JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI MKUU NCHINI NIGERIA KUFANYIKA KESHO

> Rais wa Nigeria, Muhamadu Buhari amewahimiza raia wa nchi hiyo kujitokeza kesho, Februari 23 ili kupiga kura ya kuchagua Rais na Wabunge

> Rais huyo anakabiliwa na ushindani kutoka kwa mfanyabiashara, Atiku Abubakar

#JFInternational
MAPENZI: UKIONA DALILI HIZI TAMBUA MWANAUME HUYO SI MUOAJI

> Katika mahusiano wengi hujikuta wamepoteza muda kwa kutojua au kutabiri iwapo wenza wao hasa wa kiume kama ni wa kudumu au wapita njia

> Ndani ya JamiiForums kuna uchambuzi wa dalili mbalimbali ambazo yawezekana zikabainisha iwapo Mwanaume si muoaji

Soma => https://jamii.app/DaliliSiMuoaji
RAIA WA ETHIOPIA AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili jela, Gashahuni Degu(21) baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila kibali

Zaidi, soma https://jamii.app/RaiaEthiopiaJela
BABATI, MANYARA: AJINYONGA HADI KUFA KWA TAULO

> Ni Mwanafunzi Mathayo Ezekiel(11) wa darasa la 5 katika shule ya msingi Mikiroy

> Sababu bado haijafahamika ila alijinyonga nyumbani kwao alipotoka shule wakati wazazi wake hawapo

Soma https://jamii.app/MwanafunziAfarikiKujinyonga
CHICAGO, MAREKANI: KESI YA R KELLY YACHUKUA SURA MPYA

> Kesi ya Mwanamuziki huyo imechukua sura mpya baada ya kushtakiwa kwa makosa mapya

> Anatuhumiwa kwa makosa 10 ya unyanyasaji dhidi ya Watoto aliyoyatenda mwaka 1995/6

Soma => https://jamii.app/RKellyCharges

#JFCelebrity
KENYA: AJIRUSHA MBELE YA LORI BAADA YA KUGUNDUA KASALITIWA NA MPENZIWE

> Jamaa mmoja mjini Naivasha, amejitoa uhai kwa kujirusha mbele ya lori lililokuwa kwenye mwendokasi ktk barabara kuu ya Nakuru

> Chanzo ni kusalitiwa kimapenzi

Soma https://jamii.app/AjiuaKujirushaBarabarani
#JFInternational
BAADHI YA VIONGOZI WA DRC WAPIGWA MARUFUKU KUINGIA MAREKANI

> Marekani imetangaza kuwapiga marufuku kuingia Marekani baadhi ya viongozi wa DRC pamoja na familia zao kutokana na kujihusisha na ufisadi mkubwa ktk mchakato wa uchaguzi

Soma https://jamii.app/USSanctionsDRCOfficials
#JFInternational
SERIKALI YA SUDAN YAVUNJWA, HALI YA DHARURA YATANGAZWA

> Rais wa Sudan, Omar Al Bashir ametangaza kuivunja Serikali kuu ya nchi hiyo na Serikali 18 za majimbo

> Ametangaza hali ya dharura kwa mwaka 1 na Jeshi ndilo litasimamia nchi

Soma https://jamii.app/SudanStateEmergency
#JFInternational
KATIBU MKUU UN AIONYA VENEZUELA

> Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Antonio Guterres akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ameionya Serikali ya nchi hiyo kutokiuka haki za binadamu inapowadhibiti Waandamanaji

Soma > https://jamii.app/GuterresVsVenezuela

#JFInternational
DAR: HALIMA MDEE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

> Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA) aliitwa kuhojiwa ktk kituo cha Polisi Oysterbay kwa tuhuma za kutoa kauli ya kumkosea heshima Rais Magufuli

> Baada ya kuhojiwa Mdee amenyimwa dhamana

Soma > https://jamii.app/MdeeArrested
NIGERIA: BOKO HARAM WAFANYA JARIBIO LA KUVURUGA UCHAGUZI

> Mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulio la mabomu linalodaiwa kufanywa na kundi la Boko Haram

> Milipuko 13 ilisikika leo asubuhi

Soma - https://jamii.app/BokoHaramNigeria
#JFInternational
WAZIRI MKUU: MPAKA WA HOLILI HAUKO SALAMA, NJIA ZA PANYA ZIMEKITHIRI

> Amesema mpaka huo kati ya Tanzania na Kenya uliopo wilayani Rombo(Kilimanjaro) una njia nyingi za panya zinazotumiwa wahalifu kupitisha silaha na bidhaa za magendo

Soma > https://jamii.app/MajaliwaMpakaHolili

#JFLeo
BAADHI YA SIFA ZINAZOWASILISHWA ILI KUMJUA MTU ANAYEKUFAA KIMAPENZI

> Hatangoja kujua nini unahitaji kwa kuwa hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada

> Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe katika hali ya raha na shida pia

> Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali) na ataonesha kuthamini nafasi yako mbele ya wengine

Zaidi, soma - https://jamii.app/SifaMpenziKweli
#JFMahusiano
MICHEZO: Klabu ya Barcelona yainyuka Sevilla kwa mabao 4 kwa 2

> Mshambualiaji raia wa Argentina, Lionel Messi afunga mabao 3 maarufu kama 'hat-trick'

> Hii ni hat-trick ya 32 kwa Messi tangu aanze kuitumikia Klabu ya Barcelona ktk La Liga

> Messi amebakiza hat-trick 2 ili kuifikia rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga 34 akiwa na Real Madrid

#JFSports
WATAALAMU 9 WA ARDHI WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

> Watu 9, wataalam wa idara ya Ardhi wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni Wilayani Kilombero mkoani Morogoro

> Gari hiyo ilikuwa na watu 13

Soma - https://jamii.app/WataalamuArdhiWafariki
MTWARA: KOROSHO ZARUDISHWA KWA WAKULIMA ZIKIDAIWA HAZINA UBORA

- Zaidi ya tani 68 za korosho zimekataliwa kuingizwa kwenye maghala makuu ya TANECU ili ziuzwe

- Wakulima wamedai pamoja na kuzichambua na kuzianika zikubaliwe bado zimekataliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WakulimaWarudishiwaKorosho
KOCHA WA YANGA ASEMA ANAWEZA KUONDOKA MWISHO WA MSIMU HUU

- Kocha Mwinyi Zahera amesema anaweza kuondoka kutokana na Wanachama na Mashabiki kutompa ushirikiano

- Aidha, zipo tetesi zinazodai kuwa Kocha huyo anaenda kuifundisha klabu ya Azam

Zaidi, soma https://jamii.app/ZaheraAtishiaKuondoka
MKURUGENZI HALMASHAURI YA ROMBO APEWA SIKU 16 KUTOA TSH. MILIONI 114

- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Magreth John, apeleke fedha hizo katika kijiji cha Holili

- Ni 20% ya mauzo ya madini ya pozolana ambayo Wananchi wanadai hawajalipwa

Zaidi, soma https://jamii.app/FedhaMadiniHoliliKLM
SERIKALI: MFANYABIASHARA MDOGO ANAYEGOMA KUCHUKUA KITAMBULISHO ATALIPA KODI

> Yasema kama Tsh. 20,000/- zinaonekana nyingi wanaweza kulipa kwa awamu

> Viongozi waonywa kutotoa kitambulisho kabla ya mfanyabiashara kumaliza malipo kuepusha kutoroka

Zaidi, soma https://jamii.app/VitambulishoUmachingaVsKodi
RAIS WA KOREA KASKAZINI ATUMIA TRENI KWENDA KUKUTANA NA RAIS TRUMP

- Kim Jong Un anakwenda Vietnam kushiriki kikao chake cha pili na Rais wa Marekani, Donald Trump

- Kikao kitafanyika Februari 27 na Februari 28, 2019 katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi

Zaidi, soma https://jamii.app/Kim-TrumpSummit