JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: Serikali imewapa siku 7 Wakazi wa Msalato waliojiorodhesha kudai fidia katika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato wakitambua wao si wamiliki halali wa viwanja, kufuta majina yao Ofisi za Serikali ya Mtaa

> Watakaokaidi watachukuliwa hatua

Soma https://jamii.app/ArdhiDodoma

#JFUwajibikaji
πŸ‘5
UBAKAJI NA ULAWITI MBIONI KUKOSA DHAMANA

Serikali inakusudia kurekebisha Sheria ili kuwezesha kuwajibishwa kwa Watuhumiwa wa makosa hayo kikamilifu

> Ni baada ya utafiti kuonesha Watuhumiwa hutoroka au kumalizana na Waathirika kinyume cha Sheria

Soma https://jamii.app/UbakajiDhamana

#JFUwajibikaji
πŸ‘7
KENYA: Jacob Ochola, (62) anayedai kuwa Mtoto wa kwanza wa Rais Mwai Kibaki, amefungua shauri la kutaka kutambuliwa na familia ya Hayati huyo kama Mwanafamilia na sehemu ya Warithi

> Pia, ametaka familia kuweka wazi iwapo ametajwa kwenye wosia

Soma https://jamii.app/KibakisAllegedSon

#JamiiForums
πŸ‘18πŸ€”3πŸ‘Ž1🀯1
RUSHWA YA NGONO VYUONI: UNESCO imezindua Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma kushughulikia ukatili wa aina hiyo

> Unadhani nini kifanyike kuondoa ukatili wa kijinsia Vyuoni Nchini?

Soma https://jamii.app/UkatiliVyuoni

#GenderViolence #KemeaRushwa #HumanRights
πŸ‘16🀩1
MALEZI: Tabia ya Watoto kupelekwa kwa Babu na Bibi kisha kutojaliwa katika matunzo imetajwa kuongezeka Mkoani Njombe

Inaelezwa, wanaathirika wengi wa ukatili ni wale wanaolelewa na Babu na Bibi zao huku Wazazi wakiwa na migogoro au majukumu mengine

Soma https://jamii.app/HakiZaMtotoNjombe

#HakiMtoto
πŸ‘5😒1
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Rais Kenyatta anamalizia Muhula wake kama Kiongozi wa Kenya, pia ameshakabidhi Uenyekiti wa EAC kwa Rais wa Burundi, Γ‰variste Ndayishimiye

#Governance
πŸ‘11❀1
MAUZO YA NAFAKA: UKRAINE NA URUSI ZASAINI MAKUBALIANO

Ni makubaliano ya kuruhusu mauzo ya nafaka kutoka Bandari ya Bahari Nyeusi ya Ukraine yanayolenga kupunguza uhaba wa Chakula duniani

Vita ilisababisha Bandari kufungwa na kukwamisha usafirishaji

Soma https://jamii.app/RussiaUkraineWar

#FoodSecurity
😁11πŸ‘5
MAREKANI YATOA SILAHA ZA TSH. BILIONI 627 KWA UKRAINE

Msaada unahusisha roketi 4 za HIMARS, ndege 580 ndogo zisizo na rubani, risasi 36,000 za bunduki za M777

> Marekani imetumia jumla ya Tsh. Trilioni 19 kuisaidia Ukraine tangu kuanza kwa vita

Soma https://jamii.app/MsaadKwaUkraine

#Transparency
πŸ€”12πŸ‘Ž8πŸ‘7πŸ‘3πŸ”₯2
CHUNYA-MBEYA: Change Mawanga (32) amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka na kumlawiti Mtoto (4) wa dada yake

Ukatili huo unashamiri Wilayani Chunya kutokana na imani kuwa mtu akibaka au kulawiti mtoto hupata dhahabu

> Nini kifanyike kukomesha ukatili huu kwa Watoto?

Soma https://jamii.app/JelaUbakaji

#HakiMtoto
πŸ‘12
KUFUZU CHAN 2023: SOMALIA 0-1 TANZANIA

#TaifaStars imeshinda 1-0 dhidi ya Somalia, goli likifungwa na Abdul Hamis Sopu

Mchezo huo wa Kufuzu CHAN 2023 umefanyika katika Uwanja wa Mkapa, na timu hizo zitarudiana wikiendi ijayo katika uwanja huo huo

Soma > https://jamii.app/KufuzuCHAN2023

#JFSports #CHAN2023
πŸ‘24😁7πŸ‘4
HUDUMA YA INTANETI: NINI MAONI YAKO KUHUSU MABADILIKO YA VIFURUSHI?

