JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MANCHESTER CITY IMEFANIKIWA KUTETEA UBINGWA WA CARABAO CUP

- Imefanikiwa kuchukua ubingwa huo baada ya kuigaragaza klabu ya Chelsea kwa penati 4-3

- Klabu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana na kusababisha kwenda hatua hiyo ya matuta
KONDOA, DODOMA: WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAUAWA

> Wameuawa kwa kupigwa na Wananchi wa kijiji cha Kinyasi baada ya kuvamia kituo cha mafuta

> Walifanya uporaji wa zaidi ya shilingi milioni kumi katika kituo hicho

Zaidi, soma => https://jamii.app/MajambaziKondoa

#JFLeo
SAUDI ARABIA: BINTI MFALME ACHAGULIWA KUWA BALOZI

> Saudi Arabia imemtangaza binti mfalme, Rima binti Bandar al-Saud kuwa balozi wake nchini Marekani, akiwa ni mwanamke wa kwanza kuwa balozi wa ufalme huo

Soma - https://jamii.app/FemaleAmbassadorUS
#JFInternational
WASIOTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KWENYE MALIPO WAPEWA ONYO

> Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amezitaka Taasisi zote za Serikali kutumia mfumo wa malipo wa kielektroniki(GePG) na watakaoshindwa, watachukuliwa hatua za kisheria

Soma https://jamii.app/OnyoWasiotumiaGePG
GARI LAKAMATWA LIKISAFIRISHA SAMPULI YA DHAHABU MWANZA

> Kamati ya ulinzi na usalama, inalishikilia Fuso lililokuwa likisafirisha shehena ya ndoo 226 zenye sampuli za miamba ya madini 883 mali ya Mgodi wa GGM kutoka Mkoani Geita kwenda Mwanza

Soma https://jamii.app/FusoMadiniLakamatwa
INDIA: WATU 145 WAFARIKI BAADA YA KUNYWA POMBE YENYE SUMU

> Takribani watu 145 wamefariki baada ya kunywa pombe yenye sumu, Kaskazini Mashariki mwa India huku zaidi ya 200 wakilazwa

> Tukio limetokea ktk miji ya Golaghat na Jorhat

Soma https://jamii.app/AssamHoochTragedy
#JFInternational
FAHAMU CHANZO CHA KUPATA MAGONJWA YA MOYO

> Inakadiriwa kwamba watu takriban milioni 17.5 hufariki kila mwaka kwa magonjwa hayo ya moyo

> Kutozingatia kanuni za ulaji bora, ni moja ya mambo yanayoongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya moyo

> Kuwa na uzito uliozidi au kuwa na unene uliopitiliza pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo

Fahamu zaidi - https://jamii.app/VisababishiMagonjwaMoyo
#JFAFYA
JAMHURI YAIOMBA MAHAKAMA ITOE HATI YA KUKAMATWA LISSU, MAHAKAMA YAGOMA KUMFUTIA DHAMANA

> Serikali imewasilisha maombi hayo ikidai Lissu hayupo hospitali tena, anazunguka tuu

> Mahakama imesema kufanya hivyo ni kukosa utu na Ubinadamu

Soma > https://jamii.app/LissuVsJamhuri
MABADILIKO YA NJIA KATIKA MAKUTANO YA BARABARA UBUNGO

> Wizara ya Ujenzi inawajuza wananchi na watumiaji wa Barabara za Morogoro, Mandera na Sam Nujoma mabadiliko ktk njia

> Inawataka kufuata mchoro uliotolewa na maelekezo ktk eneo husika

Soma - https://jamii.app/MabadilikoNjiaUbungo
MOROGORO: WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

> Waliofikishwa Mahakamani ni Wabunge Peter Lijualikali(Kilombero) na Susan Kiwanga(Mlimba) pamoja na Wananchi 7

> Walikamatwa Jumatano iliyopita katika Kijiji cha Sofi(Malinyi)

Soma > https://jamii.app/WabungeMahakamaMoro

#JFLeo
YA KUFAHAMU KUHUSU KILIMO CHA UFUTA

> Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi

> Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi

> Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi

> Kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/KilimoUfuta
#JFKilimo
TAKUKURU YAOMBA KUMUHOJI MKURUGENZI WA UDART

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuhoji Mkurugenzi wa Mradi wa UDART, Robert Kisena (46) na wenzake wawili

> Mahakama imeridhia ombi hilo

Soma - https://jamii.app/TakukuruKumuhojiKisena
SHILINGI 300 ZINAZOTOZWA KITUO CHA MABASI UBUNGO ZINAFANYA KAZI GANI?

> Ndani ya JamiiForums kuna mada inayohoji matumizi ya fedha hizo ikiwa hali ya vyoo ni mbaya na hakuna sehemu ya kupumzikia abiria wala wanaokuja kuwapokea wapendwa wao

Soma > https://jamii.app/KeroUbungo

#JFHoja
JE, ASKARI POLISI LAZIMA ATEKELEZE KILA AMRI ANAYOPEWA NA MKUU WAKE WA KAZI?

> Ndiyo lakini Askari atakayetekeleza amri iliyokiuka haki za binadamu hataweza kuja kujitetea baadaye

> Utetezi wake utakataliwa na yeye binafsi kuwajibishwa

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
BANGLADESH YAZIMA TOVUTI 20,000 ZA MAUDHUI YA NGONO

> Serikali ya Bangladesh imezima takribani tovuti 20,000 zenye maudhui ya ngono na michezo ya kamari

> Mahakama Kuu iliamrisha tovuti za ngono kupigwa marufuku na kuzimwa

Soma - https://jamii.app/PornSitesBlocked
#JFInternational
MAREKANI KUTOONGEZA VIWANGO VYA USHURU KWA CHINA

> Rais Donald Trump amesema hatotangaza viwango vipya ya ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya Dola Bilioni 200

> Ilitarajiwa kuongeza ushuru kutoka 10% hadi 25%, Machi Mosi

Soma - https://jamii.app/UsTarrifChineseGoods
#JFInternational
KAGERA: KESI YA WALIOUA WATU WANNE KWA KUWAKATA MAKOROMEO YAUNGURUMA

> Kesi hiyo inawakabili Alyu Hassan, NgesellaJoseph na Rashid Athumani(aliyekamatwa na simu aina ya Itel iliyokuwa inamilikiwa na mmoja ya watu waliouawa)

Zaidi, soma => https://jamii.app/KesiMauajiKagera

#JFLeo
DODOMA: WATUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

> Watuhumiwa 5 wa uhujumu uchumi wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka 19 likiwemo la kughushi risiti za EFD na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 700

Soma > https://jamii.app/KesiUhujumuDom
#JFLeo
KENYA: AMUUA KAKA YAKE KWASABABU YA SURUALI

> Mwanafunzi wa darasa la saba(16) anashikiliwa na Polisi baada ya kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu wakati wakigombana

> Mtuhumiwa anadaiwa kuvaa suruali ya kaka yake na kugoma kuifua

Soma - https://jamii.app/BrotheKillsBrother
#JFInternational