JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MWALIMU MKUU ABAKA MJUKUU, BABA ABAKA MTOTO WAKE

> Jeshi la Polisi Mbeya, linamshikilia Mwalimu Alinani Mwakifuna(59) kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake wa miaka 15

> Samwel Msukila(22) anashikiliwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa miaka 9

Soma https://jamii.app/MwlBabaWabaka
KENYATTA: HAKUNA FEDHA ZA KUWALIPA WAUGUZI WANAOGOMA

> Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesisitiza kwamba hakuna fedha za kuwalipa wauguzi wanaogoma

> Asema Serikali ina mambo mengi ya kufanya na sio kuongezea wafanyakazi mishahara kila mwaka

Soma- https://jamii.app/NoSalaryIncreaseKE
KESI YA JAMHURI DHIDI YA JAMIIFORUMS: WASHTAKIWA WANA KESI YA KUJIBU

> Mkurugenzi wa JamiiForums na mwanahisa mwenza, Micke William wamekutwa na kesi ya kujibu ktk shauri namba 456, Mahakama ya Kisutu

> Kuanza kujitetea Machi 14 na 19

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiJamhuriVsJamiiForums
DAR: ASKARI MAGEREZA WAUA RAIA NA KUMJERUHI MAMAKE WAKIMDHIBITI MTUHUMIWA

> Neema Dominick amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Askari Magereza waliokuwa wakimdhibiti Mtuhumiwa (si marehemu) asitoroke katika Mahakama ya Kigamboni

Zaidi, soma => https://jamii.app/MagerezaRisasi
#JFLeo
VENEZUELA YAFUNGA MPAKA WAKE NA BRAZIL

> Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameamuru kufungwa kwa mpaka wa Kusini mwa nchi yake, ambao unaitenganisha na Brazil

> Hatua hii imeanza kutumika rasmi usiku wa kuamkia leo kwa saa za Venezuela

Soma - https://jamii.app/MaduroBlocksBrazil
ELIMU YA URAIA: JE, POLISI ANAWEZA KUMKAMATA MWENZAKE AKIFANYA UHALIFU?

> Askari wa Jesho la Polisi anayefahamu kuwa Polisi mwenzake anajihusisha na vitendo vya kijinai halafu akashindwa kuchukua hatua yoyote ile atakuwa anafanya makosa

Zaidi, soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
JINSI YA KUTENGENEZA BARAFU ZA KULA(ICE CREAM)

> Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na yachemshe, ongeza sukari na chumvi (ukipenda)

> Ongeza corn starch au ubuyu na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vizuri, chemsha kwa dk 8, kisha acha ipoe na ongeza ladha uipendayo

> Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu

Soma - https://jamii.app/KutengenezaIceCream
#JFMapishi
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO 19 KATIKA AJALI MKOANI SONGWE

> Ametuma salamu kwenda kwa familia zilizopoteza ndugu/jamaa ktk ajali iliyotokea Wilayani Mbozi

> Rais amezitaka mamlaka kuchunguza na kuchukua hatua

Soma > https://jamii.app/RaisPoleSongwe
ARUSHA: WAZEE WAPIGANA, KISA WIVU WA MAPENZI

> Bibi aliyejulikana kwa jina la Ester Taiko(64) amepigwa na Mumewe Christopher Shanguro(74) kwa tuhuma za kutoka nje ya ndoa

> Mzee Christopher anatuhumiwa kumpiga mkewe na kumwagia oili

Soma => https://jamii.app/UgoviVikongweArusha
KISUTU, DAR: WANAFUNZI 2 NA WATU WENGINE 6 WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

> Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuwakuta na hatia ya kuchoma Kituo cha Polisi Bunju A

> Halifani Mshengeli mwenye miaka 19 ni kati ya waliohukumiwa

Soma > https://jamii.app/HukumuMaishaBunju
ENGLAND: CHELSEA FC YAFUNGIWA KUSAJILI KWA MISIMU MIWILI

> Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) limeipiga marufuku klabu hiyo kufanya usajili ndani ya misimu 2 ijayo

> Pia imetakiwa kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 1.4

Soma => https://jamii.app/FIFAVsChelseaFC
JINSI YA KUTENGENEZA MWILI BILA KWENDA 'GYM'

> Anza na Pushap za Kawaida ila usikunje ngumi. Utaanza kwa kwenda juu chini hiyo ni 1, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara 4

> Fanya pushap za miguu ikiwa imeinuka. Unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe, ndoo au hata kwenye ngazi. Juu chini mara 20 na kurudia tena mara 4

Jifunze zaidi hapa - https://jamii.app/BodyBuildNoGym
#JFUtanashati
AKAMATWA NA POLISI KWA KUWALISHA WANANCHI NYAMA YA MBWA

> Mkazi wa kijiji cha Mitonji, Mkoani Mtwara, Dismasi Malikitu(kizito) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuwauzia wananchi nyama ya Mbwa huku akiwadanganya ni nyama ya mbuzi

Soma - https://jamii.app/MatataniNyamaMbwa
DRC: AJALI YAUA 18, DEREVA ADAIWA KUWA NI MTANZANIA

> Watu 18 wamepoteza maisha na 12 kujeruhiwa ktk ajali ya barabarani mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

> Taarifa zinasema dereva huyo (Mtanzania) alikuwa amelewa

Soma- https://jamii.app/18DeadCarAccident
#JFInternational
DODOMA: RAIA WA CHINA WAKAMATWA KWA KUSAMBAZA MASHINE ZA KAMARI KINYEMELA

> Wamekamatwa kwa tuhuma ya kusambaza takribani mashine 138

> Aidha, wanatuhumiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 1 kwa Polisi waliowakamata

Soma https://jamii.app/WachinaMashineKamari
UCHAGUZI MKUU NCHINI NIGERIA KUFANYIKA KESHO

> Rais wa Nigeria, Muhamadu Buhari amewahimiza raia wa nchi hiyo kujitokeza kesho, Februari 23 ili kupiga kura ya kuchagua Rais na Wabunge

> Rais huyo anakabiliwa na ushindani kutoka kwa mfanyabiashara, Atiku Abubakar

#JFInternational
MAPENZI: UKIONA DALILI HIZI TAMBUA MWANAUME HUYO SI MUOAJI

> Katika mahusiano wengi hujikuta wamepoteza muda kwa kutojua au kutabiri iwapo wenza wao hasa wa kiume kama ni wa kudumu au wapita njia

> Ndani ya JamiiForums kuna uchambuzi wa dalili mbalimbali ambazo yawezekana zikabainisha iwapo Mwanaume si muoaji

Soma => https://jamii.app/DaliliSiMuoaji
RAIA WA ETHIOPIA AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili jela, Gashahuni Degu(21) baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila kibali

Zaidi, soma https://jamii.app/RaiaEthiopiaJela
BABATI, MANYARA: AJINYONGA HADI KUFA KWA TAULO

> Ni Mwanafunzi Mathayo Ezekiel(11) wa darasa la 5 katika shule ya msingi Mikiroy

> Sababu bado haijafahamika ila alijinyonga nyumbani kwao alipotoka shule wakati wazazi wake hawapo

Soma https://jamii.app/MwanafunziAfarikiKujinyonga
CHICAGO, MAREKANI: KESI YA R KELLY YACHUKUA SURA MPYA

> Kesi ya Mwanamuziki huyo imechukua sura mpya baada ya kushtakiwa kwa makosa mapya

> Anatuhumiwa kwa makosa 10 ya unyanyasaji dhidi ya Watoto aliyoyatenda mwaka 1995/6

Soma => https://jamii.app/RKellyCharges

#JFCelebrity