JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#TUNISIA: RASIMU YA KATIBA MPYA KUPIGIWA KURA

Katiba hiyo inayolalamikiwa kumpa Madaraka makubwa Rais Kais Saied imepingwa na Vyama vya Siasa pamoja na Asasi za Kiraia. Hivi karibuni yamekuwepo Maandamano ya kutoiunga mkono

Wakosoaji wa Rais Saied wanahofia itaua Demokrasia

Soma - https://jamii.app/TunisiaVotes

#Democracy
👍11
WAKIMBIZI 17 WAFARIKI WAKIWA NJIANI KWENDA MAREKANI

Ni baada ya Mashua waliyokuwa wakitumia kuzama baharini. Mbali na vifo vya Wakimbizi hao waliotoka Haiti, watu wengine hawajulikani walipo

Mashua hiyo ilikuwa inaelekea Jijini Miami

Soma > https://jamii.app/Wakimbizi17Haiti

#DrowningPrevention
😢4👎1
Kuzama kwenye Maji kunatajwa kuwa tatizo kubwa la #Afya ya Umma duniani, na inakadiriwa Watu wapatao 236,000 huzama kila mwaka. Nchi za Uchumi wa Chini na Kati huchangia zaidi ya 90% ya vifo vya kuzama bila kukusudia

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, kuzama kwenye maji ni miongoni mwa sababu kuu za vifo kwa Watoto na Vijana wenye umri kati ya mwaka 1 - 24

Fahamu zaidi - https://jamii.app/WDPD2022

#DrowningPrevention #PublicHealth
👍11
TFF YAMSHTAKI KOCHA AZAM FC KISA VYETI VYAKE

Sekretarieti ya TFF imemshtaki Kocha wa Azam FC U-17, Mohamed Badru kwa Kamati ya Maadili kwa madai ya kuwasilisha vyeti visivyo sahihi

Shauri lake litapangiwa tarehe ya kusikilizwa

Soma > https://jamii.app/KochaAzamFC

#JFSports
👍6😁3🤩1
Ili kukabiliana na Ajali za kuzama katika Jamii, inashauriwa;

1) Kuweka vizuizi katika maeneo ya maji ili kuepusha Watoto kuyafikia pasipo uangalizi

2) Kuhimiza Mafunzo ya Kuogelea, Usalama wa Majini na Uokoaji

Zaidi, soma - https://jamii.app/WDPD2022

#DrowningPrevention
👍6👏1
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan ameshauri ujenzi wa Mnara mpya wa Mashujaa kwa kuwa uliopo umekuwa mdogo kutokana na kukua kwa Mji

> Pia, Rais ameshauri utengenezwe utaratibu wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yenye gharama nafuu

Soma https://jamii.app/MashujaaMnara

#JFUwajibikaji
👍18🥰1
KENYA: Polisi wamevamia ofisi zinazoaminika kuwa na uhusiano na Naibu Rais, William Ruto na kuchukua Kompyuta 2 na Seva (Server) 2

> Uvamizi huo unajiri huku kukiwa na mvutano kati ya Vikosi vya Usalama na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)

Soma https://jamii.app/UvamiziOfisi

#Kenya2022
👍5👎3
MISRI: Mahakama imeliandikia Bunge barua ya kutaka kufanyike marekebisho ya Sheria ili kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya kunyongwa kwa Mohammed Adel (22) kwa lengo la kuzuia Vitendo vya Ukatili kwa Wanawake

Mohammed alihukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kumchoma visu hadi kufa Nayera Ashraf akiwa maeneo ya nje ya Chuo

Soma https://jamii.app/KunyongwaMisri

#SocialJustice #GenderViolence
👏8👍4🤔2👎1🔥1
HAJI MANARA: MIMI BADO MSEMAJI WA YANGA

Amesema anaendelea kufanya shughuli za Klabu ya Yanga kwa kuwa hajapata hukumu kutoka Kamati ya Maadili ya TFF

> Pia, amewasilisha malalamiko yake BMT akidai kanuni zilizotumika hazijasajiliwa

Soma https://jamii.app/ManaraNaTFF

#JFSports
👏16💩10👍3👎3😁2🤩2🎉1
MYANMAR: Wanaharakati wanne wa demokrasia wamenyongwa na Jeshi wakituhumiwa kusaidia Waasi kupigana na Jeshi lililochukua Mamlaka ktk Mapinduzi 2021

> Wanaharakati hao ni Kyaw Min Yu, Phyo Zeya Thaw, Hla Myo Aung na Aung Thura Zaw

