JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HISTORIA YA VITA VYA KAGERA (TANZANIA NA UGANDA)

> Vita kati ya Tanzania na Uganda, au Vita ya Kagera ilidumu kwa miezi sita kuanzia Novemba 1978 hadi Aprili 1979 na ndiyo iliyouangusha utawala wa Iddi Amin Dada uliodumu kwa muda wa miaka 8

> Vita hiyo ilianza rasmi siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Uganda, Oktoba 9, 1978 baada ya mwanajeshi wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kukutana na mpenzi wake ambaye alikuwa raia wa Tanzania

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HistoriaVitaKagera
#JFHistoria
DEREVA WA MWENDOKASI KIZIMBANI KWA KUMKATA ABIRIA KIDOLE

> Khalid Shaha(43), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shtaka la kumkata kidole Godfrey Liwa kwa kioo cha gari

> Amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana

Soma > https://jamii.app/DARTMahakama
#JFLeo
BALOZI ZA NCHI MBALIMBALI NCHINI ZALAANI KUFUNGIWA KWA GAZETI LA THE CITIZEN

> Wasema wamezoea kupata habari kutoka kwenye gazeti hilo kila siku asubuhi

> Wahoji, adhabu hiyo inaendana na kosa wanalotuhumiwa?

#JFLeo #JFCivicSpace
UKARABATI WA SEKONDARI YA MZUMBE WATILIWA MASHAKA

> Serikali imeagiza uchunguzi wa mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari ya Mzumbe baada ya kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kutofautiana na fedha halisi zilizotolewa

Soma - https://jamii.app/UkarabatiSekondariMzumbe
#JFLeo
MAREKANI YATANGAZA DAU KWA MWENYE TAARIFA ZA MTOTO WA OSAMA

> Marekani imetangaza dau la dola milioni 1 kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu mtoto wa kiume wa aliyekuwa Kiongozi wa kundi la al-Qaeda - Osama Bin Laden, Hamza Bin Laden

Soma - https://jamii.app/USRamsonOsamaSon
#JFInternational
BASATA LASITISHA USAJILI WA DUDU BAYA

> Baraza la Sanaa Tanzania limetangaza kusitisha usajili wa msanii Godfrey Tumaini, maarufu Dudu Baya kuanzia Februari 28

> Anatuhumiwa kumkashifu Marehemu Ruge Mutahaba na kuzungumza maneno ya kejeli

Soma - https://jamii.app/UsajiliDudubayaWasitishwa
#JFLeo
WATU 15 WAPOTEZA MAISHA KWENYE MLIPUKO MJINI MOGADISHU

> Mlipuko mkubwa, sauti za bunduki na mabomu imesikika ndani ya Hoteli ya Maka Al-Mukarama na kundi la Al-Shabaab linadaiwa kuhusika na tukio hilo

> Idadi ya majeruhi mpaka sasa imefikia watu zaidi ya 60

#JFInternational
ARUSHA: VITAMBULISHO VYA WAFANYABIASHARA WADOGO SIO KINGA YA KULIPA USHURU

> Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, imeeleza kuwa Vitambulisho vilivyotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kodi ya TRA

Zaidi, soma => https://jamii.app/UshuruMachingaArusha

#JFLeo
RUFAA YA DPP DHIDI YA MBOWE NA MATIKO YATUPILIWA MBALI

> Mahakama ya Rufaa jijini Dar, leo imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini dhidi ya M/kiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko

Soma - https://jamii.app/MboweMatikoDhamanaYarejeshwa
MTOTO ALIYEIBWA NA KUUZWA TSH 30,000 APATIKANA

> Mtoto Shazira Yahaya aliyeibwa akiwa na siku 7 ktk Kijiji cha Likalangiro-Songea, amepatikana ktk Wilaya ya Moshi Vijijini ambako aliuzwa kwa Tsh 30,000

> Aliibwa Septemba 26, 2018

Soma - https://jamii.app/MtotoAliyeibwaApatikana
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA POLISI

> Charles Mkumbo ataongoza Kamisheni ya Intelijensia na Liberatus Sabas amekuwa Mkuu wa operesheni na mafunzo

> Leonard Lwabuzala ataongoza kamisheni ya fedha na logistics

Zaidi, soma - https://jamii.app/UteuziMakamishnaPolisi
#JFLeo
IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAOFISA WA JESHI LA POLISI

> James Mushi, Kamanda wa Polisi Ruvuma awa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi na RPC wa Njombe, Renata Mzinga arudishwa Makao Makuu

> Aidha, ametaja Makamanda wapya wa Mikoa

Zaidi - https://jamii.app/UteuziMakamishnaPolisi
#JFLeo
TUNDURU: MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AUAWA KWA KULIWA NA MAMBA

> Mwanafunzi huyo alikuwa na Mama yake wakifua nguo kwenye Mto Ligoma

> Bimwana Swalehe(12) alikuwa akisoma Darasa la Pili Shule ya Msingi Makoteni

Soma > https://jamii.app/MambaWauaTunduru
KENYA: OFISI YA RAIS YAKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI

> Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya (EACC) imefichua sakata ya ufisadi wa Ksh bilioni 4.8 katika idara ya Magereza kuhusu ununuzi wa bunduki

> Inaripotiwa kwamba wahusika walikuwa tayari wameshapokea 80% ya Ksh bilioni 4.8 za zabuni ya kununulia vifaa hivyo ambavyo vingewekwa katika Magereza kabla ya EACC kuingilia kati na kufichua uozo huo

#JFInternational
NAIROBI, KENYA: RAIS KENYATTA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

> Mwanadiplomasia Amina Mohamed ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo

> Anachukua nafasi ya Rashid Echesa ambaye uteuzi wake umetenguliwa rasmi

Zaidi, soma => https://jamii.app/KenyattaMawaziri

#JFInternational