JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BANGLADESH: AJALI YA MOTO YASABABISHA VIFO 70

> Moto mkali uliozuka usiku kwenye nyumba kadhaa ktk mji mkuu wa Dhaka nchini Bangladesh, umesababisha vifo vya takribani watu 70, hasa wanawake na watoto na wengine kadhaa kujeruhiwa

Soma - https://jamii.app/70DeadFireAccident
ELIMU YA URAIA: Askari Polisi anaweza kunilazimisha kukiri kosa?

> Mtuhumiwa akikataa kuongea ni wajibu wa Polisi kumfikisha Mahakamani ndani ya saa 24

> Maelezo ya kukiri kosa yatokanayo na kuteswa hayakubaliki kama ushahidi Mahakamani

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
WAZIRI ATENGUA KAULI KUHUSU UAGIZAJI WA SUKARI NJE

> Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametengua kauli yake kuhusu Sukari kutokuagizwa kutoka nje ya nchi na kuwataka wazalishaji kuendelea kuagiza bidhaa hiyo

> Alitoa zuio hilo Februari 12

Soma - https://jamii.app/VibaliSukariVyarejeshwa
MWANZA: MWANDISHI WA KAMPUNI YA MWANANCHI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI

> Jonathan Musa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya kumpiga picha Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(RCO) wa Mwanza, Faustine Mafwere

Zaidi, soma => https://jamii.app/MwandishiMwananchiMwanza

#JFLeo
MWANAFUNZI AFARIKI KWA KUJIPIGA RISASI KICHWANI

> Jasmini Ngoye (18), mwanafunzi wa kidato cha nne Manispaa ya Morogoro, amekutwa amekufa baada ya kujipiga risasi ya kichwa Februari 19 huku chanzo cha kifo kikidaiwa kuwa ni msongo wa mawazo

Soma - https://jamii.app/MwanafunziAjipigaRisasi
MGOGORO WA ARDHI: MMOJA AJERUHIWA KWA MKUKI NA MABOMA ZAIDI YA 20 YATEKETEZWA KWA MOTO

> Tukio hilo limetokea katika eneo la Mferejini lililopo mpakani mwa Wilaya ya Arumeru na Monduli

> Mgogoro huo umewahusisha wakulima na wafugaji

Soma > https://jamii.app/MgogoroAruMonduli

#JFLeo
OHIO, MAREKANI: AMSHAMBULIA WAKILI WAKE BAADA YA KUFUNGWA MIAKA 47 JELA

> David Chislton aliyehukumiwa kifungo cha miaka 47 jela amemshambuliwa Wakili Aaron Brockler na kumvunja pua

> Asema ameshindwa kumtetea

Zaidi, soma => https://jamii.app/OhioManAttacksHisLawyer

#JFInternational
UNAKUMBUKA NYIMBO GANI ZILIZOTAMBA KIPINDI CHA NYUMA

> Kila kukicha wasanii wa Bongo Fleva wanaongezeka na mahadhi ya nyimbo zao hubadilika kila siku

> Tujikumbushe nyimbo za Bongo Fleva zilizotamba kipindi cha nyuma na nyingine bado zinabamba hata sasa

Tembelea - https://jamii.app/BongoFlevaKale
#JFBurudani
👍1
KONDOMU MILIONI 1 ZIKO NJIANI KUELEKEA MAFINGA & NJOMBE

> Mafinga & Njombe uhitaji ni mkubwa, Serikali imelazimika kupeleka mipira hiyo kwa dharura

> Mwisho wa mwezi kondomu milioni 9 zitaingia nchini na mwezi Machi zitaingia Millioni 90

Soma > https://jamii.app/KondomuNjombe
RPC MBEYA ATHIBITISHA KUMHOJI 'SUGU' KWA KUTOA KAULI YA UCHOCHEZI

> Kamanda wa Polisi Ulrich Matei amethibitisha kumuhoji Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kwa kukashfu vitambulisho vya Serikali

Zaidi, soma => https://jamii.app/SuguVsRPCMbeya
CHINA YAIUNGA MKONO TANZANIA KWA KUMFUNGA MALKIA WA MENO YA TEMBO

> Serikali ya China imetangaza kuiunga Mkono Tanzania baada ya kumhukumu Yang Fenglan kifungo cha miaka 17 kwa hatia ya kuua na kusafirisha meno ya Tembo 700 kwenda nje

Soma => https://jamii.app/ChinaBacksTanzania
👍1
PROFESA JUMA KAPUYA: KUBALINI MATOKEO ACHENI KUSEMA SEMA

> Profesa Juma Kapuya(74) ametoa kauli hiyo baada ya ndoa yake aliyofunga na Mwajuma Mwiniko(25) kuzua mjadala

> Amehoji, watu walitaka aoe Mwanamke anayefanana na bibi yake?

Soma => https://jamii.app/NdoaYaProfKapuya
MALAWI: MGOMBEA URAIS AMTEUA MAMA YAKE KUWA MGOMBEA MWENZA

> Chikomeni Chirwa(41) amempendekeza Mama, Niness Kayengo(akishinda atakuwa Makamu wa Rais)

> Akichaguliwa atahalalisha kilimo cha bangi(anaamini kitatengeneza ajira milioni 10)

Soma > https://jamii.app/ChikomeniMalawi
JOSEPH MBILINYI 'SUGU' AACHIWA KWA DHAMANA

> Amepewa dhamana iliyohusisha bondi ya shilingi milioni 5. Mbunge huyo wa Jimbo la Mbeya Mjini ametakiwa kwenda kuripoti kesho saa 4:00 asubuhi

> Anatuhumiwa kwa kutoa kauli ya uchochezi

Soma > https://jamii.app/SuguVsRPCMbeya
Miili mingi imekwama na mingine kusagika. Taarifa zaidi zitafuata
MWALIMU MKUU ABAKA MJUKUU, BABA ABAKA MTOTO WAKE

> Jeshi la Polisi Mbeya, linamshikilia Mwalimu Alinani Mwakifuna(59) kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake wa miaka 15

> Samwel Msukila(22) anashikiliwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa miaka 9

Soma https://jamii.app/MwlBabaWabaka
KENYATTA: HAKUNA FEDHA ZA KUWALIPA WAUGUZI WANAOGOMA

> Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesisitiza kwamba hakuna fedha za kuwalipa wauguzi wanaogoma

> Asema Serikali ina mambo mengi ya kufanya na sio kuongezea wafanyakazi mishahara kila mwaka

Soma- https://jamii.app/NoSalaryIncreaseKE
KESI YA JAMHURI DHIDI YA JAMIIFORUMS: WASHTAKIWA WANA KESI YA KUJIBU

> Mkurugenzi wa JamiiForums na mwanahisa mwenza, Micke William wamekutwa na kesi ya kujibu ktk shauri namba 456, Mahakama ya Kisutu

> Kuanza kujitetea Machi 14 na 19

Zaidi, soma https://jamii.app/KesiJamhuriVsJamiiForums
DAR: ASKARI MAGEREZA WAUA RAIA NA KUMJERUHI MAMAKE WAKIMDHIBITI MTUHUMIWA

> Neema Dominick amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Askari Magereza waliokuwa wakimdhibiti Mtuhumiwa (si marehemu) asitoroke katika Mahakama ya Kigamboni

Zaidi, soma => https://jamii.app/MagerezaRisasi
#JFLeo