JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI KUTOONGEZA VIWANGO VYA USHURU KWA CHINA

> Rais Donald Trump amesema hatotangaza viwango vipya ya ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya Dola Bilioni 200

> Ilitarajiwa kuongeza ushuru kutoka 10% hadi 25%, Machi Mosi

Soma - https://jamii.app/UsTarrifChineseGoods
#JFInternational
KAGERA: KESI YA WALIOUA WATU WANNE KWA KUWAKATA MAKOROMEO YAUNGURUMA

> Kesi hiyo inawakabili Alyu Hassan, NgesellaJoseph na Rashid Athumani(aliyekamatwa na simu aina ya Itel iliyokuwa inamilikiwa na mmoja ya watu waliouawa)

Zaidi, soma => https://jamii.app/KesiMauajiKagera

#JFLeo
DODOMA: WATUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

> Watuhumiwa 5 wa uhujumu uchumi wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka 19 likiwemo la kughushi risiti za EFD na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 700

Soma > https://jamii.app/KesiUhujumuDom
#JFLeo
KENYA: AMUUA KAKA YAKE KWASABABU YA SURUALI

> Mwanafunzi wa darasa la saba(16) anashikiliwa na Polisi baada ya kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu wakati wakigombana

> Mtuhumiwa anadaiwa kuvaa suruali ya kaka yake na kugoma kuifua

Soma - https://jamii.app/BrotheKillsBrother
#JFInternational
MSANII R KELLY AACHIWA KWA DHAMANA

> Nyota wa R&B, R Kelly (52) ameachiwa huru kutoka gerezani Chicago Marekani baada ya kulipa dhamana ya kiasi cha dola 100,000

> Amekana mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake wanne

Soma - https://jamii.app/RKellyFreeBail
#JFSanaa
MISRI: ADHABU YA KIFO YAGUBIKWA NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

> Wataalam wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wamelaani kitendo cha kuteswa na kuuawa kwa wanaume 9 nchini Misri

> Walihukumiwa hukumu ya kifo na Mahakama

Soma - https://jamii.app/DeathPenaltyEgypt
#JFInternational
NIGERIA: UPINZANI WAANZA KUPINGA MATOKEO YA URAIS

> Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria PDP kimesema hakitambui matokeo ya urais yanayotangazwa na Tume ya Uchaguzi yanaoonesha kuwa Rais Muhamadu Buhari anaongoza kwa kura

Soma - https://jamii.app/PDPVsResults
#JFInternational
UKEREWE: MVUA YAUA WAWILI NA KUHARIBU NYUMBA 16

> Watoto wawili wa familia moja wamefariki huku watu 77 wakazi wa Kijiji cha Mibungonanakwekwe Mwanza, wakikosa makazi baada ya nyumba zao 16 kubomolewa kwa mvua iliyoambatana na upepo mkali

Soma - https://jamii.app/MvuaYauaUkerewe
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN AJIUZULU

> Mohammad Javad Zarif ametangaza kujiuzulu kwake kupitia akaunti yake ya Instagram

> Zerif alihusika kikamilifu ktk mpango wa kupunguza matumizi ya nyuklia wa Iran uliosainiwa mwaka 2015

Soma => https://jamii.app/ZerifResigns

#JFInternational
YA KUFAHAMU KUHUSU BETRI YA SIMU AU TABLET

> Betri yako ikiwa na ujazo mkubwa basi kuna uwezekano mkubwa wa simu yako kukaa na chaji sana. Ujazo wa betri ya simu unapimwa kwa Milli Ampere Hour au kwa kifupi MAH

> Uimara wa betri unatokana na seli zilizotumika kutengenezea betri husika. Seli imara zinaruhusu kuchajiwa mara nyingi bila kuharibika

> Ni vyema ukitaka betri imara ununue kwenye makampuni yanayojulikana na wale wanaonunua Power bank hii pia inawahusu

Soma - https://jamii.app/UfahamuBetriSimu
#JFTeknolojia
HATARI ANAZOWEZA KUKUTANA NAZO MTOTO MTANDAONI

> Maudhui yasiyofaa kutokana na uwepo maudhui chungu nzima kuanzia nyimbo za ibada hata filamu za utupu

