JamiiForums
52.8K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RWANDA KUZINDUA 'SATELLITE' ITAKAYOZIUNGANISHA SHULE ZA VIJIJINI NA 'INTERNET'

> Satellite hiyo iliyopewa jina la 'Icyerekezo'(uelekeo) imelenga kuwaandaa Vijana na mafunzo ya tehama kwa maisha ya baadaye

Zaidi kuhusu uzinduzi huu, soma => https://jamii.app/RwandaSatellite

#JFLeo
MWANAO AMEWAHI KUKUAIBISHA MBELE ZA WATU?

> Watoto wadogo hukariri yale wanayoyaona na kuyasikia kila siku na wakati mwingine huyasema wakiwa mahali popote hata kama hawajui maana yake

> Je, mwanao amewahi kusema au kufanya jambo mbele za watu mpaka ukapatwa na aibu?

Tembelea - https://jamii.app/KuaibishwaMtoto
#JFHoja
WATU 25 WAFARIKI KWENYE AJALI YA MOTO WA TRENI

> Takribani watu 25 wamefariki na 40 kujeruhiwa ktk ajali ya moto uliotokea ktk kituo cha Treni jijini Cairo, Misri

> Kutokana na ajali hiyo Waziri wa Usafiri, Hicham Arafat ameomba kujiuzulu

Soma - https://jamii.app/20DeadStationFire
#JFInternational
INDIA: BASTOLA FEKI YASABABISHA APOTEZE MAISHA

> Mohammad Palash Ahmed(25), amefariki baada ya kupigwa risasi na Polisi alipoteka Ndege iliyobeba abiria 148 akiwa na bastola feki akitaka nafasi ya kuongea na Waziri Mkuu wa India

Soma - https://jamii.app/KilledToyGun
#JFInternational
VENEZUELA: RAIS WA MPITO AKABILIWA NA KIFUNGO CHA MIAKA 30

> Kiongozi wa upinzani Venezuela, Juan Guaidó, anaandamwa na kifungo cha miaka 30 baada ya kukiuka agizo la kumtaka asitoke nje ya nchi, lililotolewa na Mahakama ya Juu

Soma - https://jamii.app/GuaidoJail30Yrs
#JFInternational
SEHEMU YA KIWANDA CHA BORA YATEKETEA KWA MOTO

> Janga hilo limekikumba kiwanda hicho cha Viatu kilichopo maeneo ya TAZARA jijini Dar

> Kikosi cha zima moto tayari kimefika eneo la tukio na kuendelea na juhudi za uokoaji

Zaidi, soma => https://jamii.app/MotoKiwandaBora
BARIADI: MTU MMOJA AMEFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MGODI

> Aidha, watu wengine watatu pia wanahofiwa kufariki katika mgodi huo

> Tukio hilo limetokea katika mgodi wa dhahabu wa Burambaka uliopo katika Kijiji cha Gasuma

Soma => https://jamii.app/MgodiBurambaka

#JFLeo
NJOMBE: WATU 4 AKIWEMO MTOTO WA MIAKA 15 KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAUAJI

> Mtoto David Kasila mwenye umrinwa miaka pamoja na Mariano Malekela, Edwin Malekela na Kalistus Costa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Machi 4, 2019

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtotoMauajiNjombe

#JFLeo
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MSANII DUDU BAYA

> Msanii Godfrey Tumaini maarufu 'Dudu Baya' anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano

> Anatuhumiwa kumkashfu na kutoa lugha za kejeli kwa marehemu, Ruge Mutahaba
TRUMP AKATAA KUIONDOLEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI

> Rais wa Marekani, Donald Trump alitoka katikati ya mkutano na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un baada ya Kim kuitaka Marekani kuiondolea nchi yake vikwazo vyote ilivyoiwekea

Soma - https://jamii.app/UsVsNorthKorea
#JFInternational
MAJARIBIO YA CHANJO YA UKIMWI NCHINI YALETA MATUMAINI

> Utafiti wa awali wa chanjo ya UKIMWI umeonesha kuwa, ina uwezo wa kusisimua na kufanya mwili wa binadamu utengeneze kinga dhidi ya ugonjwa huo

> Chanjo hiyo ilitengenezwa nchini Sweden

Zaidi https://jamii.app/ChanjoUKIMWITanzania
KIWANDA CHA MABEHEWA KUJENGWA NCHINI

> Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa amefanya makubaliano na Kampuni ya Afrika Jambo Group ya Afrika Kusini kujenga kiwanda cha mabehewa nchini kitakachogharimu dola milioni 150

Soma - https://jamii.app/UjenziKiwandaMabehewa
#JFLeo
BIASHARA: Wanawake wafanyabiashara ndogo ndogo wakigomea kulipa ushuru wa Tsh. 500

> Wanawake hao wameeleza kuwa hawawezi kulipa ushuru huo kwakuwa tayari wametimiza sharti la kuwa na vitambulisho vya Serikali

#JFBiashara
UCHUMI: BOT YATOA TAARIFA BAADA YA UKAGUZI WA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA, DAR

> Benki Kuu yasema imebaini maduka mengi hayafanyi kazi hiyo kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa

> BOT imeanza kuyafutia leseni za biashara maduka hayo

Soma > https://jamii.app/BOTVsForexDar

#JFUchumi
HATMA RUFAA YA MBOWE NA MATIKO KUJULIKANA KESHO

> Hatma ya dhamana ya Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko inatarajiwa kujulikana kesho Machi Mosi, ambapo uamuzi utatolewa na Mahakama ya Rufani kuhusu rufaa aliyokata DPP

Soma - https://jamii.app/HukumuRufaaMbowe
#JFLeo
ELIMU YA URAIA: JE, UNAWEZA KUMUOMBA POLISI AKUSAIDIE MATATIZO YA KIFAMILIA?

> Inawezekana kama tatizo ikiwa lina asili ya kijinai

> Iwapo kinachotokea ni uhalifu kama kumpiga vibaya mwanamke/mtoto, au wanandugu kujamiiana

Zaidi, soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
HISTORIA YA MASHUJAA NA MAKUMBUSHO YA VITA VYA MAJIMAJI

> Vita ya Maji Maji vilivyotokea kati ya Mwezi Julai 1905 mpaka Agosti 1907 na ilianza katika vilima vya Umatumbi Kaskazini mwa mji wa Kilwa na kiongozi aliitwa Kinjeketile

> Watu hawa walipigana kupinga kukandamizwa na kulazimishwa na Wakoloni wa Kijerumani namna ya kuishi, mazao ya kuzalisha na nani wa kumtumikia

> Jina la vita limetokana na imani ya matumizi ya dawa iliyochanganywa na Maji, punje za Mahindi

Tembelea - https://jamii.app/HistoriaVitaMajimaji
#JFHistoria