JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SUDAN YAFUNGUA MPAKA WAKE NA ETHIOPIA

Mpaka wa Gallabat ulifungwa Juni 27, 2022 baada ya Sudan kuishutumu Ethiopia kwa kuwanyonga Wanajeshi wake 7

> Hatua hiyo ni baada ya Viongozi wa nchi hizo kukubaliana kutatua mzozo maeneo ya mpakani

Soma https://jamii.app/MpakaSudanEthiopia

#JFDiplomasia
👍6
DAR: Serikali imekata rufaa kupinga Mahakama ya Kisutu kumfutia Kesi ya Uhujumu Uchumi Jitesh Jayantilal Ladwa (wa Hoteli za Golden Tulip) ikidai Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kutoa uamuzi huo

> Alikuwa anakabiliwa mashtaka 24 yakiwemo ya kujihamishia Hisa za Wanahisa wenzake

Soma https://jamii.app/SerikaliRufaa
👍3
Siku ya Mandela inalenga kuhamasisha watu wote kuchukua hatua na kuleta mabadiliko katika Jamii kwani kila mmoja ana uwezo kufanya hivyo

#MandelaDay
👍10🎉2😁1
TETESI: RONALDO ANATAKA KUICHEZEA ATLETICO

Inadaiwa Cristiano Ronaldo anamshawishi Kocha Diego Simeone ili amsajili kwa ajili ya kuichezea Atletico Madrid msimu ujao

> Anataka kuondoka Man. United ili apate nafasi ya kucheza UEFA Champions League

Soma https://jamii.app/UsajiliWaCR7

#JFSports
👍8
Idara ya Ujasusi ya DR-Congo inamshikilia Mwanahabari wa Marekani, Stavros Nicolas Niarchos (33) kwa kudaiwa kukaribia makundi yenye silaha Kusini Mashariki mwa nchi hiyo

> Anadaiwa kuwasiliana na Wanamgambo wa Bakata Katanga

Soma - https://jamii.app/USJournalistDetained

#PressFreedom
👍5
MWANZA: Maombi ya Diana Bundala 'Mfalme Zumaridi' ya kutokuwa na imani na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Monica Ndyekobora yameshindwa kupata majibu baada ya Hakimu huyo kusema alipata changamoto ya kiafya

> Maamuzi yatatolewa Julai 27, 2022

Soma https://jamii.app/KesiYaZumaridi
👍6
UINGEREZA: Hali ya Joto inatarajiwa kuwa Nyuzi Joto 43 kwa siku ya Jumanne Julai 19, 2022 ikiwa ni hali ya joto kali kuwahi kutokea katika historia ya Nchi hiyo

> Mamlaka ya Hali ya Hewa Uingereza imesema leo Julai 18, 2022 hali ya joto ni Nyuzi Joto 40

Soma https://jamii.app/JotoUK

#ClimateChange
👍4🔥3👎2
TARIME: Watu 6 waliodaiwa kuwa Majambazi Sugu wa Mifugo wamehukumiwa kwenda jela miaka 70 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha aina ya bunduki na mapanga

> Washtakiwa hao walifanya fujo Mahakamani hapo kupinga hukumu kabla ya kudhibitiwa

Soma - https://jamii.app/MaraMahakamani

#JFMatukio
👍15🥰2😁1
SOMALIA: Ndege ya Shirika la Ndege la Jubba imeanguka wakati ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden Adde Jijini Mogadishu ilipokuwa ikitokea Baidoa

> Watu 36 katika ndege hiyo wameokolewa

Soma https://jamii.app/NdegeYaanguka
👍6👎2😢2
KENYA: Serikali imepunguza bei ya Unga wa Mahindi kuwa Ksh. 100 (Tsh. 1,944) kwa Kilogram Mbili kutoka Ksh. 210 (Tsh. 4,084) iliyokuwa awali

> Hatua hii ni ili kukabiliana na mfumuko wa bei uliotokea hivi karibuni

Soma https://jamii.app/BeiYaUngaKE

#Governance
👍13😁9🔥1
HOMA YA MGUNDA NI NINI?

