JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#COVID19: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema waliopata chanjo ya #Corona hadi sasa ni asilimia 9.81 kati ya wote wanaostahili kupata

> Waziri amesema hayo wakati akipokea chanjo aina ya #Sinovac dozi milioni 1 kutoka Serikali ya Uturuki

Soma - https://jamii.app/Uviko19
#JamiiForums
IRINGA: Mahakama ya Rufani Tanzania imeiondoa Mahakamani kesi iliyomkabili Abdul Nondo baada ya DPP kukosa nia ya kuendelea nayo

> Alishtakiwa kwa makosa ya kuchapisha taarifa za uongo Mtandaoni na kutoa taarifa za uongo kwa Mtumishi wa Umma Mafinga

Soma https://jamii.app/NondoKesi
KUELEKEA NDOA YA MREMA: Mwenyekiti wa TLP, Augustino Lyatonga #Mrema anatarajia kufunga ndoa Machi 24, 2022

> Mrema amesema ikitokea ameshindwa kufika Kanisani kutokana na hali yake ya kiafya, ndoa hiyo itafungiwa hata chumbani kwake

Soma > https://jamii.app/MremaNdoa
#JamiiForums
MATUMIZI YAKO YA SIMU YANAJENGA AU KUDHOOFISHA FAMILIA YAKO?

Mdau anasema kwa Dunia ya leo imekuwa ni changamoto kuweza kuhusiana vema Majumbani, Simu ikiwa moja ya sababu ya upungufu huo

Anasema baadhi ya Makosa ambayo Wazazi/Walezi huyafanya na Simu ni kuona Teknolojia ya Kidigitali haifai kwa Mtoto. Wengine hukosea kwa kummilikisha Mtoto kifaa cha Kidigitali bila misingi ya matumizi

Zaidi, soma - https://jamii.app/SimuFamilia
#DigitalSafety #Familia
MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI KUPELEKWA MAHAKAMANI

Kamanda wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa akiwa Kituo cha Mabasi cha Magufuli amesema β€œDereva atakayekutwa anaendesha Gari bila kufuata #Sheria atapelekwa Mahakamani na sio kulipa faini kama awali”

Soma - https://jamii.app/DerevaAjaliJela
MGOGORO WA #UKRAINE NA #URUSI: Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin amesema hakuna nchi kati ya zilizopo ktk G20 inayoweza kumfukuza Uanachama Nchi nyingine

> Hii ni baada ya Marekani kuomba Urusi iondolewe G20

Soma https://jamii.app/G20
#RussiaUkraineConflict
MGOGORO WA #URUSI NA #UKRAINE: Serikali ya Tanzania imefafanua sababu ya kupiga Kura ya Kutofungamana ktk Baraza la Usalama la UN

> Imesema, kutafuta suluhu ktk meza ya mazungumzo ndilo tulilotaka lakini halikutokea

Soma > https://jamii.app/UkraineTZ
#RussiaUkraineCrisis
BASATA: STEVEN NYERERE ALITEULIWA KIHALALI ILA ASIANZE KAZI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo lina majukumu kisheria ya kusuluhisha migogoro ya Vyama vya Wasanii vilivyosajiliwa limesema Msemaji aliteuliwa kwa vikao vya Bodi ya Shirikisho

Soma https://jamii.app/SteveBASATA
BALOZI WA DENMARK AITEMBELEA JAMIIFORUMS

Balozi wa #Denmark Nchini Tanzania, Mette Norgaard Spandet jana Machi 23, 2022 ametembelea Ofisi za #JamiiForums na kukutana na Watendaji na Mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi

Balozi Mette na timu yake wamepata kuelezwa namna JF inavyoendesha shughuli zake za uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora Nchini #Tanzania
#AFGHANISTAN: TALIBAN YAZUIA UFUNGUZI WA SHULE ZA WASICHANA

Wameamua kutozifungua tena Shule za Wasichana kinyume na ahadi walioitoa ya kuruhusu Wasichana kusoma

Uamuzi huo unarudisha nyuma juhudi za kutambuliwa Kimataifa na kupokea ufadhili

Soma https://jamii.app/GirlsTaliban
#JFLeo
#Marekani: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Madeleine Albright, Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo amefariki kwa #Saratani akiwa na miaka 84

Alikuwa Mtu muhimu ktk Utawala wa Bill Clinton ambapo alifanikisha NATO kujitanua ktk Mataifa mengi

Soma - https://jamii.app/StateSecretary
#URUSI: Anatoly Chubais ambaye ni mmoja wa Washauri wa Rais Vladimir Putin, amejiuzulu nafasi yake kama Mjumbe wa Kimataifa anayeratibu Maendeleo Endelevu ya Urusi Kimatafa

> Inadaiwa kuwa kwa sasa Chubais na Mkewe wapo Nchini #Uturuki

Soma https://jamii.app/UrusiChubais
RAIS SAMIA: DARAJA LA TANZANITE LIWEKWE ALAMA YA TANZANITE

Rais Samia Suluhu amesema alama ya Mwenge ktk Daraja la Tanzanite iondolewe na iwekwe alama ya Tanzanite ili watu waone inafananaje

> Amesema alama ya Tanzanite itakamilisha jina la Daraja

Soma https://jamii.app/Tanzanite
#UGANDA: Mahakama imetoa hati ya kumkamata Mwandishi wa Vitabu, Kakwenza Rukirabashaija kwa kutofika Mahakamani

Alitoroka Nchi baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kumtusi Rais Yoweri Museveni na mwanaye, Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Soma - https://jamii.app/KakwenzaLawsuit
#FreeSpeech
#UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameomba watu Duniani kuandamana kupinga Operasheni ya #Urusi Nchini Ukraine iliyoanza Februari 24, 2022

> Zelensky amesema kuunga mkono Ukraine ni kuunga mkono Uhuru na Maisha

Soma https://jamii.app/WorldProtest
#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
MODERNA KUOMBA KUTUMIKA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 6

Itawaomba wadhibiti wa Marekani na Ulaya, kuidhinisha dozi 2 ndogo kwa Watoto chini ya Miaka 6

Watoto milioni 18 Nchini Marekani walio chini ya Miaka 5, ndio kundi la umri ambalo halijapata Chanjo

Soma https://jamii.app/ModernaBabies
BOTSWANA YAKATAA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA TANZANIA

Chama cha Soka cha Botswana (BFA) kimesema Tanzania iliomba kucheza Michezo 3 huku viwango vya FIFA vikiwa ni michezo 2

> BFA imesema mchezo huo wa 3 usingekuwa na umuhimu kwao

Soma > https://jamii.app/TFFFIFA
#Sports
πŸ‘1
BELEDWEYNE, SOMALIA: Shambulio la Bomu la kujitoa mhanga la Wanamgambo wa Al-Shabaab limesababisha vifo vya watu 15 akiwemo Mbunge, Amina Mohamed Abdi

> Baadhi ya ripoti zinaonesha idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa kuliko inayotajwa sasa

Soma https://jamii.app/BomuMhanga
#JamiiForums