JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MYANMAR: Wanaharakati wanne wa demokrasia wamenyongwa na Jeshi wakituhumiwa kusaidia Waasi kupigana na Jeshi lililochukua Mamlaka ktk Mapinduzi 2021

> Wanaharakati hao ni Kyaw Min Yu, Phyo Zeya Thaw, Hla Myo Aung na Aung Thura Zaw

Soma https://jamii.app/WanaharakatiWanyongwa

#Democracy
👍9👎1🤯1
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameipa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa siku 67 kuibadilisha bohari hiyo kiutendaji

> Aidha, ameagiza kurudishwa kwa Mifumo ya TEHAMA iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya Taasisi hiyo

Soma https://jamii.app/MabadilikoMSD

#KemeaRushwa
👍7🤔6
MDAU: Rushwa ni mwenendo usiofaa anaoufanya mtu kwa manufaa yake binafsi. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Elimu itolewe kwa wananchi ili waweze kujua Haki zao za Msingi. Pia kuwepo na Usimamizi mzuri wa Mali/Fedha

Pia, kuwepo kwa njia wezeshi za watu kujiajiri kutafanya Rushwa ipungue na kuleta Maendeleo yenye Tija Nchini

Msome > https://jamii.app/MdauRushwa

#KemeaRushwa
👍112
#JFSPORTS: Cristiano Ronaldo amerejea Jijini Manchester na anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag kuhusu hatma yake

> Inadaiwa aliiambia klabu yake anataka kuondoka lakini hadi sasa hakuna timu iliyoonesha uhakika wa kumsajili

Soma https://jamii.app/CR7ManUtd
👍9😁3
MTWARA: Gari lenye Namba T207 CTS la Shule ya Msingi na Sekondari ya King David limepata ajali leo Julai 26, 2022 na kusababisha vifo vya Wanafunzi 8, Dereva na Msaidizi wa Wanafunzi

> Chanzo cha ajali bado hakijajulikana

Soma https://jamii.app/AjaliGariLaShule

#JFMatukio
😢29😱7👍1
#MICHEZO: Wakili wa Taasisi za Filbert Bayi, Karoli Tarimo ameiomba Mahakama iruhusu kulikamata basi la TFF ili kulipa deni la Tsh. 56,446,700

Deni hilo ni gharama ya kambi kwa Timu za Vijana wa Miaka 13, 15, 17 na ile ya Wanawake Kibaha

Soma - https://jamii.app/BasiTFF

#JFSports
😁14👍10
ZIMBABWE: Benki Kuu imezindua sarafu za dhahabu ktk juhudi za kukabiliana na ongezeko la Mfumuko wa Bei wakati sarafu ya nchi hiyo ikizidi kushuka thamani

> Kila sarafu itawekewa bei kwa kiwango cha Soko la Kimataifa kwa 'ounce' 1 ya dhahabu

Soma https://jamii.app/ZimbabweInflation

#JFUchumi
👍213
ULINZI KIDIGITALI: Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni haumaanishi kudhibiti anayoyaona tu au Watu anaoongea nao, lakini ni pamoja na kuzuia vitendo vyote vinavyofanyika Mtandaoni kuutweza utu wake

Maudhui ya Mtoto ambaye hawezi kusoma akichekwa, Mtoto akipigwa, akiongea maneno ambayo hayalingani na umri wake, Watoto wakipigana n.k ni matukio yanayoweza kurekebishwa bila kuwekwa Mtandaoni.

Soma - https://jamii.app/MtandaoWatoto

#OnlineSafety #DigitalRights
👍6
MANYARA: ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KISA TSH. ELFU 10

Petro Basco (38) Mkazi wa Gabadaw-Babati anatuhumiwa kumpiga mkewe Maria Sakware (49) kwa fimbo na kumsababisha kifo

> Inadaiwa Petro alimtuhumu Maria kuchukua pesa Tsh. 10,000

Soma https://jamii.app/MauajiManyara

#JFMatukio
🤔6👎2😢2🥰1
TETESI: JUVENTUS YAMUWINDA WERNER AU MARTIAL

Juventus inamtaka Timo Werner (Chelsea) au Anthony Martial (Man. Utd) iwapo haitampata Alvaro Morata (Atletico Madrid)

