JamiiForums
53K subscribers
34.3K photos
2.41K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SAA 5 KABLA YA UCHAGUZI NIGERIA: TUME YATANGAZA KUAHIRISHA KWA WIKI MOJA

> Uchaguzi wa Rais na Wabunge umesogezwa mbele hadi Jumamosi tarehe 23 mwezi huu

> Aidha, uchaguzi wa Magavana umepangwa kufanyika tarehe 9 ya mwezi Machi 2019

Soma => https://jamii.app/NigeriaElectionDelayed
WANAWAKE WENYE MIAKA 30+ HATARINI KUUGUA SARATANI

> Breast Cancer Now limefadhili utafiti uliobaini kwamba, Saratani hutambulika mapema kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 35 hadi 39 wanapofanyiwa uchunguzi kila mwaka(mammograms)

Zaidi, soma - https://jamii.app/WomenVsBreastCancer
#JFAfya
MISRI: MCHAKATO WA RAIS ABDEL FATTAH KUKAA MADARAKANI HADI 2034 WAANZA

> Mchakato huo utamuwezesha rais Abdel Fattah al-Sisi kukaa madarakani hata baada ya muhula wake kuisha 2022

> Wabunge 485 kati ya 596 wameunga mkono mabadiliko hayo

Soma => https://jamii.app/MisriRais2034

#JFInternational
KAYA 2,086 ZAKUMBWA NA MAFURIKO MTWARA

> Wananchi wa vitongoji vya Migombani-Mbuyuni na Mchangani wamelazimika kuyahama makazi yao kufuatia kufurika kwa maji ktk Mto Ruvuma

> Kumetokea uharibifu wa zaidi ya Ekari 3,014 za Mpunga na Mahindi

Soma - https://jamii.app/Kaya2086MafurikoMTR
ARUSHA: MKURUGENZI WA KAMPUNI YA OBC AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Siku 3 zilizopita Serikali iliagiza kukamatwa kwa ndugu, Isack Mollel(59) Mkurugenzi wa Ortello Business Cooperation, kwa tuhuma za kuajiri Wafanyakazi 10 wa kigeni bila vibali

Soma => https://jamii.app/MkurugenziOBCMahakamani
SERIKALI YAAHIDI KUSHIGHULIKIA SUALA LA KIJANA ALIYEPIGWA RISASI NA POLISI, ARUSHA

> Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola

> Richard Peter, alipigwa risasi na Askari Polisi ktk eneo la Kituo cha Polisi, Usa River

Soma > https://jamii.app/SerikaliVsMauajiArusha
Mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0

> Goli pekee la Simba SC limefungwa na Meddie Kagere kunako dakika ya 71 ya mchezo huo

#JFLeo #JFMichezo
MAREKANI: WATANO WAFARIKI KWENYE MAJIBIZANO YA RISASI

> Watu 5 wameripotiwa kufariki na askari 5 kujeruhiwa ktk makabiliano ya risasi yaliyotokea ktk jimbo la Illinois nchini Marekani

> Aliyeendesha shambulizi hilo naye ameuawa

Soma - https://jamii.app/5KilledGunmanUS
#JFInternational
AKIUA KICHANGA KWA KUJIFUNGULIA KWENYE NDOO ILIYOJAA MAJI

- Polisi mkoani Manyara inamshikilia Ramla Omary(23) kwa kutupa kichanga shimoni baada ya kukiua alipokuwa anajifungua

- Inaelezwa Ramla amefanya hivyo kwa madai kuwa ana maisha magumu

Zaidi, soma https://jamii.app/AjifunguliaNdooMNYR
SIMIYU: MWILI WAOKOTWA UKIWA UMETOLEWA BAADHI YA VIUNGO

- Mwili wa Mmwanamke ambaye jina lake halijafahamika umeokotwa katika kijiji cha Lamadi Wilayani Busega

- Umekutwa katika nyumba chakavu ukiwa umekatwa sehemu za siri na titi la kushoto

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiMwanamkeSMY1
UFARANSA: MAANDAMANO YAFANYIKA KWA MIEZI MITATU MFULULIZO