Soma https://jamii.app/WanaharakatiWanyongwa

#Democracy
👍9👎1🤯1
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameipa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa siku 67 kuibadilisha bohari hiyo kiutendaji

> Aidha, ameagiza kurudishwa kwa Mifumo ya TEHAMA iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya Taasisi hiyo

Soma https://jamii.app/MabadilikoMSD

#KemeaRushwa
👍7🤔6
MDAU: Rushwa ni mwenendo usiofaa anaoufanya mtu kwa manufaa yake binafsi. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Elimu itolewe kwa wananchi ili waweze kujua Haki zao za Msingi. Pia kuwepo na Usimamizi mzuri wa Mali/Fedha

Pia, kuwepo kwa njia wezeshi za watu kujiajiri kutafanya Rushwa ipungue na kuleta Maendeleo yenye Tija Nchini

Msome > https://jamii.app/MdauRushwa

#KemeaRushwa
👍112
#JFSPORTS: Cristiano Ronaldo amerejea Jijini Manchester na anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag kuhusu hatma yake

> Inadaiwa aliiambia klabu yake anataka kuondoka lakini hadi sasa hakuna timu iliyoonesha uhakika wa kumsajili

Soma https://jamii.app/CR7ManUtd
👍9😁3
MTWARA: Gari lenye Namba T207 CTS la Shule ya Msingi na Sekondari ya King David limepata ajali leo Julai 26, 2022 na kusababisha vifo vya Wanafunzi 8, Dereva na Msaidizi wa Wanafunzi

> Chanzo cha ajali bado hakijajulikana

Soma https://jamii.app/AjaliGariLaShule

#JFMatukio
😢29😱7👍1
#MICHEZO: Wakili wa Taasisi za Filbert Bayi, Karoli Tarimo ameiomba Mahakama iruhusu kulikamata basi la TFF ili kulipa deni la Tsh. 56,446,700

Deni hilo ni gharama ya kambi kwa Timu za Vijana wa Miaka 13, 15, 17 na ile ya Wanawake Kibaha

Soma - https://jamii.app/BasiTFF

#JFSports
😁14👍10
ZIMBABWE: Benki Kuu imezindua sarafu za dhahabu ktk juhudi za kukabiliana na ongezeko la Mfumuko wa Bei wakati sarafu ya nchi hiyo ikizidi kushuka thamani

> Kila sarafu itawekewa bei kwa kiwango cha Soko la Kimataifa kwa 'ounce' 1 ya dhahabu

Soma https://jamii.app/ZimbabweInflation

#JFUchumi
👍213
ULINZI KIDIGITALI: Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni haumaanishi kudhibiti anayoyaona tu au Watu anaoongea nao, lakini ni pamoja na kuzuia vitendo vyote vinavyofanyika Mtandaoni kuutweza utu wake

Maudhui ya Mtoto ambaye hawezi kusoma akichekwa, Mtoto akipigwa, akiongea maneno ambayo hayalingani na umri wake, Watoto wakipigana n.k ni matukio yanayoweza kurekebishwa bila kuwekwa Mtandaoni.

Soma - https://jamii.app/MtandaoWatoto

#OnlineSafety #DigitalRights
👍6
MANYARA: ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KISA TSH. ELFU 10

Petro Basco (38) Mkazi wa Gabadaw-Babati anatuhumiwa kumpiga mkewe Maria Sakware (49) kwa fimbo na kumsababisha kifo

> Inadaiwa Petro alimtuhumu Maria kuchukua pesa Tsh. 10,000

Soma https://jamii.app/MauajiManyara

#JFMatukio
🤔6👎2😢2🥰1
TETESI: JUVENTUS YAMUWINDA WERNER AU MARTIAL

Juventus inamtaka Timo Werner (Chelsea) au Anthony Martial (Man. Utd) iwapo haitampata Alvaro Morata (Atletico Madrid)

Kocha wa Juve, Max Allegri amemtaja Morata kama mchezaji aliyeweza kukamilisha safu yake ya Ushambuliaji

#JFSports
👍8👎1
UGANDA: Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Waandamanaji wanaopinga kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula

> Aidha, Rais Museveni amesema kupunguza kodi/kutoa ruzuku ili kujaribu kudhibiti Mfumuko wa Bei ni kuwapa Watu 'Faraja Bandia'

Soma https://jamii.app/UgandaProtests

#Democracy #InflationCrisis
🤔6👍4