JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: ANA HALI MBAYA BAADA YA KUAMUA KUJITAHIRI KWA WEMBE

> Katheya Riungu(40) amelazwa Hospitali ya Tharaka-Nithi akiwa ktk hali mbaya baada ya kujitahiri kwa wembe nyumbani kwake

> Alichukua hatua hiyo kwa kuogopa fedheha kwa marafiki

Soma - https://jamii.app/MeAjitahiriWembeKE
MWANAMKE AUA MTOTO WA MWENZIE KWASABABU YA WIVU WA MAPENZI

> Paskazia Andrew(17) anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Shinyanga kwa kumuua kwa kumkata panga kichwani Kashindye Mgemagiko

> Inadaiwa ni mtoto wa mumewe kwa mwanamke mwingine

Soma - https://jamii.app/AuaMtotoPanga
KENYA: MAHAKAMA YASEMA SIO KOSA KUENDESHA GARI UKIWA UMEKUNYWA POMBE

> Mahakama ya Kiambu imetoa hukumu ikieleza kuwa, kuendesha gari ukiwa amekunywa pombe sio kosa kama unaweza kukidhibiti vyema chombo hicho cha moto

Zaidi, soma -
-https://jamii.app/DrunkDrivingNotOffensive
ETHIOPIA KUWASAIDIA RAIA WAKE WALIOKAMATWA NCHINI

> Raia 541 wamekwama nchini baada ya kukamatwa kwa makosa ya uhamiaji haramu

> Serikali ya nchi hiyo imepanga kuwasaidia kupata nyaraka za kusafiria ili warejee nchini kwao

Soma => https://jamii.app/Raia541EthipiaTz
WAZIRI MKUU WA UHISPANIA ATANGAZA UCHAGUZI WA HARAKA

> Pedro Sanchez ametangaza uchaguzi Mkuu utakaofanyika Aprili 28, 2019 badala ya Juni, 2020 kama ilivyotarajiwa

> Ni baada ya Serikali yake kushindwa ktk kura ya bajeti Bungeni

Soma - https://jamii.app/SanchezCallsSnapElection
VYAKULA VYA KULA AU KUVIEPUKA KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

> Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali

> Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine vinaweza kuleta matatizo

> Wagonjwa wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats)

Zaidi, soma - https://jamii.app/VyakulaVidondaTumbo
MAHAKAMA KUU YATENGUA UTEUZI WA WADHAMINI WA CUF KAMBI YA PROF. LIPUMBA

> Uamuzi umetolewa leo na Jaji Dkt. Benhajj Masoud, pia amesema majina ya wajumbe waliopendekezwa na kambi ya Katibu Mkuu Maalim Seif nao hawana na sifa ya kuteuliwa

Soma > https://jamii.app/WajumbeBodiCUF
ELIMU KUHUSU JESHI LA POLISI: Katika nchi ya demokrasia, Jeshi la Polisi siyo wakala wa serikali iliyopo madarakani bali ni chombo cha kuwalinda raia na mali zao.

> Polisi wanajukumu la kumlinda na kumwangalia kila mmoja wetu

Soma >https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
IJUE SHERIA: Je, ni kazi ya Polisi kumtia hatiani mtuhumiwa? Hapana hii sio kazi yao

> Wanawajibika kukamata Watuhumiwa, kufanya uchunguzi na kuwapeleka Mahakamani pamoja na ushahidi ili Mahakama iweze kufanya uchambuzi na kutoa hukumu

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
MSUMBIJI: MTOTO WA RAIS MSTAAFU AKAMATWA KWA KASHFA YA RUSHWA

> Ndambi Guebuza, mtoto wa Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Guebuza amekamatwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kashfa ya rushwa ya dola bilioni 2 za deni la Taifa

Soma https://jamii.app/PresidentSonArrestedCorruption
BODI YA FILAMU YAMRUHUSU WEMA SEPETU KUENDELEA NA SANAA

> Alipewa adhabu ya kutoendelea na shughuli za sanaa baada ya kusambaza maudhui ya ngono mtandaoni mwaka 2018

> Imemfungulia adhabu hiyo kwa kuwa amefanya aliyoagizwa kwa zaidi ya 75%

Soma - https://jamii.app/WemaSepetuAsamehewaTFB
MBOWE NA MATIKO WARUDISHWA MAHABUSU KUSUBIRI RUFAA YA DPP

> Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe(Mbunge wa Hai) na Esther Matiko(Mbunge wa Tarime Mjini) warejeshwa gerezani kusubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu maombi yao ya dhamana

Zaidi, soma => https://jamii.app/MboweMatikoVsDPP
SUDAN KUSINI: GESI ILIYOTUMIKA KUWATAWANYA WAANDAMANAJI YASABABISHA KIFO

> Mwanaume muuza matunda ndani ya Mji wa Khartoum amefariki kwa kile kinachoelezwa kuwa alivuta gesi ya kutoa machozi iliyotumika kuwatawanya waandamanaji

Soma =>https://jamii.app/GesiKifoSudan

#JFInaternational
UINGEREZA: WABUNGE 7 WA CHAMA CHA LABOUR WAJIUZULU

> Wabunge saba kutoka Chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza (Labour) wamejiuzulu kutokana na kutokukubaliani kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya na vita dhidi ya ubaguzi

Soma - https://jamii.app/7PMsResignUK
#JFInternational
AFYA: UFAHAMU UGONJWA WA PUMU

> Ugonjwa wa pumu huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu zinazojulikana kama ''bronchioles''

> Kupitia JamiiForums, ipo mada inayochambua zaidi kuhusu ugonjwa huu

Zaidi, soma > https://jamii.app/UgonjwaPumu

#JFAfya
TANZANIA YATAJWA KUWA NA KIWANGO KIKUBWA CHA KODI KATIKA SEKTA YA MADINI

> Taarifa hii imetolewa na taasisi inayoshughulika na usimamizi wa rasilimali za asili na maendeleo endelevu dunia (NRGI)

> Imeleeza kuwa kiwango cha kodi kwa Tanzania ni asilimia 74

Soma => https://jamii.app/KodiMadiniTz
IJUE SHERIA: Je, naweza kumwita Askari Polisi wakati wowote ninapohitaji?

> Unapaswa kuwaita Askari Polisi kwa malalamiko au taarifa zinazohusu uhalifu muda wowote hata usiku wa manane

> Unaweza kuwaita Polisi kwa njia ya simu namba 112

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi
#JFCivic
HALI YA RUGE MUTAHABA: MSAADA WA HALI NA MALI WAHITAJIKA TOKA KWA YEYOTE ATAYEGUSWA

> Mbaki Mutahaba(mdogo wa Ruge Mutahaba) amesema gharama za matibabu ni kubwa mno

> Kwa atayeguswa kuchangia matibabu ya Ruge Mutahaba wameombwa kufanya hivyo kupitia namba 0752 222 210

#JFLEO
WATUMISHI 3 WIZARA YA MADINI KUSIMAMISHWA KAZI

> Waziri wa Madini, Doto Biteko amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuwasimamisha na kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 3 kwa kugawa leseni za uchimbaji wa madini bila kufuata utaratibu

Soma https://jamii.app/WatumishiKusimamishwaKazi
KENYA: MBARONI KWA KUTAKA KUMTOROSHA MTOTO HOSPITALINI

> Bonface Murage Wangechi (22) amekutwa hatiani kwa kutaka kumtorosha mtoto wake baada ya kushindwa kulipa fedha za matibabu kwenye Hospitali ya Taifa, kiasi cha Ksh 56,937

Soma - https://jamii.app/ArrestedHospitalBill