JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GAMBIA: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA KUBATILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mpinzani Ousainou Darboe alisema Kampeni zilihusisha rushwa

Ilidaiwa Rais Adama Barrow au Wanachama wa Chama chake waliwapa Fedha/Zawadi Wanakijiji ili wapate kura

Soma - https://jamii.app/UchaguziGambia
MAREKANI: WASIO NA DALILI ZA COVID-19 KUJITENGA KWA SIKU TANO

Waliokutwa na Virusi baada ya kujitenga kwa Siku 10 wanapaswa kuvaa Barakoa kwa Siku 5 wanapokuwa karibu na wengine

#Omicron inachukua 73% ya maambukizi ya Corona Nchini Marekani

Soma https://jamii.app/5DaysNteenUS
#UVIKO3
URUSI: MAHAKAMA YAAMURU SHIRIKA LA HAKI ZA BINADAMU KUFUNGWA

Shirika la Memorial limefungwa kwa kuvunja Sheria za kujisajili kama wakala wa Mashirika ya kigeni

Urusi kuna ukandamizaji dhidi ya upinzani na makundi ya Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/MemorialClosed
#HumanRights
GAVANA BoT: HUWEZI KUTUMIA FEDHA ZA NDANI KWENYE MIRADI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amesema Mikopo haikopwi kwa ajili ya kula bali kufanya Miradi ambayo itaendelea kuzalisha na kuleta uhimilivu mzuri wa deni

Akihojiwa na Clouds Media amesema "Nchi haiwezi ikaweka rehani Watu au rasilimali zake na inazitumia ili Serikali iendelee kupata kipato"

Soma - https://jamii.app/LuogaMikopo

#JFLeo
HONG KONG: Polisi wamewakamata Watu sita kutoka Tovuti ya Stand News kwa tuhuma za njama ya kuchapisha uchochezi

Ofisi ya Tovuti hiyo imevamiwa na Maafisa wapatao 200. Polisi wasema waliidhinishwa kukamata nyenzo muhimu za Habari

Soma - https://jamii.app/StandNewsHK

#PressFreedom
NACHINGWEA: Wananchi waliouziwa Ardhi kuanzia Juni 2020 mpaka Desemba 2021 wametakiwa kurudisha Ardhi kwani mauziano hayo ni batili

DC Hashim Komba amesema Serikali ilisitisha ugawaji wa Ardhi tangu Juni 2020 mpaka pale itakapotoa mwongozo rasmi

Soma - https://jamii.app/ViwanjaNachingwea
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema athari inayotokana na Kirusi cha Corona aina ya Omicron bado ipo juu. Maambukizi ulimwenguni yameongezeka kwa 11% wiki iliyopita

Ushahidi waonesha #Omicron ina ukuaji wa haraka zaidi

Soma - https://jamii.app/WHOOmicron

#UVIKO3
SOMALIA: JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAINGILIA MVUTANO WA RAIS NA WAZIRI MKUU

Rais Mohamed Abdullahi alimsimamisha kazi Waziri Mkuu, Mohammed Roble kufuatia tuhuma za ufisadi, kitendo ambacho Waziri Roble amesema ni jaribio la Mapinduzi

Soma - https://jamii.app/SiasaSomalia
Marekani inapanga kuchukua hatua mpya ili kushinikiza Utawala wa Kijeshi Nchini #Myanmar kurudisha Serikali ya Kiraia kutokana na kukandamizwa kwa Wapinzani

UN imetahadharisha juu ya ongezeko la visa vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/USvsMyanmar

#Democracy
DARFUR, SUDAN: GHALA LA WFP LAVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA

Ghala la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilikuwa na Tani 1,900 za Chakula cha Msaada

Darfur imeshuhudia ongezeko la mapigano tangu Oktoba kutokana na migogoro ya ardhi na maji

Soma - https://jamii.app/WFPLooted
ZANZIBAR: Rais Hussein Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu

Yusuph Nassor ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Viwango (ZBS) na Dkt. Idrissa Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi

Soma - https://jamii.app/UteuziZnz3
ASHRAF GHANI: SIKUWA NA NAMNA NYINGINE ZAIDI YA KUKIMBIA AFGHANISTAN

Rais wa zamani wa #Afghanistan amekanusha kuwepo mazungumzo ya kuwaachia #Taliban Madaraka kwa amani, kama walivyodai Maafisa wa zamani wa Afghanistan na Marekani

Soma - https://jamii.app/AshrafGhaniFlee
#JFLeo
AFRIKA KUSINI YALEGEZA KANUNI ZA KUDHIBITI COVID-19

Serikali inaamini Nchi imepita kilele cha Wimbi la Nne

Marufuku ya watu kuwa nje kuanzia saa sita usiku imeondolewa. Mikusanyiko ya ndani haitakiwi kuzidi watu 1,000 na nje watu 2,000

Soma - https://jamii.app/OmicronSA

#UVIKO3
👍1
CHINA: WACHEZAJI MPIRA WAPIGWA MARUFUKU KUCHORA TATTOO

Mamlaka ya Michezo Nchini #China imepiga marufuku Wachezaji wa Timu ya Taifa na Wanamichezo wengine kujichora #Tattoo na kuamuru walionazo waziondoe ili kuwa mfano mzuri kwa Jamii

Soma - https://jamii.app/TattooBanChina
#Sports
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kingine cha miaka 6

Patience Kilanga Ntwina ateuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Soma - https://jamii.app/RaisUteuzi4
Baadhi ya aliyozungumza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake kwa Taifa kuelekea mwaka mpya 2022

Zaidi, soma - https://jamii.app/Hotuba2022

#JFLeo
RAIS SAMIA: KIRUSI CHA OMICRON KIMEINGIA NCHINI

Akihutubia Taifa, amesema Kirusi hicho kinaenea kwa kasi kubwa na tayari kimeingia hapa Nchini. Amewasisitiza wananchi kuchukua tahadhari

Ametoa wito kwa watu kupata chanjo akisema, "Natambua chanjo haizuii mtu kupata maambukizi ila inapunguza makali ya ugonjwa huo. Niwahimize wananchi kuchanja, chanjo zipo"

#UVIKO3
- Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watendaji wa JamiiForums tunakutakia Mapokezi mema ya Mwaka mpya wa 2022

- Tunathamini mchango wako na thamani uliyonayo kwetu huku tukiamini utaendelea kuwa nasi ndani ya Mwaka 2022

#JamiiForums #HappyNewYear2022