Ni Ugonjwa unaoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu

Homa ya Mgunda 'Leptospirosis' husababishwa na Bakteria aina ya 'Leptospira interrogans'

Baadhi ya dalili zake ni Homa, Maumivu ya Kichwa na Misuli, Uchovu na kutokwa damu puani

Fahamu zaidi - https://jamii.app/UgonjwaHomaMgunda

#JFAfya #PublicHealth
👍4
IMF YAIDHINISHIA TANZANIA MKOPO WA TSH. TRILIONI 2.4

Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 1.046 (Takriban Tsh. 2,422,536,000,000) kwa #Tanzania katika kipindi cha miezi 40 kusaidia kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine

Vita hiyo imetajwa kukwamisha Uchumi wa Tanzania kuimarika kufuatia mlipuko wa #COVID19

Soma - https://jamii.app/IMF-TZMkopo
😁21👍7👏1
HOMA YA MGUNDA: BINADAMU ANAPATAJE MAAMBUKIZI?

1) Kugusa mkojo/maji maji mengine ya mwili kutoka kwa wanyama walioambukizwa

2) Kugusa Maji, Udongo au Chakula kilichochafuliwa na mkojo wa Wanyama

3) Kunywa Maji yaliyochafuliwa na Bakteria wa Homa Ya Mgunda

Fahamu zaidi - https://jamii.app/UgonjwaHomaMgunda

#JFAfya #PublicHealth
👍3
Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuipa Ukraine msaada zaidi wa Kijeshi wa Dola Milioni 508 (Tsh. Trilioni 1.17)

> Pia, Nchi Wanachama zimekubalina kuongeza vikwazo ikiwemo kuzuia dhahabu ya Urusi kuzuiwa kuuzwa Ulaya

Soma https://jamii.app/EUUkraine2022

#RussiaUkraineWar
👎4👍3
SPURS YAENDELEA KUJIIMARISHA, YAMSAJILI SPENCE

Tottenham imemsajili Beki, Djed Spence (21) kutoka Middlesbrough kwa Paundi Milioni 20 (Tsh. 55,400,000,000)

Spurs tayari imewasajili Ivan Perisic, Fraser Forster, Yves Bissouma, Richarlison na Clement Lenglet (Mkopo)

#JFSports
👍5
PAKISTAN: Miili 20 imeopolewa na takriban Watu 30 hawajulikani walipo baada ya mashua iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu 100 wa ukoo mmoja kupinduka kwenye Mto Indus

> Boti hiyo iliyojaa mizigo ilikuwa ikielekea katika harusi ya kifamilia

Soma https://jamii.app/VifoPakistan
😢9🤯4👍2👎1
IVORY COAST: Wanaharakati wa Haki za Wanawake wamesema Muswada unaopendekezwa wa kuhalalisha na kurejesha tena ndoa za wake wengi kwa Wanaume ni kurudisha nyuma jitihada za Vita ya Usawa wa Kijinsia

> Ndoa hizo zilipigwa marufuku nchini humo 1964

Soma https://jamii.app/MswadaIvoryCoast

#GenderEquality
😁9
Mtazamo hasi kuhusu Wosia unatajwa kusababisha migogoro mingi katika jamii, huku Watoto na Watoto wakiathiriwa zaidi

> Nini Mtazamo wako kuhusu kuandika Wosia? Unafikiri sababu nyingine zinazopelekea watu wachache kuwa na Wosia ni zipi?

> Je, wewe upo tayari kuandika Wosia?

Soma https://jamii.app/ElimuYaWosia

#JFSheria
👍8
ARUSHA: Diwani wa Kata ya Mswakini, Nanga Mollel amethibitisha vifo vya Watoto watano wa Familia moja Wilayani Monduli, ikidaiwa walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya tumbo

Inadaiwa vifo hivyo vimetokea kwa siku tofauti (Julai 5, 16, 17 na 19, 2022)

Soma https://jamii.app/VifoWatotoArusha
😢8👎7👍1
BARIDI KUONGEZEKA IRINGA, NJOMBE NA MBEYA

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema hali ya hewa inatarajiwa kufikia viwango vya 4°C katika Mikoa hiyo

Kwa sasa viwango ni Njombe 15°C, Iringa 20°C na Mbeya 21°C

Soma https://jamii.app/BaridiKuongezeka
😁20👍16🤔10😢2🔥1