JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: VICHOCHEO VYA MABADILIKO ILI TANZANIA TUNAYOITAKA IPATIKANE

1) Utawala wa Sheria na wa Haki: Kuna umuhimu wa kuwa si tu na Katiba Mpya, bali Katiba bora inayoweka misingi mizuri ya mgawanyo mzuri wa madaraka na mamlaka na uendeshaji wa shughuli za Serikali na Sera za Taifa

2) Uhuru wa Maoni: Wananchi wana Haki ya kutoa maoni na kufikisha ujumbe wao kwa Mamlaka husika kwa njia zinazokubalika Kikatiba

Soma - https://jamii.app/MabadilikoTZ

#StoriesOfChange
CHINA YATAJWA KUWA MKAMATAJI MKUBWA ZAIDI WA WAANDISHI WA HABARI

Ripoti ya Reporters Without Borders inasema Wanahabari 127 wanashikiliwa hivi sasa

China imekuwa ikifanya kile kilichotajwa kama kampeni ya ukandamizaji dhidi ya Uandishi wa Habari

Soma - https://jamii.app/RipotiRSFChina
Katika siku za karibuni mitandao ya kijamii na Mifumo ya Kidijitali imekuwa maeneo muhimu kwa Jamii ya Tanzania kutumia #UhuruWaKujieleza na kupigania haki zao nyingine

Tukifurahia Miaka 60 ya Uhuru wa #Tanganyika ni kwa kiwango gani tumeweza kuitumia mifumo ya Dijitali katika kusimamia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala Bora?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse Desemba 9, 2021

#JamiiForums #DigitalSpaces #Democracy
UJERUMANI: Bunge limepiga Kura na kumpitisha Olaf Scholz wa Social Democrat Party kuwa Kansela mpya wa Nchi hiyo baada ya Angela Merkel ambaye ameitumikia kwa miaka 16

Ataongoza Serikali mpya ya Mseto kati ya SPD na vyama vingine viwili

Soma - https://jamii.app/ScholzGermany

#JFLeo
UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Mwaka 2019/20 CAG aliainisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa 51 zilikuwa na upungufu wa Miundombinu ya Shule

Upungufu mkubwa ulikuwa kwenye nyumba za Walimu na majengo ya Utawala

Soma - https://jamii.app/MiundombinuShule

#JFUwajibikaji
RAIS KENYATTA KUFANYA ZIARA YA SIKU 2 TANZANIA

Rais wa Kenya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Uhuru zitakazofanyika Dar es Salaam

Vilevile akiwa Nchini, Rais Uhuru Kenyatta na Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa Mikataba nane

Soma https://jamii.app/ShereheUhuru

#JFLeo
#BANGLADESH: Mahakama imewahukumu adhabu ya kifo Wanafunzi 20 wa Chuo Kikuu kwa mauaji ya Kijana aliyeikosoa Serikali kwenye Mitandao ya Kijamii

Abrar Fahad alimkosoa Waziri Mkuu, Sheikh Hasina kwa kusaini makubaliano ya kugawana Maji na #India

Soma - https://jamii.app/FahadMurderBang
KUELEKEA MIAKA 60 YA UHURU: RAIS SAMIA AHUTUBIA TAIFA

- Rais Samia Suluhu Hassan anahutubia Taifa kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara)

- Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo Desemba 09, 1961

Fuatilia: https://jamii.app/SamiaHotuba-Dec21
Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka 60, Tanzania imefanikiwa kujenga Uchumi hadi kufikia Nchi ya Uchumi wa Kati wa Chini mapema kuliko ilivyokadiriwa kwenye Malengo ya Dira ya Taifa

Asema, "Wastani wa Pato kwa Mtu kwa mwaka 1961 lilikuwa Tsh. 776 na kwa mwaka jana 2020 ni Tsh. 2,653,790"

Soma - https://jamii.app/SamiaHotuba-Dec21
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye Miundombinu ya Umeme, akieleza kuwa kabla ya Uhuru Nchi ilikuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 17.5 za Umeme lakini sasa ni Megawati 1,909

Amesema, "Lengo letu ni kuendelea kuongeza uzalishaji wa umeme ili kuendana na malengo ya kugeuza Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda"

Soma - https://jamii.app/SamiaHotuba-Dec21

#Miaka60YaUhuru
AFYA: Rais Samia Suluhu Hassan amesema mwaka 1961 kulikuwa na Hospitali 113, Vituo vya Afya 22 na Zahanati 1,188. Hivi sasa Nchi ina jumla ya Zahanati 7,163, Vituo vya Afya 929 na Hospitali 369

Asema, "Tunaendelea kuboresha sekta hii kwa kuhakikisha tunaajiri Madaktari wengi zaidi ili tuweze kufikia viwango vya WHO"

Soma - https://jamii.app/SamiaHotuba-Dec21

#Miaka60YaUhuru
RAIS SAMIA: TUNA MFUMO BORA WA KUWEKA VIONGOZI MADARAKANI

Amesema sote ni mashahidi Tanzania imekuwa na Mfumo bora wa kuweka Viongozi madarakani unaoheshimiwa na imara kupitia Chaguzi zinazofanyika kila baada ya miaka mitano

Ameeleza, "Wananchi wamekuwa wakitekeleza Haki yao ya msingi ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka"

Soma - https://jamii.app/SamiaHotuba-Dec21

#Miaka60YaUhuru
Katika siku za karibuni mitandao ya kijamii na Mifumo ya Kidijitali imekuwa maeneo muhimu kwa Jamii ya Tanzania kutumia #UhuruWaKujieleza na kupigania haki zao nyingine

Tukifurahia Miaka 60 ya Uhuru wa #Tanganyika ni kwa kiwango gani tumeweza kuitumia mifumo ya Digitali katika kusimamia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala Bora?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse Desemba 9, 2021

#JamiiForums #DigitalSpaces #Democracy
MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA

Tanganyika ilipata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza Desemba 09, 1961. Harakati za Uhuru ziliongozwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere

Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara imetajwa kuchangia kuleta mafanikio mbalimbali yakiwemo; Kujenga Umoja wa Kitaifa, Kuimarisha Uchumi, kuboresha Huduma za Kijamii na kuimarisha Demokrasia na Utawala wa Sheria

Unazungumziaje miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika?

#Miaka60YaUhuru #Tanzania60
Katika siku za karibuni mitandao ya kijamii na Mifumo ya Kidijitali imekuwa maeneo muhimu kwa Jamii ya Tanzania kutumia #UhuruWaKujieleza na kupigania haki zao nyingine

Tukifurahia Miaka 60 ya Uhuru wa #Tanganyika ni kwa kiwango gani tumeweza kuitumia mifumo ya Digitali katika kusimamia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala Bora?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse Desemba 9, 2021

#JamiiForums #DigitalSpaces #Democracy
Matukio Katika Picha: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaongoza Viongozi wa Kitaifa na Kimataifa pamoja na Wananchi katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

#Miaka60YaUhuru