi, soma https://jamii.app/HiaceZagomaMoshi-Mach2019
PROFESSA LIPUMBA ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CUF

- Ameshinda leo Machi 13 kwenye uchaguzi mkuu wa 7 wa Chama Cha Wananchi(CUF) uliofanyika Jijini Dar

- Amepata kura 516(88.9%), haikuelezwa ni kura ngapi zimepigwa ila kulikuwa na Wajumbe 598

Zaidi, soma https://jamii.app/LipumbaAwaMwenyekiti