JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BURKINA FASO: Wanajeshi wakisaidiana na Vikosi vya #Ufaransa wamewaua takriban Magaidi 60 kati ya Januari 16, 2022 hadi Januari 23, 2022

Burkina Faso inakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye uhusiano na Al-Qaida na Islamic State tangu 2015

Soma https://jamii.app/Magaidi60
YEMEN: Ripoti ya UN inasema Watoto 2,000 waliosajiliwa na Waasi wa Kihouthi kuwa wapiganaji walifariki vitani, kati ya Januari 2020 - Mei 2021

Wahouthi hutumia Misikiti na Shule kueneza nadharia zao. Vita vya #Yemen vimedumu kwa miaka 7

Soma https://jamii.app/ChildDeathYemen
#ChildSafety
MISS USA 2019 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJIRUSHA GHOROFANI

Kwa mujibu wa Polisi, Cheslie Kryst (30) amefariki baada ya kujirusha ghorofani Manhattan, New York

Kabla ya kifo chake aliweka picha yenye ujumbe "Siku hii ikuletee Pumziko la Amani" Instagram

Soma - https://jamii.app/MissUSA

#JFMatukio
Waziri wa Habari, Nape Nnauye ametangaza kufanyika kwa mabadiliko kwenye Kanuni, ikiwemo namba 18 ya mwaka 2018 inayohusiana na miundombinu ya utangazaji wa kidigitali

Marekebisho hayo yamepelekea Chaneli za bure zionekane tena kwenye DStv

Soma - https://jamii.app/LocalChannelsLaw

#JFSheria
VIASHIRIA/TABIA HATARISHI KWA MTU ANAYETAKA KUJARIBU KUJIUA

1. Miongoni mwa dalili za Watu wanaotaka kujiua ni upweke au kujitenga. Mara nyingi Watu wanaofikiria kujiua huwa wanakwepa mwingiliano na wengine, hupenda kuwa wenyewe

2. Kufanya Mazungumzo ya kujiua: Kuna baadhi ya Watu ambao hupenda kuzungumzia kuhusu kujiua au kuua wengine. Wanasaikolojia wanaonya Watu hawa wasichukuliwe kimasihara

Soma - https://jamii.app/SuicideWarningSigns
#SuicideAttempts
KENYA: TAKRIBAN WATU 13 WAHOFIWA KUFARIKI KWENYE MLIPUKO

Mlipuko umetokea leo, Januari 31 asubuhi ktk eneo la Mandera baada ya Daladala kukanyaga Bomu lililokuwa limetegwa ardhini

Mlipuko umetokea Siku 2 baada Ufaransa kutoa tahadhari ya Shambulio

Soma - https://jamii.app/ManderaBombKE

#JFMatukio
TANGA: Watu watano wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na mapanga, huku wengine 3 wakijeruhiwa katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Kijiji cha Kibirashi na Elerai Wilayani Kilindi

Mgogoro wa ardhi umetajwa kuwa chanzo cha mapigano

Soma - https://jamii.app/5WauawaTanga

#JFMatukio
Polisi imetoa ufafanuzi wa tukio la Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Grayson Mahembe kujinyonga katika mahabusu alipokuwa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji

> Jeshi limesema ili kutoharibu ushahidi watuhumiwa wa kesi hii hawakuwekwa pamoja

Soma https://jamii.app/AskariAliyejiua
NIGERIA: Kundi la Vijana walio chini ya mwamvuli wa Bunge la Vijana wa Kaskazini mwa Nchi hiyo limeshinikiza Bilionea Aliko Dangote kugombea Urais mwaka 2023

Wamesema wafanyabiashara wanaojua namna ya kupata faida ndiyo wanaopaswa kuitawala #Nigeria

Soma https://jamii.app/DangoteNigeria
HISTORIA: MFAHAMU KWAME NKRUMAH, RAIS WA KWANZA WA GHANA

Alizaliwa Septemba 21, 1909 huko Nkroful, Ghana na kufariki Aprili 27, 1972. Aliongoza #Ghana kupata Uhuru (1957) na kuwa Rais wa kwanza Nchini humo

Nkrumah alikuwa Mwasisi wa wazo la kuundwa kwa Shirikisho la Nchi za Afrika, wazo lililozaa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU, sasa AU). Aliondolewa Madarakani kwa Mapinduzi ya Kijeshi Mwaka 1966

Fahamu zaidi - https://jamii.app/KwameNkrumah

#JFHistoria
#Tokophobia ni hofu ya kubeba Ujauzito na inaweza kumsababisha Mwanamke kuepuka kuzaa. Tatizo hili huainishwa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza (Primary Tokophobia) ni Hofu inayompata Mwanamke ambaye hajawahi kuzaa

Kundi la pili (Secondary Tokophobia) ni Hofu/Uoga unaompata Mwanamke ambaye alishabeba Ujauzito. Huyu hupata Hofu kutokana na mambo aliyoyapitia katika Mimba ya awali.

