JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: RAIS BIDEN ATEUA MWANAMKE MWEUSI KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA JUU

Ketanji Jackson anakuwa Mwanamke wa kwanza Mweusi kwenye Mahakama ya juu kabisa ambayo awali ilitangaza hastahili kupata Uraia wa Marekani kutokana na rangi ya Ngozi yake

Soma https://jamii.app/KentanjiSupreme
#JFLeo
RELI, DARAJA VYASOMBWA NA MAJI. ABIRIA WAKWAMA MOROGORO

Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Morogoro zimesababisha uharibifu wa Miundombinu ya Reli ya kati na Barabara ambapo Daraja la Kidete limekatika na kupelekea Treni kusimamisha safari zake

Soma - https://jamii.app/AbiriaKilosa
URUSI: Mtandao wa #Facebook unaomilikiwa na Kampuni ya Meta umezuiwa Nchini Urusi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupishana ktk Masharti ya vitu vya kuweka Mitandaoni wakati huu wa vita na #Ukraine

Soma - https://jamii.app/FBBanRussia

#DigitalRights #RussiaUkraineConflict #PressFreedom
RAIS SAMIA AKUTANA NA MTAWALA WA DUBAI

Rais Samia amezungumza na Makamu wa Rais ambaye ni Waziri Mkuu wa UAE na Mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum

> Ni baada ya kuhutubia katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 Mjini Dubai

Soma https://jamii.app/RaisSamiaDubai

#JFLeo
POLAND KUKATAA KUCHEZA NA URUSI MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

- Poland imesema itakataa kucheza mchezo huo wa Machi 25, 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine

- Pia itakuwa mwenyeji wa michezo yote ambayo Ukraine ilitakiwa kuwa mwenyeji ila itashindwa kutokana na vita

#JFSports
SERIKALI YATOA TAHADHARI YA MLIPUKO WA POLIO

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesisitiza Wazazi kuhakikisha Watoto wanapatiwa dozi kamili ya chanjo #Polio

> Hatua hii imekuja baada ya Malawi kuripoti kisa cha kwanza baada ya muda mrefu

Soma https://jamii.app/MlipukoPolio
#JFAfya
PWANI: MELI YA MAFUTA YAUNGUA

Meli ndogo iliyokuwa na Mafuta imeungua ikiwa kwenye maegesho ya Bandari ya Nyamisati. Meli hiyo ilikuwa na safari ya kuelekea Kisiwa cha Mafia kupeleka mafuta hayo

Soma - https://jamii.app/MeliNdogo

#JamiiForums #JFLeo
UKRAINE: MASHAMBULIZI YAPELEKEA MAELFU KUKIMBILIA NCHI JIRANI

Zaidi ya Raia 150,000 wa #Ukraine wamevuka Mipaka kuingia Mataifa jirani katika upande wa Magharibi kutafuta usalama, wakati Urusi ikishambulia Mji Mkuu wa Nchi hiyo pamoja na Miji mingine kwa mashambulizi ya angani

Soma - https://jamii.app/UkraineUsalama

#RussiaUkraineConflict
SWEDEN YAUNGANA NA POLAND KUKATAA KUCHEZA NA URUSI

- Sweden imeungana na Poland kukataa kucheza na Urusi katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar

- Mshindi wa mchezo kati ya Poland na Urusi angekutana na Mshindi kati ya Sweden na Jamhuri ya Czech

#JFSports
BILIONEA ABRAMOVICH AJIWEKA KANDO CHELSEA LAKINI BADO NI MMILIKI

Mmiliki wa Chelsea FC ametangaza kujiweka kando na majukumu ya Uongozi ndani ya Klabu hiyo na kukabidhi kwa Bodi ya Wadhamini ambapo yeye ataendelea kubaki katika nafasi ya umiliki

Soma - https://jamii.app/ChelseaUnrest
SERIKALI KUSAIDIA WATANZANIA WALIO UKRAINE KURUDI NCHINI

Serikali inawasaidia Watanzania takriban 300 waliopo #Ukraine kuingia Poland na Romania ambapo kuna utulivu ili waweze kurejea Nchini

Hadi sasa, hakuna madhara yaliyoripotiwa kwa Watanzania

Soma - https://jamii.app/WatanzaniaUkraine
UKRAINE: WAFUNGWA WENYE UZOEFU WA KIJESHI KUACHWA HURU

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali asema wataachwa huru ili wasaidie kuipigania Nchi yao

Aidha, Wanawake wamesema watapambana kwa kuchangia damu ili kunusuru majeruhi

Soma - https://jamii.app/MilitaryExperience

#RussiaUkraineConflict
MWANZA: 'MFALME ZUMARIDI' AKAMATWA NA POLISI

Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi anakabiliwa na tuhuma za usafirishaji haramu wa binadamu na unyonyaji. Amesafirisha watu 149 wakiwemo Watoto 24

Amekuwa akiwaaminisha watu kuwa yeye ni Mungu

Soma - https://jamii.app/MfalmeZumaridi
MPANGO WA VIBERENGE MLIMA KILIMANJARO WAINGIA DOA, WAZIRI MKUU AUKOSOA

Ametaka tathmini ya kina kufanyika akisema, "Nasikia mnataka kuweka kiberenge cha kupanda Mlima Kilimanjaro, mnataka kuua Mlima? Mkiweka machuma ya kupanda Mlima mtaharibu"

Soma - https://jamii.app/PMKili
#Ukraine imeonesha utayari wa kufanya mazungumzo na #Urusi mpakani mwa nchi hizo mbili ili kupunguza athari kwa raia wasio na hatia

Hatua imekuja baada ya Urusi kuonesha kuwa ingeweza kutumia Bomu la Nyuklia kuipiga Ukraine

Soma https://jamii.app/MazungumzoVita
#RussiaUkraineConflict
UMOJA WA ULAYA (EU) WAPIGA MARUFUKU NDEGE ZA URUSI

Hii inamaanisha Ndege za Urusi hazitoweza kutua, kuruka au kupita juu ya anga la Nchi yoyote ya Umoja huo

Pia, umepiga marufuku Vyombo vya Habari vya Sputnik na Russia Today

Soma https://jamii.app/EURussiaBan

#RussiaUkraineCrisis
#UPDATES - UKRAINE: Shirika la UNHCR limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini #Ukraine imefikia Watu 368,000

Makadirio ya Jumamosi tu zaidi ya Watu 150,000 wamekimbilia #Poland, na Mataifa mengine ikiwemo #Hungary na #Romania

Soma https://jamii.app/RefugeesUkraine

#RussiaUkraineConflict
DR CONGO: Boti ya mizigo imewaka moto Bandarini na kuua watu 20, huku wengine 11 wakiungua vibaya

Serikali imepiga marufuku abiria kupanda boti za mizigo lakini wengi hutumia usafiri huo kutokana na Miundombinu duni ya Barabara

Soma - https://jamii.app/20DeadDRC

#JamiiForums
MICHEZO: Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa katika viwanja visivyoegemea upande wowote, ikionya huenda Nchi hiyo ikaondolewa kwenye mashindano ikiwa hali ya #Ukraine haitaimarika

Soma https://jamii.app/FIFARussia

#JFSports
MICHEZO: Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Chelsea hawajakubali maombi ya Roman Abramovich kukabidhi majukumu ya kuiongoza timu kwa bodi hiyo huku yeye akibaki kuwa Mmiliki

> Inaelezwa, hofu ya Wajumbe hao ni kuonekana wanatumia klabu kwa malengo binafsi

Soma - https://jamii.app/31/Chelsea