- Waandamanaji wanaovaa vizibao vya njano na kupinga sera za kiuchumi za Rais Macron waliandamana jana

- Takribani Waandamanaji 41,500 waliandamana ikiwa ni wikiendi ya 14 mfululizo

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamaniVisibaoNjano
MWANZA: POMBE KALI ZILIZOKUWA HAZIJALIPIWA USHURU ZAKAMATWA

- TRA imekamata katoni 10,786 za pombe ya Shimha Waragi zilizokuwa ziingizwe sokoni

- Kiwanda kinachotengeneza pombe hizo kinadaiwa kilitaka kukwepa ushuru wa Tsh. Milioni 38.6

Zaidi, soma https://jamii.app/PombeKaliMwanzaTRA
UGONJWA WA VITILIGO: CHANZO, DALILI NA TIBA

> Husababishwa na kinga za mwili kujishambulia (autoimmune reaction) na kuathiri seli za melanocytes zinazotengeza rangi ya ngozi na kusababisha mabaka meupe katika baadhi ya maeneo ya mwili

Zaidi, soma https://jamii.app/UgonjwaVitiligo
TUME YA UCHAGUZI NIGERIA YAKANA KUINGILIWA KISIASA

- Yasema sababu ya kuahirisha uchaguzi si ya kisiasa wala kiusalama bali mazingira mabaya yaliyochelewesha ndege zilizobeba vifaa

- Aidha, sababu nyingine ni ofisi 3 za Tume kuungua kwa moto

Zaidi, soma https://jamii.app/NigeriaElectionDelayed
BAADA YA KIPIGO, KOCHA WA YANGA AISIFU SIMBA

- Kocha Mwinyi Zahera amekisifu kikosi cha Simba na kusema Wachezaji wa Yanga walikosa ubunifu jana

- Amesema Wachezaji wake ni wazuri ila wanakosa suluhisho la namna ya kucheza na kufunga magoli

Zaidi, soma https://jamii.app/ZaheraAikubaliSimba
PAPA FRANCIS AMVUA MADARAKA KADINALI KWA KUMBAKA MTOTO

- Kadinali wa zamani, Theodore McCarrick(88) amevuliwa madaraka ikiwa ni miaka 50 tangu atuhumiwe

- Amepatikana na hatia ya kuvunja amri ya 6 kwa kufanya uzinzi na mtoto na watu wazima

Zaidi, soma https://jamii.app/UbakajiKadinaliMadaraka19
ZIMBABWE: WATU 24 WAFARIKI BAADA YA MACHIMBO YA MADINI KUJAA MAJI

- Ni baada ya migodi miwili ya dhahabu kukumbwa na mafuriko Ijumaaa kufuatia bwawa la karibu kuvunja kingo zake

- Watu wengine 8 wameokolewa huku wengine wakihofiwa kupoteza maisha

Zaidi, soma https://jamii.app/ZimbabweMinesFlooded
KENYA YAKANUSHA KUMUITA BALOZI WAKE WA SOMALIA NYUMBANI

- Imesema imemuita kwenda Mogadishu kwa ajili ya majadiliano na ushauri kuhusu mgogoro wa mpaka baharini

- Pia wameiomba Somalia kutuma Mwakilishi ili kupata taarifa za pande zote

Zaidi, soma https://jamii.app/Kenya-SomaliaCrisis
SAUDI ARABIA YAITETEA 'APP' YA KUWAFUATILIA WANAWAKE

- Serikali imetetea 'app' hiyo ya simu inayowezesha Wanaume kufuatilia nyendo za Wanawake wanaowahusu

- Yasema programu hiyo ya Absher inasaidia jamii pamoja na Wanawake, Wazee na Walemavu

Zaidi, soma https://jamii.app/SaudiaYateteaApp
SERIKALI YATANGAZA VITA NA WATEKAJI WA WATOTO

> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza vita na watu wanaoteka watoto na kudai fedha au kuwaua

> Amesema ujambazi Wilayani Kibondo na Kakonko kwa kiasi kikubwa unafanywa na wageni kutoka nje

Soma - https://jamii.app/SerikaliVsWatekajiWatoto