Wadau ndani ya JamiiForums.com wamelalamikia kitendo cha baadhi ya Kampuni za Simu kupunguza ukubwa wa Vifurushi vya Intaneti ghafla, na pasipo taarifa rasmi

Wanahoji: Je, Kampuni za Simu zinafanya zitakavyo? Zitaendelea kubadilisha Vifurushi vya Intaneti bila kutoa taarifa mpaka lini?

Mjadala > https://jamii.app/HudumaIntanetiTZ

#DigitalRights
😱12πŸ‘10😒2😁1
MDAU: KUFANYA MAZOEZI KANDO YA BARABARA SI SALAMA

Anasema wengi wa wanaokimbia kando ya barabara hugongwa na Vyombo vya Usafiri kwani wanakimbia bila tahadhari

Pia, moshi wa Vyombo vya Usafiri si salama kwa anayekimbia

Soma zaidi - https://jamii.app/JoggingBarabarani

#JFAfya
πŸ‘22
CHANJO YA COVID-19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linakuja na mpango mbadala wa kutoa chanjo ya kujikinga na Corona kwa kuamua kuweka kipaumbele katika Nchi au maeneo hatarishi ya Watu kuambukizwa Ugonjwa huo

Soma https://jamii.app/ChanjoMabadiliko

#COVID19 #JFAfya
πŸ‘6πŸ‘Ž2πŸŽ‰1
RAILA ODINGA: SIPO TAYARI KUSHIRIKI MDAHALO NA RUTO

Amesema hayupo tayari kushirikiana na Mpinzani wake mkuu kwa madai
ni wazo baya kuungana na William Ruto jukwaani, kwani Kiongozi huyo atafanya na kusema lolote ili kupata Madaraka

Soma - https://jamii.app/RailaRutoDebate

#Kenya2022
πŸ‘11😁5
Mdau wa JamiiForums.com anasema
Muonekano, mali, kazi na elimu visiwe vigezo vya kuchagua mwenza wa maisha

Ameshauri kuzingatia mwenye hofu ya Mungu na kujali, kukuheshimu, na mshauri wa mambo ya kimaendeleo

> Je, una maoni gani kwenye hoja ya Mdau?

Soma https://jamii.app/MwenzaWaMaisha

#JFMahusiano
πŸ‘18
MALAYSIA: Zaidi ya Watu 500 wamekusanyika na kuandamana wakilalamikia gharama za maisha kuwa kubwa Jijini Kuala Lumpur

> Wanalalamikia ongezeko la bei za bidhaa, usalama wa chakula na misaada kwa Wananchi

Soma https://jamii.app/ProtestInMalaysia

#Governance
πŸ‘13πŸ”₯2😁1
#TUNISIA: RASIMU YA KATIBA MPYA KUPIGIWA KURA

Katiba hiyo inayolalamikiwa kumpa Madaraka makubwa Rais Kais Saied imepingwa na Vyama vya Siasa pamoja na Asasi za Kiraia. Hivi karibuni yamekuwepo Maandamano ya kutoiunga mkono

Wakosoaji wa Rais Saied wanahofia itaua Demokrasia

Soma - https://jamii.app/TunisiaVotes

#Democracy
πŸ‘11
WAKIMBIZI 17 WAFARIKI WAKIWA NJIANI KWENDA MAREKANI

Ni baada ya Mashua waliyokuwa wakitumia kuzama baharini. Mbali na vifo vya Wakimbizi hao waliotoka Haiti, watu wengine hawajulikani walipo

Mashua hiyo ilikuwa inaelekea Jijini Miami

Soma > https://jamii.app/Wakimbizi17Haiti

#DrowningPrevention
😒4πŸ‘Ž1
Kuzama kwenye Maji kunatajwa kuwa tatizo kubwa la #Afya ya Umma duniani, na inakadiriwa Watu wapatao 236,000 huzama kila mwaka. Nchi za Uchumi wa Chini na Kati huchangia zaidi ya 90% ya vifo vya kuzama bila kukusudia

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, kuzama kwenye maji ni miongoni mwa sababu kuu za vifo kwa Watoto na Vijana wenye umri kati ya mwaka 1 - 24

Fahamu zaidi - https://jamii.app/WDPD2022

#DrowningPrevention #PublicHealth
πŸ‘11
TFF YAMSHTAKI KOCHA AZAM FC KISA VYETI VYAKE

Sekretarieti ya TFF imemshtaki Kocha wa Azam FC U-17, Mohamed Badru kwa Kamati ya Maadili kwa madai ya kuwasilisha vyeti visivyo sahihi

Shauri lake litapangiwa tarehe ya kusikilizwa

Soma > https://jamii.app/KochaAzamFC

#JFSports
πŸ‘6😁3🀩1