JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JE, KUTOMSAIDIA AU KUMSAIDIA MTU NI KIPIMO CHA ROHO MBAYA/NZURI?

> Kwa asilimia kubwa mtu akishindwa kumsaidia mtu jambo fulani watu husema kuwa mtu huyo ana roho mbaya

> Pia jamii huwaona watu wenye roho nzuri ni wale wanaosaidia wengine na huwa wanasifiwa na kupendwa mno

> Je, matendo ya mtu katika kusaidia wengine ni kipimo tosha juu ya uzuri au ubaya wa roho yake?

Tembelea - https://jamii.app/RohoMbayaVsNzuri
#JFMaisha
WAGANGA WA KIENYEJI 65 MBARONI

- Waganga 45 wa Mkoani Simiyu na 20 wa Mkoani Njombe wanashikiliwa wakihisiwa kuhusika na mauaji ya watoto

- Wanahusishwa na mauaji yaliyotokea Njombe ambapo baadhi ya miili ilikutwa haina baadhi ya viungo

Zaidi, soma https://jamii.app/Waganga65MbaroniSMY
RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO BARAZA LA MAWAZIRI

- Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

- Wataapishwa Ikulu kesho Machi 4, 2019

Soma https://jamii.app/MabadilikoMawaziriMach2019
LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA VIUMBE HAI WA PORINI NA MAJINI

> Huadhimishwa kila Machi 3 ili kueneza uelewa wa mimea na wanyama mwituni

> Mwaka huu, imedhamiria kueneza uelewa kuhusu viumbe hai wa majini na umuhimu wao kwa maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/SikuWanyamapori-2019
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA TFDA NA TBS ZIUNGWE

- Awataka Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda kuandaa muswada

- Asema itaweza kuondoa malalamiko ya Wafanyabiashara kuhusu tozo nyingi na urasimu

Zaidi, soma https://jamii.app/KuunganishwaTFDA-TBS
BARCELONA YAFUTA ‘UTEJA’ KWA REAL MADRID

- Ni baada ya jana kushinda goli 1-0 na hivyo kushinda jumla ya michezo 96 dhidi ya 95 ya Madrid kwa mara zote walizokutana

- Aidha, imekuwa timu ya kwanza ya La Liga kushinda michezo 4 mfululizo katika dimba la Santiago Bernabeu

Zaidi, soma https://jamii.app/Barca-RealMadrid
MKUU WA WILAYA YA NEWALA APATA AJALI

> Bi. Aziza Mangosongo amelazwa baada ya gari lake kupinduka maeneo ya Mandawa, Lindi

- Taratibu za kumhamisha na wenzake watatu kwenda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi zinaendelea

Zaidi, soma https://jamii.app/DCNewalaApataAjali
WAPIGANAJI WANAOHUSISHWA NA AL-QAEDA WAUA WANAJESHI 21 WA SYRIA

- Wameuawa leo alfajiri katika mapigano yaliyotokea maeneo ya Masasna, Syria

- Shirika linalochungaza Haki za Binadamu nchini humo limesema idadi hiyo ni miongoni mwa kubwa kuwahi kutokea

Zaidi, soma https://jamii.app/21RegimeForcesKilledSYR
KIZIMBANI WAKITUHUMIWA KWA WIZI WA MTANDAONI

- Rajab Makwaya, Rashid Kayombo na Said Issa wamepelekwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora

- Wanatuhumiwa kuiba Tsh. Milioni 2 kwa simu na kumiliki nyumba walizozipata kinyume na sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniWiziMtandaoni
LEMA: CHADEMA IMEPATA BARAKA KWA KUONDOKA KWA LOWASSA

- Mbunge huyo wa Arusha Mjini amedai uamuzi wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa kurejea CCM ni kuweka maslahi binafsi mbele

- Ahusisha na kesi ya mkwewe Sioi Sumari

Zaidi, soma https://jamii.app/LemaVsLowassa
DART YAWATAHADHARISHA ABIRIA WAKE

- Ni kutokana na mvua iliyonyesha leo jijini Dar na kusababisha maji kujaa maeneo ya Jangwani

- Abiria wa Mbezi na Kimara wameshauriwa kutumia mabasi hayo hadi Morocco kisha wachukue usafiri mbadala hadi Kivukoni na Gerezani iwapo mvua itaendelea kunyesha

Zaidi, soma https://jamii.app/DARTYatahadharishaAbiria
MAFURIKO YASABABISHA VIFO VYA WATU 12 AFGHANISTAN

> Mafuriko ya mvua yamesababisha vifo vya watu 12 nchini Afghanistan na uharibifu mkubwa wa mali eneo la Kandahar

> Watu 18 wamejeruhiwa na nyumba laki 5 na elfu 75 zimeharibiwa

Soma - https://jamii.app/12DeadFloods
#JFInternational
WATUMIA "EARPHONES" HATARINI KUPATA MATATIZO YA USIKIVU

> Serikali imesema wanaoshinda na spika masikioni (earphones) kwa muda mrefu wapo hatarini kupata matatizo ya usikivu

> Inakadiriwa, watu 466,000,000 duniani wana matatizo ya kusikia

Soma https://jamii.app/EarphonesVsHearing

#JFLeo
MAANDAMANO YA KUMPINGA RAIS WA ALGERIA YASABABISHA KIFO

> Mtu mmoja amefariki na wengine zaidi ya 180 wamejeruhiwa katika maandamano ya kupinga Rais Abdelaziz Bouteflika (82) kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tano nchini humo

Soma - https://jamii.app/DeathProtestsAlgeria
#JFInternational
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA PROF. KABUDI NA DKT. MAHIGA

> IKULU: Rais John Magufuli, leo amewaapisha Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Zaidi - https://jamii.app/ViapoMawaziriIkulu
#JFLeo
Kauli ya Rais kuhusiana na kilichofanywa na Polisi katika Sakata la kutekwa Mo Dewji
WAHUKUMIWA JELA MIAKA 3 KWA KOSA LA UVUVI HARAMU

> Watu 7 Wilayani Ukerewe wamehukumiwa kwenda jela miaka 3 na Mahakama inayotembea (Mobile Court) kwa kosa la kufanya uvuvi haramu

> Wengine 14 wamefikishwa Mahakama hapo kwa kosa hilo hilo

Soma - https://jamii.app/JelaUvuviHaramu
#JFLeo
MAAFISA WA SERIKALI NCHINI CAMEROON WATEKWA

> Afisa mwandamizi ktk ofisi ya Gavana Buea, ametekwa na watu wasiojulikana na kudaiwa fidia ya mamilioni ya Faranga

> Mwingine ni Mkuu wa kikanda wa Wizara ya Mazingira na Ulinzi

Soma - https://jamii.app/CameroonOfficialsKidnap
#JFInternational