> Kufanya mawasiliano na watu wasiofaa. Wapo watu wasio-waaminifu ambao wanatafuta watoto wadogo kuwalaghai ama kuwarubuni

> Mitandao inaweza kumuharibia mwanao sifa au kitabia kwa kupenda kuwa maarufu na umaarufu huwafanya watoto wapige picha za ajabu na kuweka mtandaoni

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HatariMtandaoMtoto
#JFMahusiano
MBEYA: BAADA YA KUKAA MOCHWARI KWA MIEZI 8, FAMILIA YAKUBALI KUUZIKA MWILI WA KIJANA WAO

> Familia ya kijana Frank Kapange imekubali kuuchukua mwili wake baada ya kuamuliwa na Mahakama

> Mwili huo umekaa mochwari kwa miezi 8 na siku 22

Soma > https://jamii.app/MwiliFrankKapange

#JFLeo
AFRIKA KUSINI: MCHUNGAJI ALIYEJINASIBU KUFUFUA MTU, KUSHTAKIWA

> Wakurugenzi wa Makampuni 3 ya mazishi wasema watamshtaki mchungaji Lukau kwa kuwadanganya

> Walilaghaiwa na wasaidizi wa mchungaji huyo hadi na wao wakashiriki

Soma > https://jamii.app/LukauSaga

#JFInternational
ELIMU YA URAIA: JE, NINI KITATOKEA IWAPO ASKARI POLISI ATAKUNYIMA DHAMANA?

> Iwapo Askari Polisi atakunyima dhamana ni lazima auweke uamuzi wake katika maandishi na aeleze sababu za kukunyima dhamana

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
KENYA: AKAMATWA KWA KUMTEKETEZA KWA MOTO MKEWE

> Alianza kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumteketeza kwa moto

> Wawili hao walikuwa ktk mgogoro tangu Mwanaume huyo arejee kutoka Marekani mwezi mmoja uliopita

Soma > https://jamii.app/EldoretMumeAua

#JFLeo
UCHUMI: SERIKALI YAJIPANGA KUNUNUA NDEGE YA MIZIGO

> Serikali imesema ndege hiyo ya mizigo itatumika kusafirisha mazao yanayoharibika kwa haraka(mandunda & mboga) kwenda nje ya nchi

> Serikali yaanza kusaka masoko ya mazao hayo

Zaidi, soma => https://jamii.app/TanzaniaNdegeMizgo

#JFUchumi
TANZIA: RUGE MUTAHABA AFARIKI DUNIA

> Mkurugenzi huyo wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu

> Rais Magufuli atuma salamu za pole

Zaidi, soma => https://jamii.app/RIPRuge

#RIPRuge
HADHARA CHARLES NJEJE MWANAMKE MPIGA DANADANA ALIYEMKUNA RAIS TRUMP

> Moja ya video yake aliyorekodiwa akiwa nchini Malawi imesambaa kwenye mitandao hadi kumfikia Rais wa Marekani, Donald Trump

> Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika "Amazing" akimanisha 'Inashangaza'

#JFMichezo
UFAHAMU KUHUSU CHAJA ZA SIMU

> Umeshawahi kutumia chaja moja ikawa inachaji simu upesi na nyengine ikawa inachaji kidogo dogo?

> Hili linatokana na kuchajia chaja ambayo ina Ampere ndogo. Ampere ndio inayokujulisha kiasi gani cha umeme kinaingia kwenye betri na kifupi chake ni herufi A

> Kabla hujanunua chaja kwanza angalia betri yako inataka Ampere ngapi

Zaidi, soma - https://jamii.app/UfahamuChajaSimu
#JFTeknolojia
UFAHAMU KUHUSU CHAJA ZA SIMU

> Umeshawahi kutumia chaja moja ikawa inachaji simu upesi na nyengine ikawa inachaji kidogo dogo?

> Hili linatokana na kuchajia chaja ambayo ina Ampere ndogo. Ampere ndio inayokujulisha kiasi gani cha umeme kinaingia kwenye betri na kifupi chake ni herufi A

> Kabla hujanunua chaja kwanza angalia betri yako inataka Ampere ngapi

Zaidi, soma - https://jamii.app/UfahamuChajaSimu
#JFTeknolojia