JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
'VUMBI LA KONGO' LAPIGWA MARUFUKU

Dawa hiyo imefutiwa usajili Tanzania baada ya kubainika imechanganywa na Dawa ya Nguvu za Kiume iitwayo ‘Viagra’

> Imeeleza kuwa, hiyo ni kinyume cha Sheria/Miongozo ya usajili wa Dawa za Tiba Asili na Mbadala

Soma https://jamii.app/VumbiLaKongoMarufuku

#JFAfya
👍20😁14🤔2👏1
#KEMEARUSHWA: Rushwa hukwamisha Uwajibikaji na huwaacha Watu ktk Utawala na Viongozi wasioaminika hivyo kukabiliwa na Unyonyaji na Ufisadi

> Wanaotumia Ofisi au Mamlaka fulani kwa Manufaa ya Binafsi wawajibishwe ili wawe mfano

Soma https://jamii.app/RushwaAdui

#JFUwajibikaji
🔥6👍3
Wadau ndani ya JamiiForums wametaja baadhi ikiwemo Kuongea na Simu kwa sauti kubwa ndani ya Daladala, Kupiga Mswaki hadharani na kumuonesha Mtu picha moja tu kwenye Simu yeye anaanza kuangalia na nyingine

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle
😁7👍6
MDAU: Siku hizi mtu anaona kuliko kuhoji Kiongozi asipotimiza majukumu yake na kukosa fursa kwa kuonekana mkosoaji, ni bora akubaliane na kila jambo ili apate uteuzi fulani

> Tuwajibishane na kukosoa pale panapostahili kwa manufaa ya Jamii

Soma https://jamii.app/KuhojiUwajibikaji

#JFUwajibikaji
👍22😱1
KAFULILA, HAPI WATEMWA. CHALAMILA AREJESHWA

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Chalamila amewahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Mbeya na Mwanza

Mbali na Chalamila, Wakuu wa Mikoa wapya walioteuliwa ni pamoja na Peter Serukamba (Singida), Nurdin Babu (Kilimanjaro) na Fatma Mwasa (Morogoro)

Wengine ni Halima Dengego (Iringa), Dkt. Raphael Chegeni (Mara) na Dkt Yahaya Nawanda (Simiyu), Kanali Ahmed Abbas (Mtwara) na Kanali Laban Thomas (Ruvuma)

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
👍20👎3👏21
MABADILIKO YA VITUO: Anthony Mtaka (Dodoma) amepelekwa Njombe, Queen Sendiga (Iringa) anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Waziri Kindamba anahamishiwa Songwe (alikuwa Njombe), Martin Shigella aliyekuwa Morogoro anahamishiwa Geita

Omary Mgumba amehamishiwa Tanga (alikuwa Songwe), Adam Kigoma Malima amehamishiwa Mwanza (alikuwa Tanga) na Rosemary Senyamule wa Geita anaenda Dodoma

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
👍10👏1
WAKUU WA MIKOA 10 WABAKI KWENYE NAFASI ZAO

Amos Makalla (Dar es Salaam), John Mongella (Arusha), Mwamvua Hoza Mrindoko (Katavi), Charles Makongoro Nyerere (Manyara), Zainab Rajab Telack (Lindi) na Juma Homera (Mbeya)

Wengine ni Thobias Andengenye (Kigoma), Sophia Mjema (Shinyanga), Balozi Batilda Salha Burian (Tabora) na Abubakar Kunenge (Pwani)

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
👍14
UTEUZI MAKATIBU TAWALA: Kamishna Dkt. Mussa Ali Mussa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro. Prof. Godius Kahyarara Mkoa wa Geita na Mhandisi Leonard Robert anakuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa

Wengine ni Toba Nguvila (Kagera), Elikana Mayuganya Balandya (Mwanza), Prof. Siza Donald Tumbo (Shinyanga) na Dkt. John Rogath Mboya (Tabora)

Mbali na Uteuzi, amewahamisha Vituo vya Kazi Makatibu Tawala wa Mikoa 10 na wengine 9 wamesalia kwenye Vituo vyao vya Kazi

Soma - https://jamii.app/KatibuTawala2022

#Governance
👍7
JULAI 28: SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI

Homa ya Ini (#Hepatitis) ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya aina mbalimbali

Virusi vinavyosababisha Homa ya Ini vipo katika makundi matano: A, B, C, D na E

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takriban 90% ya watu waishio na Homa ya Ini hawafahamu kuwa wanaugua Ugonjwa huo