Kocha wa Juve, Max Allegri amemtaja Morata kama mchezaji aliyeweza kukamilisha safu yake ya Ushambuliaji

#JFSports
👍8👎1
UGANDA: Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Waandamanaji wanaopinga kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula

> Aidha, Rais Museveni amesema kupunguza kodi/kutoa ruzuku ili kujaribu kudhibiti Mfumuko wa Bei ni kuwapa Watu 'Faraja Bandia'

Soma https://jamii.app/UgandaProtests

#Democracy #InflationCrisis
🤔6👍4
UTEUZI: Balozi Caroline Kitana Chipeta ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, The Hague nchini Uholanzi

Kabla hajateuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Balozi Chipeta alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje

Soma - https://jamii.app/UteuziBalozi

#Governance
👍4🤯1
KENYA: Mgombea Urais (Chama cha wa Roots), Profesa George Wajackoyah amesema hatashiriki kwenye Mdahalo unaotarajiwa kufanyika Julai 26, 2022 kwa kudai kuwa matokeo ya Mdahalo huo yameshapangwa

> Anakuwa mgombea wa 2 kujitoa baada ya Raila Odinga

Soma https://jamii.app/MdahaloUrais

#Democracy
👍5
DR-CONGO: Takriban Watu watano wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa ktk Siku ya 2 ya maandamano ya kupinga uwepo wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa ktk Mji wa Goma

> Vikosi hivyo vinadaiwa kushindwa kudhibiti Waasi katika eneo hilo

Soma https://jamii.app/DRCProtests

#JFDiplomasia
👍13👏1
KENYA: Shule ya Mosoriot imefungwa baada ya Mwalimu wa Shule hiyo, Bernard Kirui kubainika aliwaingilia Watoto 3 wa kiume wenye umri wa miaka 11-13

> Inadaiwa Mwalimu alikuwa akilala ktk Bweni la Wavulana licha ya kuwa na chumba alichotengewa

Soma https://jamii.app/WatotoUnyanyasaji

#HakiMtoto
😢10🤔5👍4👎2
UCHAGUZI KENYA: William Ruto amemkosoa Mpinzani wake, Raila Odinga kwa kutoshiriki Mdahalo wa Wagombea Urais akisema kitendo hicho ni kuepuka #Uwajibikaji

Asema Raila si Mgombea halisi, anakimbia Maswali magumu, na hana la kusema kwa Wakenya

Soma - https://jamii.app/RutoDebate

#Kenya2022
😁13👍6
UPDATE: Waliofariki dunia katika maandamano ya kupinga uwepo wa Walinda Amani wa UN Nchini DR Congo wamefikia 15. Miongoni mwao ni Raia 12 na Walinda Amani 3

Waandamanaji wanadai Walinda Amani wameshindwa kudhibiti waasi hivyo uwepo wao hauna faida

Soma https://jamii.app/ChaosDRC2022

#Governance
👍15
#JFDATA: Mashirika mengi bado yanachukulia masuala ya Ulinzi wa Kidigitali kama kitu ambacho si lazima kuwa nacho

Kwa mujibu wa Ripoti ya Acronis (2022), nusu ya Mashirika Duniani hutenga chini ya 10% ya Bajeti yote ya TEHAMA kwenye Usalama wa Kidigitali

86% ya Mashirika Duniani yana wasiwasi kuhusu ongezeko la mashambulizi ya Mtandaoni

Soma zaidi - https://jamii.app/UlinziDigitali7
👍7
UMOJA WA MATAIFA (UN): Mashambulizi dhidi ya Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC yanaweza kuwa Uhalifu wa Kivita

> Hadi sasa, Wafanyakazi watatu wa Umoja wa Mataifa na Raia 12 wa DRC wameuawa katika matukio hayo

Soma https://jamii.app/GhasiaDRC

#JFDiplomasia
👍6👎2
ZAMBIA: Esther Lungu (Mke wa Rais wa zamani) amehojiwa na Wakala wa Kupambana na Utakatishaji Fedha wa Zambia kuhusu umiliki wake wa nyumba 15 zilizopo Lusaka

> Serikali ya Hichilema imekosolewa kuwa inafanya matukio hayo kwa sababu za kisiasa

Soma https://jamii.app/SiasaYaZambia

#Governance
👍10👎3👏1