JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Yanayojiri katika Mjadala wa "Miaka 60 Ya Uhuru: Mchango wa Digitali katika Uhuru wa Kujieleza, Demokrasia na Utawala Bora" kupitia Clubhouse

Ungana Nasi - https://www.clubhouse.com/room/PA0oo9ge
Maoni kadhaa yaliyotolewa katika Mjadala wa "Miaka 60 Ya Uhuru: Mchango wa Digitali katika Uhuru wa Kujieleza, Demokrasia na Utawala Bora" uliofanyika Clubhouse

#JamiiForums
WHO: KUKABILI TISHIO JIPYA LA COVID-19 NI VEMA KILA MMOJA KUCHANJWA

WHO imetoa wito kwa Mataifa tajiri kutohodhi Chanjo na kutatiza usambazaji wake huku ikisisitiza kuacha kutolewa Chanjo za nyongeza ili kupeleka Chanjo kwa Mataifa Masikini

Soma - https://jamii.app/WHOCoronaVacc
#UVIKO3
RIPOTI: WANAHABARI 293 WAMEFUNGWA MWAKA 2021

Pia, Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ) imesema takriban Waandishi wa Habari 24 waliuawa kwa sababu ya kazi yao

Waandishi 50 bado wapo gerezani nchini #China

Soma - https://jamii.app/RipotiCPJ

#PressFreedom #JamiiForums
MEXICO: Takriban watu 53 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafirishwa kupata ajali

Mamlaka zinasema zaidi ya watu 100 wanaosemekana kuwa wahamiaji kutoka Amerika ya Kati, walijazwa kwenye lori hilo

Soma - https://jamii.app/53DeadMexico
CHANJO YA COVID-19 HAIKUZUII KUPATA CHANJO NYINGINE

Kituo cha CDC kinasema waliopata Chanjo ya #COVID19 wanaweza kupokea Chanjo za maradhi mengine

Mwitikio wa Chanjo mwilini hautofautiani endapo mtu atapata chanjo ya aina moja au tofauti

Soma https://jamii.app/ChanjoTofauti

#UVIKO3
MDAU: KUFANYA MAKOSA NI JAMBO LA MUHIMU KWA BINADAMU

Anasema Watu wengi hawana Maendeleo binafsi hususani Kiuchumi kwa kuwa wanaogopa kukosea na kuendelea kufanya mambo yale yale

Kufanya makosa humsaidia Mtu kujitambua, kugundua kipaji chake, kuleta ugunduzi, kutatua changamoto za Maisha, kuleta Mawazo mbadala pamoja na kuboresha Afya ya Ubongo na Akili

Msome - https://jamii.app/FaidaMakosa

#StoriesOfChange
MGAWANYO WA MAJUKUMU KATI YA MUME NA MKE NDANI YA NDOA

Kifungu cha 63 cha Sheria ya Ndoa kinaweka wajibu kwa Mume kumtunza Mke wake kwa kumpa mahitaji yote muhimu kama Mavazi, Chakula na Malazi kulingana na uwezo wake

Mke pia atakuwa na jukumu hilo tu ikiwa Mume hawezi kutunza Familia kwasababu za ugonjwa hasa wa Kiakili na Ulemavu.

#JamiiForums #16DaysOfActivism
Desemba 10 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya #HakiZaBinadamu

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres amesema vitisho vipya vimeibuka kwa Haki za Msingi za Binadamu. Mamilioni ya Watoto wanakosa Haki yao ya kupata Elimu. Ukosefu wa Usawa nao unaongezeka

#HumanRightsDay
IKULU, DAR: Tanzania na Kenya zimekubaliana masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha Mpaka, kushirikiana kupambana na COVID-19 na kushirikiana kwenye Sekta ya Utalii

Rais Samia ameeleza hayo baada ya Utiaji Saini wa Hati za Makubaliano na Ushirikiano

Soma -https://jamii.app/TZKEMakubaliano
Upungufu wa Miundombinu ya Shule huathiri ufanisi wa utoaji #Elimu kwa Shule za Sekondari hasa kwa Wanafunzi wa Jinsia ya Kike

Ili kutatua changamoto za upungufu wa Miundombinu zilizoibuliwa na CAG, Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI zinashauriwa kutoa kipaumbele zaidi kwenye upangaji na utoaji wa Bajeti ya Miundombinu

Soma - https://jamii.app/MiundombinuShule

#JFUwajibikaji
MAKABIDHIANO YA VYUMBA VYA MADARASA KUFANYIKA DESEMBA 31

Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameongeza siku 15 kwa Halmashauri zote kukamilisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa

Madarasa yatakabidhiwa Desemba 31, 2021 badala ya Desemba 15 ya awali

Soma - https://jamii.app/MadarasaDec31