JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAHAMU KUHUSU CHEMBE YA MOYO NA VISABABISHI VYAKE

> Chembe ya moyo (Angina Pectoris) ni tatizo linalotokea pale moyo unapopata hewa ya Oksijeni kidogo tofauti na mahitaji yake

> Inaelezwa kuwa Watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni; Wanaovuta sigara, Wanene kupita kiasi na wenye ugonjwa wa kisukari

> Dalili kubwa ni maumivu katikati ya kifua yanayokua kuelekea kwenye mkono wa kushoto

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UgonjwaChembeMoyo
#JFAfya
NDEGE ZA ISRAEL ZAISHAMBULIA NGOME YA HAMAS

> Ndege za kijeshi za Israel zimeishambulia ngome ya Hamas Kaskazini mwa Gaza

> Hatua hiyo imekuja baada ya Hamas kuulipua upande wa Israel katika eneo la Gaza

Soma - https://jamii.app/IsraelVsHamasGaza
#JFInternational
MAWAZIRI WA FEDHA AFRIKA WAKUTANA KUJADILI HATUA NA SERA ZA KIUCHUMI

> Mawaziri wa fedha na wataalamu wa nchi za Afrika wamekutana Yaoundé, Cameroon kwenye mkutano wa siku 5, kujadili sera na hatua zinazohitajika kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya kiuchumi

#JFInternational
PUTIN ASITISHA MKATABA WA UTEKELEZAJI WA SILAHA ZA NYUKLIA

> Rais Vladimir Putin amesaini amri ya kusitisha mara moja utekelezaji wa Mkataba wa Silaha za Nyuklia za masafa ya Kati(INF) hadi Marekani itakapoacha kupuuza wajibu wake

Soma - https://jamii.app/PutinSuspendsNuckearTreaty
#JFInternational
FAHAMU HAYA KUHUSU IPTV (KUANGALIA RUNINGA KWA KUTUMIA INTANETI)

> Hii ni aina ya uangaliaji runinga kupitia mtandao (intaneti) ambapo kituo cha runinga badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa intaneti

> Utahitaji kifaa chenye intaneti na uwezo wa kurusha matangazo ili kuweza kuangalia kama vile simu janja (smartphone), kompyuta au runinga zenye intaneti (smart tv)

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UfahamuTvIntaneti
#JFTeknolojia
SERIKALI: MARUFUKU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRISHA MIZIGO NA BARUA

> Ni marufuku kusafirisha vifurushi na barua bila ya kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA)

> SUMATRA imeagizwa kuendesha oparesheni kali ili kudhibiti vitendo hivyo

Soma > https://jamii.app/GvtVsUsafirishajiMizigo

#JFLeo
MAREKANI: MGONJWA WA PILI WA UKIMWI APONA

> Wanasayansi wamefanikiwa kumtibu mgonjwa wa pili aliyeathirika na VVU tangu ugonjwa huo uanze kuathiri Wanadamu miaka ya 1980

> Mchakato wa kutengeneza tiba hiyo umechukua takribani miaka 12

Soma > https://jamii.app/USTibaHIV

#JFLeo
NEC YAONGEZA VITUO 858 VYA KUPIGIA KURA

> Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage leo Machi 5 amesema wameongeza vituo vya kupigia kura 858 na kufanya idadi ya vituo kupanda kutoka 36,549 hadi 37,407

> Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 2020

Soma - https://jamii.app/OngezekoVituoKura
#JFLeo
UCHAGUZI YANGA SASA KUFANYIKA MACHI 10, 2019

> Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Yanga, uliosimamishwa kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi Mahakamani, sasa umepangwa kufanyika Machi 10

> Awali, ulipangwa kufanyika Januari 13, 2019

Soma - https://jamii.app/UchaguziYangaMachi10
#JFMichezo
ELIMU YA URAIA: SHERIA INASEMAJE KUHUSU KUKAMATWA KWA WATOTO?