Fahamu zaidi > https://jamii.app/HomaIni2022

#WorldHepatitisDay2022 #JFAfya
👍9
DALILI ZA HOMA YA INI

Baadhi ya dalili ni Homa, Kukosa Hamu ya Kula, Kuharisha, Kichefuchefu, Maumivu ya Tumbo, Macho kuwa ya Njano, Kutapika, Maumivu ya Misuli, Uchovu na Mwili kukosa nguvu

Soma zaidi - https://jamii.app/HomaIni2022

#WorldHepatitisDay2022 #PublicHealth #JFAfya
👍9
MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI (HEPATITIS)

Mtu anaweza kupata maambukizi ya Homa ya Ini (hutofautiana kulingana na aina ya Kirusi) kupitia Chakula/Maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye maambukizi, kujamiiana bila Kinga na mtu mwenye Ugonjwa na kuchangia matumizi ya vitu vyenye ncha kali

Pia, maambukizi yanaweza kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto wakati wa kujifungua

Zaidi, soma - https://jamii.app/HomaIni2022

#WorldHepatitisDay2022 #JFAfya
👍9
MAJERAHA KUMUWEKA POGBA NJE HADI 2023

Paul Pogba wa Juventus anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti, hivyo anaweza kukosa Michuano ya Kombe la Dunia 2022

> Aliumia goti akiwa mazoezini siku chache tangu asajiliwe akitokea Man. United

Soma https://jamii.app/PogbaAumia

#JFSports
😁5👍2🤯2😢2
#JFAFYA: Takwimu za UNAIDS zinaonesha kuongezeka kwa Maambukizi ya VVU huku ikikadiriwa kuwa kila dakika 2 kwa mwaka 2021, msichana mmoja aliambukizwa VVU

> Pia, kila dakika 1 kwa mwaka huo mtu mmoja alifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI

Soma https://jamii.app/VVUAfrika
👍9😱5😢5😁2
NIGERIA: Raia wamedai kuwa Serikali imetelekeza Vyuo Vikuu vya Umma kwa kuwa Watoto wao wanasoma Vyuo vya Nje ya Nchi hivyo itungwe Sheria itakayodhibiti Maafisa wa Serikali kusomesha Watoto wao nje ya Nchi

> Wahadhiri wa Vyuo Vikuu wapo kwenye mgomo

Soma https://jamii.app/VyuoNigeria

#Governance
👍22😁21
#TUNISIA: MABADILIKO YA KATIBA YAMUONGEZEA RAIS MAMLAKA

Tunisia imepitisha #Katiba mpya baada ya kura ya maoni ya 30% ya wapigakura

Inampa Rais udhibiti wa Serikali, Amri juu ya Jeshi na uwezo wa kuteua Serikali bila idhini ya #Bunge

Soma - https://jamii.app/KatibaMpyaTuns

#Democracy
👎16😁5
KUCHELEWESHA MALIPO HUSABABISHA MIRADI KUKAMILIKA CHINI YA KIWANGO

Kumekuwepo na ukiukwaji wa Matakwa ya Mikataba katika Miradi ya Maendeleo. Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG 2020/21 hii imesababisha hasara kubwa kwa Serikali, hali iliyopelekea kutozwa Riba ya Tsh. Bilioni 6,311.83

Kucheleweshwa kwa malipo ya Wakandarasi kuna athari mbalimbali ikiwemo Miradi kukamilika chini ya kiwango, Kukosekana thamani ya fedha na Wakandarasi kukosa Imani na Serikali kutokana na kuvunjwa kwa vipengele vya Mikataba yao

#JFUwajibikaji
👍12🤬1
UNAWEZAJE KUJIKINGA NA HOMA YA INI?

1) Usichangie matumizi ya vitu vyenye ncha kali vikiwemo viwembe

2) Kunywa Maji na kula Chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama

3) Jua Afya yako kwa kufanya vipimo vya Homa ya Ini

4) Tumia Kinga kwa usahihi wakati wa kujamiiana

Fahamu zaidi > https://jamii.app/HomaIni2022

#WorldHepatitisDay2022 #JFAfya
👍5
LOLIONDO: Washtakiwa 3 kati ya 27 waliokuwa wanakabiliwa na makosa mawili likiwamo la mauaji ya Askari katika eneo la Loliondo, wamefutiwa kesi na kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha

> Wameachiwa baada ya DPP kukosa nia ya kuwashtaki

Soma https://jamii.app/KesiLoliondo
👍12😁3🥰1
#JFSHAIRI: Ukatili ni kitendo anachofanyiwa Mtu yeyote kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza Kisaikolojia, Kimwili, Kiafya, Kingono na Kiuchumi

Jifunze kupitia Shairi hili kutoka kwa Mdau wa JamiiForums.com likizungumzia Ukatili unaofanyika kwenye Jamii

#JamiiForums #Violence #GBV
👍10