#JFMaarifa
LAMPARD ATHIBITISHWA KUWA KOCHA WA EVERTON

- Everton imemthibitisha Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard kuwa Kocha wake hadi Juni 2024

- Lampard alianza Ukocha katika Klabu ya Derby County mwaka 2018, kabla ya kuinoa Chelsea mwaka 2019 hadi 2021

#JFSports
MDAU: JINSI YA KUTUNZA/KUIMARISHA AFYA YA AKILI YA MTOTO

Ni muhimu kutenga muda wa kuzungumza na kumsikiliza Mtoto kila siku. Pia, mhimize kujenga Uhusiano mzuri na Familia na Marafiki

Epuka kufoka na kumpa vitisho: Watoto wanapokosea, usipige kelele. Waeleweshe nini kimekwenda vibaya kisha uwaoneshe njia sahihi

Soma - https://jamii.app/ChildMentalHealth
#MentalHealth
NJIA ZA KUPATA MAFANIKIO KATIKA MASOMO

Mshiriki wa #StoriesOfChange anashauri Wanafunzi kumtanguliza Mungu. Pia, waende na muda kwa kuweka malengo mwanzo wa muhula wa masomo

Chagua marafiki wanaokusaidia kukua na tambua lengo kuu la kuwa shuleni

Soma - https://jamii.app/MafanikioMasomo

#JFElimu
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Soko la Mbuyuni lililopo Moshi mjini, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, 01 Februari 2022

Shuhuda ambae ni Mlinzi wa Soko la Mbuyuni Hassan Sulemani amesema moto ulianza majira ya saa 7:30 usiku ambapo moto huo ulianza kwenye vibanda vya katikati ya soko.

#JFMatukio
MALI: BALOZI WA UFARANSA APEWA SAA 72 ZA KUONDOKA

Mali imemfukuza Balozi huyo kuhusiana na matamshi ya kiuadui yaliyotolewa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa alisema Utawala wa Kijeshi wa #Mali ni haramu na maamuzi yake siyo ya Uwajibikaji

Soma https://jamii.app/FranceAmbMali

#JFDiplomasia
👍1
MSUMBIJI: KIONGOZI WA WANAMGAMBO ANAYEDAIWA NI MTANZANIA AUAWA

> Tuahil Muhidim aliyeuawa Januari 30 anadaiwa kuongoza mashambulizi na kuushikilia mji wa Macimboa da Pria mwaka 2020

> Pia, anadaiwa kuteka Watawa 2 wa Kibrazili kwa wiki zaidi ya 3

Soma https://jamii.app/KiongoziWanamgambo

#JFMatukio
BUNGENI: UCHAGUZI WA SPIKA KUFANYWA LEO

Wagombea ni Dkt. Tulia Ackson, Abdulla Mohammed Said, Mhandisi Aivan Jackson Maganza, David Mwaijolele, George Gabriel Bussungu, Kunje Ngombale Mwiru, Maimuna Kassim, Ndonge Ndonge na Saidoun Abrahaman Khatib

Soma https://jamii.app/Uspika2022

#Democracy
DKT. TULIA ACKSON AJIUZULU NAFASI YA NAIBU SPIKA

Dkt. Tulia Ackson amejiuzulu nafasi ya Naibu Spika baada ya kuteuliwa na Chama cha CCM kugombea nafasi ya Uspika

Taarifa ya kujiuzulu imetolewa na Katibu wa Bunge mbele ya Wabunge leo kwenye zoezi la Uchaguzi wa Spika

#Democracy
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, akichukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine

Yunus alikuwa Mtayarishaji wa Vipindi na Mtangazaji wa BBC

Soma - https://jamii.app/ZuhuraIkulu

#Governance