> Sheria ya Mtoto inasema kuwa endapo Mtoto atakamatwa na Askari Polisi, ni
jukumu la lazima kwa askari huyo kumtaarifu mzazi au mlezi wa mtoto huyo pasipo kuchelewa

Soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
EWURA: MAFUTA YA DIZELI YAPANDA HUKU PETROLI IKISHUKA

> Bei ya rejareja kwa dizeli imeongezeka kwa Shilingi 51 kwa lita 1 sawa na ongezeko 2.44%

> Aidha, bei ya Petroli imepungua kwa Shilingi 23 kwa lita 1 ambayo ni sawa na 1.07%

Zaidi, soma => https://jamii.app/BeiMafutaMachi

#JFLeo
UMUHIMU WA KUMSIKILIZA MTOTO WAKO

> Ukimsikiliza mtoto unampa kujua kuwa yeye ni wa thamani kwako na kumfanya aone kwamba unamjali na kujali mawazo yake

> Wataalamu wanaeleza kuwa mzazi akimsikiliza mtoto hujenga mahusiano ya karibu sana na kumfanya mtoto awe muwazi tangu akiwa mdogo

> Msikilize lolote analolizungumza na jali mawazo yake

Zaidi, soma - https://jamii.app/UmuhimuKumsikilizaMtoto
#JFMahusiano
UEFA YAKATAA OMBI LA REFA ALIYEOMBA KUTOCHEZESHA MCHEZO KATI YA REAL MADRID NA AJAX

> Mwamuzi Felix Brych aliomba asichezeshe mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya(UEFA)

> Brych alieleza kuwa ana mgogoro na waamuzi wasaidizi wa mchezo huo

#JFMichezo
BUNGOMA, KENYA: MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMUUA MWANAFUNZI

> Ni Mwalimu wa Bishop Adudo Boys School ambaye alimpiga Mwanafunzi kwa kosa la kutomaliza kazi ya darasani aliyompatia

> Imeelezwa kuwa alimjeruhi kichwani

Soma => https://jamii.app/MwalimuAuaBungoma

#JFInternational
KISUTU, DAR: TAKUKURU YAWASILISHA OMBI LA KUTAKA MALINZI AHOJIWE TENA

> Hii ni baada ya shahidi wa 11 katika kesi hiyo kumaliza kutoa ushahidi wake

> Hakimu Kasonde anayesimamia kesi hiyo amekubaliana na ombi hilo

Zaidi, soma > https://jamii.app/MalinziKuhojiwaTena
KENYA: RAIS KENYATTA AWATAKA WANAOMTUHUMU KWA WIZI, WAMRIPOTI KWA DCI

> Rais Kenyatta awataka wanaomtuhumu kwa wizi wa mali za taifa wamripoti kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI)

> Awataka waache siasa kwenye vita ya rushwa

Soma > https://jamii.app/KenyattaDCI

#JFInternational
ELIMU YA URAIA: Mfumo wa Kisheria na Uhuru wa Vyombo vya Habari

> Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ndio sheria Mama kwenye tasnia ya habari nchini

> Ndani ya miaka 4 magazeti 6 yamefungiwa kwa muda kati ya miezi mitatu (3) na miaka mitatu.

#JFCivicSpace
BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA KUJENGA BARABARA KIGOMA

> Serikali na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimesaini mikataba 2 ya mkopo wa takribani Tsh bilioni 589.3 za ujenzi wa barabara ya Kabingo-Kasulu-Manyovu

Soma - https://jamii.app/AfDBMkopoTanzania
#JFLeo
TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJINUFAISHA

> Mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, ukiitumia kwa mlengo chanya inaweza kukutajirisha kwasababu inatumiwa na wengi, imegeuza Dunia kuwa kijiji kimoja na hukukutanisha na watu kiurahisi

> Inakuza watu kiakili kwani kuna kurasa nyingi nzuri zenye mafundisho tofauti ikiwemo ndoa, uchumi, biashara, mahusiano & familia na inaweza kukusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika maisha

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/SocialMediaUse
#JFHoja
WAFUNGWA NA MAHABUSU 340 WAKUTWA NA VIRUSI VYA UKIMWI

> Wafungwa na mahabusu 340 kati ya 15,250 ktk Gereza Kuu la Kingolwira Mkoani Morogoro waliopima Virusi Vya UKIMWI, wanaume waliokutwa na maambukizi ni 292 na wanawake ni 48

Soma - https://jamii.app/Wwfungwa340VVU
#JFLeo