JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JF SCHEDULED MAINTENANCE

Kuanzia saa Sita Kamili hadi saa Nane Kamili usiku wa leo tovuti ya JamiiForums.com itakuwa haipatikani kufuatia maboresho yanayotarajiwa kufanyika wakati huo

Tunashukuru kwa kuendelea kutumia huduma zetu na asante kwa ushirikiano wako

#JamiiForums
MAREKANI: Wamarekani 40,000 wametapeliwa kupitia matangazo ya kujifanya Kampuni inatoa zawadi. Utapeli unaozidi kukua kwa miaka 3 iliyopita

Kwa miezi tisa ya mwanzo ya Mwaka 2021 jumla ya Dola milioni 148 sawa na Tsh. Bilioni 340.6 zimetapeliwa

Soma - https://jamii.app/UtapeliWaZawadi
ELON MUSK APINGA KULAZIMISHA WATU KUPATA CHANJO YA #COVID19

Mmiliki wa Kampuni ya #Tesla amesema kulazimisha Watu kupata Chanjo au kuwafukuza kazi si sahihi

Ametoa wito Watu washawishiwe kupata Chanjo badala ya kulazimishwa

Soma - https://jamii.app/ElonMusk

#UVIKO3
UFUATILIAJI WA USALAMA WA CHANJO ZA COVID-19 NI ENDELEVU

Shirika la Afya (WHO) limesema ufuatiliaji wa usalama ni muhimu kitaifa, kikanda na kimataifa

Mchakato unahusisha wadau na Wataalamu wa Afya ili kuhakikisha usalama kila mara

Soma - https://jamii.app/ChanjoUfuatiliaji

#UVIKO3
Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake 3 inatarajiwa kuendelea leo

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya aliyepinga Mahakama kupokea kielelezo kinachodaiwa kuwa ni maelezo yake

Soma - https://jamii.app/UamuziPingamizi
SUDAN: Polisi wametumia Mabomu ya Machozi kutawanya Waandamanaji waliokusanyika karibu na Makazi ya Rais Jijini Khartoum

Tangu Mapinduzi kufanyika Nchini humo Oktoba 25, watu wapatao 50 wameripotiwa kupoteza maisha huku mamia wakijeruhiwa

Soma - https://jamii.app/KhartoumProtests

#JFLeo
GHANA: Mamlaka nchini Ghana zimetangaza kupiga faini Mashirika ya Ndege yatakayosafirisha Raia wa Kigeni ambao hawajapata chanjo

> Mashirika yatalipa Dola 3,500 (sawa na Tsh. Milioni 8) kwa kila msafiri asiyepata chanjo ya #COVID19

Soma https://jamii.app/WasichanjaGhana

#UVIKO3
UPDATE: Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi yatupilia mbali Hoja zote 7 za Utetezi ktk pingamizi la kuitaka Mahakama isipokee kielelezo chenye maelezo ya Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya

Jaji Joachim Tiganga amepokea kielelezo

Soma https://jamii.app/UamuziPingamizi
MDAU: TABIA UNAZOTAKIWA KUACHA ILI KUTOKA ULIPO NA KUSONGA MBELE

1) Kujilinganisha na Wengine: Tabia hii ni mwizi wa furaha yako. Mtu pekee wa kujilinganisha naye ni wewe mwenyewe

2) Kurudia Makosa: Kukosea kupo katika maisha na hilo lipo wazi, ila jifunze kwa makosa kisha songa mbele

3) Kushindwa kusema Hapana: Kama unataka kuwa na maisha ya wasiwasi na yasiyo na furaha basi shindwa kusema Hapana

Soma - https://jamii.app/TabiaSOC

#StoriesOfChange
Baadhi ya Wawasilishaji na Wadau walioshiriki katika Warsha ya kujadili Mapendekezo ya Mabadiliko ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni (2020) ulioandaliwa na Jamii Forums kwa kushirikiana na CIPESA - Uganda

Warsha imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Four Points by Sheraton (zamani New Africa Hotel) jijini Dar es Salaam leo

#JamiiForums
TUNISIA: SHUGHULI ZA BUNGE KUSITISHWA HADI UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA

Tangu aliposimamisha Bunge na kumfukuza aliyekuwa Waziri Mkuu, Rais Kais Saied ameendelea kushikilia Madaraka akisisitiza uamuzi huo ulihitajika kutokana na mwenendo mbaya wa Siasa

Soma - https://jamii.app/RaisKaisBunge
HALI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA CAG KWA OR - TAMISEMI

Ripoti ya Ukaguzi 2019/20 inaonesha kati ya Mapendekezo 15 yaliyotolewa na CAG 2018/19, Ofisi ya Rais – TAMISEMI haikutekeleza pendekezo lolote kikamilifu

Mapendekezo 6 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, Mapendekezo 5 hayajatekelezwa na Mapendekezo 4 yamejirudia

Soma - https://jamii.app/UtekelezajiMapendekezo

#JFUwajibikaji