JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA POLISI

> Charles Mkumbo ataongoza Kamisheni ya Intelijensia na Liberatus Sabas amekuwa Mkuu wa operesheni na mafunzo

> Leonard Lwabuzala ataongoza kamisheni ya fedha na logistics

Zaidi, soma - https://jamii.app/UteuziMakamishnaPolisi
#JFLeo
IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAOFISA WA JESHI LA POLISI

> James Mushi, Kamanda wa Polisi Ruvuma awa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi na RPC wa Njombe, Renata Mzinga arudishwa Makao Makuu

> Aidha, ametaja Makamanda wapya wa Mikoa

Zaidi - https://jamii.app/UteuziMakamishnaPolisi
#JFLeo
TUNDURU: MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AUAWA KWA KULIWA NA MAMBA

> Mwanafunzi huyo alikuwa na Mama yake wakifua nguo kwenye Mto Ligoma

> Bimwana Swalehe(12) alikuwa akisoma Darasa la Pili Shule ya Msingi Makoteni

Soma > https://jamii.app/MambaWauaTunduru
KENYA: OFISI YA RAIS YAKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI

> Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya (EACC) imefichua sakata ya ufisadi wa Ksh bilioni 4.8 katika idara ya Magereza kuhusu ununuzi wa bunduki

> Inaripotiwa kwamba wahusika walikuwa tayari wameshapokea 80% ya Ksh bilioni 4.8 za zabuni ya kununulia vifaa hivyo ambavyo vingewekwa katika Magereza kabla ya EACC kuingilia kati na kufichua uozo huo

#JFInternational
NAIROBI, KENYA: RAIS KENYATTA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

> Mwanadiplomasia Amina Mohamed ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo

> Anachukua nafasi ya Rashid Echesa ambaye uteuzi wake umetenguliwa rasmi

Zaidi, soma => https://jamii.app/KenyattaMawaziri

#JFInternational
FASTJET KUNUNUA NDEGE 6 ILI KUREJESHA SHUGHULI ZAKE TANZANIA

> Shirika la ndege la FastJet limesema liko mbioni kununua ndege 6 ili kurejesha shughuli zake kwenye soko la Tanzania

> Pia kurejesha safari za Afrika Kusini, Nairobi na Mombasa

Soma - https://jamii.app/FastJetKurejeaSokoni
#JFLeo
MWILI WA RUGE MUTAHABA KUAGWA KESHO VIWANJA VYA KARIMJEE

> Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group umewasili nchini jioni ya leo

> Maelfu ya Watanzania wamejitokeza kuusindikiza msafara uliobeba mwili wake

#RIPRuge #RugeMutahaba
ELUMU YA URAIA: JE, POLISI ANAWEZA KUKUSHIKILIA MAFICHONI?

> Hapana. Jeshi la Polisi likikushikilia mafichoni ni kinyume cha sheria

> Askari Polisi wanapokuweka rumande ni jukumu lao kuangalia afya yako na kuzilinda haki zako

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFLeo
MVUA YAUA WATU WAWILI ZANZIBAR

> Watu wawili wamefariki katika matukio mawili tofauti yaliyosababishwa na mvua kubwa za masika zilizoanza kunyesha visiwani Unguja

> Waliofariki ni mtoto, Hassan Mohamed (4) na Skachi Abdallah Zahor (26)

Soma - https://jamii.app/MvuaVifoUnguja
#JFLeo
HUSSEIN BASHE: KIKWETE ULIMDHALILISHA LOWASSA, ALIONDOKA CCM KWA SABABU YAKO

> Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini(CCM), Hussein Bashe amemjibu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete aliyemkaribisha tena Edward Lowassa ndani ya CCM

Zaidi, soma => https://jamii.app/BasheVsKikweteTwitter

#JFLeo
ELIMU YA URAIA: JE, ASKARI POLISI ANAWEZA KUJIUNGA NA CHAMA CHA SIASA?

> Hapana, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ni marufuku Askari Polisi kujiunga au kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha siasa

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
RAIS MAGUFULI AWASILI VIWANJA VYA KARIMJEE KUMUAGA RUGE MUTAHABA

> Rais Magufuli amewasili kwenye viwanja hivyo akiwa ameambatana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

#RIPRuge
UUZAJI WA NYUMBA YA MICHAEL JACKSON UNASUASUA KUTOKANA NA UDHALILISHAJI ALIOUFANYA

> Nyumba hiyo inadaiwa kutumiwa ktk kuwanyanyasa kijinsia vijana wa kiume

> 2016 ilikuwa dola milioni 100, 2017 dola milioni 70 na sasa ni dola milioni 31

Soma - https://jamii.app/SaleMJHouse
#JFLeo
LIBERIA: MTOTO WA ALIYEKUWA RAIS AKAMATWA KWA UBADHIRIFU WA FEDHA

> Charles Sirleaf Mtoto wa aliyekuwa Rais Ellen Sirleaf amekamatwa kwa tuhuma za upotevu wa fedha ndani ya Benki Kuu ya Liberia

> Alikuwa Naibu Gavana wa Benki hiyo

Zaidi, soma => https://jamii.app/CharlesSirleafArrested

#JFLeo
RAIS ATOA ONYO KWA WANAOWATOZA USHURU WAJASIRIAMALI

> Rais Magufuli amesema hatamvumilia kiongozi yeyote wa Mkoa, Wilaya ama Halmashauri atakayebainika kuhusika kuwatoza ushuru ama tozo yoyote wajasiriamali wadogo waliopatiwa vitambulisho

Soma - https://jamii.app/UshuruWajasiriamaliVitambulisho
#JFLeo
SAUDI ARABIA: MTOTO WA OSAMA BIN LADEN AFUTIWA URAIA

> Hamza Bin Laden(30) anatuhumiwa kwa kutoa vitisho vya kuishambulia Marekani

> Marekani imetangaza donge nono la zawadi ya Dola Bilioni 1 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake

Soma > https://jamii.app/SaudiaVsHamzaBinLaden

#JFInternational
RWANDA NA UGANDA ZAINGIA KWENYE MZOZO

> Uganda imeishutumu Rwanda kwa kuyazuia magari ya mizigo, ya abiria na Wananchi wake kuingia nchini humo

> Waziri wa Mambo ya Nje Rwanda akanusha, adai raia wao wanakamatwa Uganda

Soma => https://jamii.app/RwandaVsUgandaBoarder

#JFInternational
TSHISEKEDI ATOA AHADI YA KUWAACHIA HURU WAFUNGWA WA KISIASA

> Rais wa DRC, ameahidi kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa ndani ya siku 10 zijazo

> Pia atahakikisha wanasiasa waliokimbia nchini humo kwasababu za kisiasa, wanarejea

Soma - https://jamii.app/WafungwaKisiasaDRC
#JFLeo
JE, MKE KUMZIDI MUME KIPATO HUFANYA NDOA ISIWE IMARA?

> Wanaume wengi hutishwa na wanawake wenye mafanikio makubwa zaidi yao, hasa ya kifedha na wakati mwingine katika elimu

> Kuna tatizo lolote mume kuzidiwa pato na mkewe? Ni kweli kuna madhara hutokea katika ndoa iwapo mke atamzidi kipato mumewe?

Tembelea - https://jamii.app/MkeKuzidiKipato
#JFMahusiano