JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZIFAHAMU FAIDA TATU(3) ZA KULALA BILA NGUO

> Kupata usingizi wa kutosha, hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya ngozi na husaidia kulinda sehemu za siri zisipate maambukizi ya fangasi

Zaidi, soma => https://jamii.app/FaidaKulalaUtupu
NIGERIA: RAIS MUHAMMADU BUHARI ACHAGULIWA TENA, WAPINZANI WAKATAA MATOKEO

> Rais Buhari ametangazwa kuibuka mshindi kwa kupata kura 15,191,847 (56%) huku mpinzani wake wa karibu Atiku Abubakar akipata 11,262,978 (41%)

Zaidi, soma => https://jamii.app/BuhariReelected

#JFInternational
NDUGU WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUPIGWA SHOTI YA UMEME

> Wasichana, Zulfa Chami (24) na Zuhura Chami (28) wamepoteza maisha, baada ya kupigwa shoti ya umeme kwenye kamba ya nguo katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi wakati wakianika nguo

Soma - https://jamii.app/WafarikiShotiUmeme
FIFA YAMFUNGIA MAISHA MWAMUZI KUTOKA TANZANIA

> Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Duniani imemfungia maisha Oden Charles Mbaga kwa kujihusisha na rushwa ya upangaji matokeo

> Atakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 468 ndani ya siku 30

Soma https://jamii.app/FIFAYamfungiaMbaga
#JFMichezo
BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAANZA VIKAO VYAKE

> Bunge la Afrika Mashariki limeanza vikao vyake vya wiki 2 Zanzibar

> Baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa ni kupambana na rushwa, utawala bora, ukuzaji wa lugha ya Kiswahili, usawa wa kijinsia

Soma - https://jamii.app/BungeEAC
RAIS WA IRAN AKATAA OMBI LA KUJIUZULU LA WAZIRI

> Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema, Rais Hassan Rouhani amekataa ombi la kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Nje Mohammad Javad Zarif

> Zarif alitangaza kujiuzulu wadhifa wake na kueleza shukrani zake kwa watu wa Iran na wafanyakazi wenzake, huku akiomba radhi kwa kushindwa kufanya vizuri kazi zake

#JFInternational
WAZIRI MWAKYEMBE ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMCHUKULIA HATUA DUDUBAYA KWA KUMDHIHAKI RUGE

> Pia ameagiza BASATA limchukulie hatua msanii huyo

> Asema anachokifanya si sahihi, mchango wa Ruge ni mkubwa na hata yeye kaumia

Soma > https://jamii.app/MwakyembeVsDudubaya

#RIPRuge
PAKISTAN YASHAMBULIA NA KULIPUA NDEGE VITA MBILI ZA INDIA

> Shambulio hilo limetekelezwa kwenye Jimbo linalogombaniwa la Kashmir na kuwakamata Marubani 3

> Siku 3 zilizopita India ilifanya shambulio kwenye maeneo ya Pakistan

Soma > https://jamii.app/PakistanVsIndiaJets

#JFInternational
LESENI ZA MIGODI MIKUBWA KUANZA KUTOLEWA NCHINI

> Serikali kupitia Wizara ya Madini inakamilisha taratibu za utoaji wa Leseni kwa Migodi mikubwa hapa nchini

> Aidha, kipaumbele ni katika uongezaji thamani madini ikiwemo ujenzi wa vinu

Soma - https://jamii.app/LeseniMigodiMikubwa
#JFLeo
WALIOIGIZA SAUTI YA KENYATTA NA KUFANYA WIZI WAKAMATWA

> Polisi nchini Kenya wamewakamata watu 7 wanaodaiwa kuigiza sauti ya Rais Uhuru Kenyatta na Maafisa wa Serikali katika kumuibia pesa M/kiti wa Sameer Africa, Naushad Merali

Soma - https://jamii.app/WeziMeraliWakamatwa
#JFInternational
ELIMU YA URAIA: JESHI LA POLISI LINA UHUSIANO NA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI?

> Jeshi la Polisi lina jukumu la kuhakikisha kuwa shughuli zote za kisiasa zinafanyika kwa uhuru na kwa kudumisha amani na utulivu wa Taifa bila ya upendeleo

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
ELIMU YA URAIA: JESHI LA POLISI LINA UHUSIANO NA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI?

> Polisi wana jukumu la kuhakikisha kuwa shughuli zote za kisiasa zinafanyika kwa uhuru na kwa kudumisha amani na utulivu wa Taifa bila ya upendeleo

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
CHANGAMOTO KUBWA ZINAZOJITOKEZA KWENYE BIASHARA

> Ukosefu wa uadilifu na udanganyifu katika kampuni, huleta tabia ya kutoaminiana katika biashara au ujasiriamali

> Usimamizi mbovu wa fedha, mikopo, rasilimali, matumizi ya hovyo, madeni yasiyo ya lazima na maamuzi mabaya

> Mabadiliko ya taratibu za uendeshaji wa biashara za mara kwa mara. Mahala ambapo hapana taratibu nzuri na thabiti siku zote si rafiki kiuwekezaji

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/ChangamotoBiashara
#JFBiashara
KENYA: MWANAFUNZI AFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA KIRANJA

> Mwanafunzi wa Sekondari ya St. Joseph Nyabigena amefariki huku chanzo kikidaiwa ni kupigwa na kiranja

> Kiranja huyo anadaiwa kumpiga marehemu kofi na kisha teke la tumbo

Soma - https://jamii.app/KiranjaAuaMwanafunzi
#JFInternational
MOROGORO: WANAFUNZI 682 WASOMEA KWENYE VYUMBA 7 VYA MADARASA

> Mwanafunzi hao wa Shule ya Msingi Diovuva wamelazimika kusoma kwa kupokezana(zamu)

> Shule hiyo kwa sasa ina vyumba vya madarasa 7 huku uhaba ukiwa ni wa vyumba 6

Zaidi, some => https://jamii.app/MadarasaDiovuva
Serikali imesimamisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa muda wa siku 7 kuanzia leo Jumatano, Februari 27 kwa madai ya kuchapisha habari ya upotoshaji kuhusu maoni ya wataalamu waliozungumzia kuporomoka kwa shilingi iliyochapishwa Februari 23, 2019
KESI YA MAUAJI KANISANI: DED ITIGI NA WENZAKE WAOMBA UPELELEZI UHARAKISHWE

> DED Luhende na wenzake 6 wamewasilisha ombi hilo Mahakamani kupitia Wakili Victoria Revocati

> Wajibiwa ni mapema mno kulalamikia upelelezi wa kesi ya mauaji

Soma => https://jamii.app/KesiDEDItigiUpelelezi
NIDA: ASILIMIA 80 YA WATANZANIA HAWANA VYETI VYA KUZALIWA

> Wengi ni Wananchi waishio Tanzania Bara ambao hawasajiliwa wala kuwa na vyeti vya kuzaliwa

> Aidha, kwa upande wa waliosajiliwa na kuwa na vyeti hivyo ni asilimia 13.4%

Zaidi, soma => https://jamii.app/NIDAVyetiKuzaliwa
KIAMBU, KENYA: WAKAMATWA NA MASANDUKU YENYE FEDHA BANDIA

> Jeshi la Polisi linawashikilia Bi. Nancy Muthori na Joseph Muhayo baada ya kuwakamata wakiwa na masanduku hayo

> Wamekamatwa katika Mtaa wa Ruiru wanakoishi

Zaidi, soma => https://jamii.app/FedhaBandiaKiambu

#JFLeo