JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: WASAFIRI WA NDEGE WAKWAMA UWANJA WA JOMO KENYATTA

> Usafiri wa anga umevurugika nchini Kenya kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa Mamlaka ya anga ya nchi hiyo(KAA)

> Wadai kutopendezwa na Bodi ya Menejimenti ya KAA

Zaidi, soma => https://jamii.app/KenyaSafariNdege

#JFInternational
NDUGU WASUSIA MAJENEZA YENYE MIILI KWENYE MPAKA WA NCHI

> Watu waliokuwa wakisafirisha miili 3 ya marehemu kutokea Afrika Kusini - Msumbiji wamesusia majeneza mpakani baada ya kuambiwa hawana nyaraka stahiki za kuvusha miili hiyo

Soma - https://jamii.app/WasusiaMaitiMpakani
#JFInternational
WAFANYAKAZI WA CLOUDS WAPATA AJALI WAKITOKA KUMZIKA RUGE

> Wafanyakazi 6 wa Kampuni ya Clouds Media Group wamepata ajali nje kidogo ya Jiji la Dodoma baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupinduka

> Hakuna aliyepata majeraha makubwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/AjaliWafanyakaziCMG
#JFLeo
OPARESHENI: MAGOGO YA KUKATIA NYAMA BUCHANI KUCHOMWA MOTO

> Operesheni hii imelenga kuwasaidia walaji wa nyama kula nyama isiyo na uchafu wowote

> Wafanyabiashara watakiwa kuyaondoa magogo hayo na kutumia mashine za kukatia nyama

Zaidi, doma => https://jamii.app/MagogoNyamaBucha

#JFLeo
ROMBO: MAITI YA KIJANA YAKUTWA MSITUNI

> Mwili wa Godwin Massawe (25) umepatikana katika msitu wa Katangara huku chini yake kukiwa na Biblia, amevaa rozari shingoni na kupiga magoti

> Alitoweka Januari 20 na mwili wake ulipatikana Machi 1

Soma - https://jamii.app/MwiliKijanaPorini
#JFLeo
UFAHAMU KUHUSU SHERIA ZA KODI YA MAPATO

> Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapato yake yanatokana na vyanzo mbalimbali kama vilivyoainishwa ikiwemo Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika, Ajira yoyote afanyayo mtu

> Uwekezaji katika rasilimali kama nyumba, ardhi na hisa, Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio (Final Withholding Tax) kama Kodi ya pango, malipo ya gawio kutoka katika kampuni kwa Mtanzania, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (Mrahaba)

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/SheriaKodiMapato
#JFSheria
MZEE AUAWA KWA TUHUMA ZA KUROGA MVUA ISINYESHE

> Wananchi wenye hasira wamemuua Mzee Dimon Senyagwa (85) kwa kumshambulia kwa mawe na silaha za jadi wakimtuhumu kuzuia mvua isinyeshe kwa kutumia ushirikina ili mazao yaliyopandwa yanyauke

Soma - https://jamii.app/MzeeKifoUshirikina
#JFLeo
KINONDONI, DAR: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 8

> Francis Mwakajila(25) anatuhumiwa kufanya kosa hilo Januari 14, 2019

> Francis amekana kutenda kosa hilo. Ashindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande

Soma => https://jamii.app/KijanaAbakaUbungo

#JFLeo
BIASHARA YA HOSTELI, FAIDA NA CHANGAMOTO ZAKE

> Ni biashara ambayo ili kuifanyia kazi haraka itategemea na wingi wa wanachuo katika chuo unachokilenga katika biashara yako

> Usafi na ubora ni muhimu kuzingatia hasa Huduma za maji na choo, gharama isiwe kubwa sana, na umeme usiwe wa kusumbua

> Changamoto zake ni kama nyumba ya kupanga na pale ambapo unawekeza pesa nyingi halafu chuo kinakuja kujenga hosteli zake

Soma - https://jamii.app/BiasharaHosteli
#JFBiashara
IRAN YAITUHUMU MAREKANI KUTAKA SERIKALI YAKE

> Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameituhumu Marekani kwa kupanga njama ya kutumia shinikizo la kiuchumi kuipindua Serikali hiyo

> Amesema Iran haiko katika vita vya kiuchumi na Marekani

Soma - https://jamii.app/USVsIranGovern
#JFInternational
ELIMU YA URAIA: JE, POLISI ANAHAKI YA KUKUPIGA UWAPO KIZUIZINI?

> Hana haki ya kukupiga au kukutisha. Kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, na taratibu za Askari Polisi

> Una haki ya kumzuia Polisi kukupiga kama kuna uwezekano

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
BAADA YA RAIS MAGUFULI KUHOJI SAKATA LA MO DEWJI, MAMBOSASA ATOA MAJIBU

> Kamanda wa Polisi Dar, Lazaro Mambosasa amesema yeye alishamaliza kazi yake

> DCI anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.

Zaidi, soma => https://jamii.app/MambosasaAjibu

#JFLeo
UGANDA: AJUZA WA MIAKA 80 AJIUNGA NA DARASA LA KWANZA

> Mzee huyo wa miaka 80 amesema lengo lake ni kusomea Ualimu

> Amesema ndugu zake wengi wamemtenga hivyo ameazimia kusoma hadi atakapohitimu Chuo Kikuu cha Makelele

Soma > https://jamii.app/80YrsStudentUganda

#JFInternational
KAGAME KUWA NA ZIARA YA SIKU 2 NCHINI

> Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwasili nchini leo Alhamisi kwa ziara ya kikazi

> Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais Dkt. John Magufuli

Soma - https://jamii.app/KagameVisitsTZ
#JFLeo
INDONESIA: VIFO KWENYE MAPOROMOKO YA MIGODI VYAONGEZEKA

> Idadi ya vifo kufuatia ajali iliyotokea katika machimbo ya migodi Kaskazini mwa Indonesia imeongezeka na kufikia watu 16

> Watu 18 wameokolewa wakiwa na majeraha makubwa

Soma - https://jamii.app/GoldminesTragedy
#JFInternational
KAMATI ZA BUNGE KUANZA VIKAO MACHI 11

> Wabunge watapokea Wasilisho la Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti 2019/2020

> Pia zitafanya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha ktk Bajeti ya 2018/2019

Soma - https://jamii.app/VikaoKamatiBunge
#JFLeo
KISUTU: MKURUGENZI WA M HOLDINGS GROUP INAYOMILIKI BANK M AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Sanjeev Kumar amefikishwa mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na kusomewa mashtaka 29 yakiwemo 12 ya utakatishaji wa fedha

> Akosa dhamana na kupelekwa mahabusu

Soma > https://jamii.app/SanjeevKumarKisutu

#JFLeo
WABUNGE PETER LIJUALIKALI NA SUSAN KIWANGA WAACHIWA KWA DHAMANA

> Uamuzi huo umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro

> Mahakama imewapa dhamana baada ya kutupilia mbali maombi ya Jamhuri ya kupinga dhamana yao

Soma => https://jamii.app/KiwangaLijualikaliDhamana

#JFLeo