JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: WASAFIRI WOTE KULAZIMIKA KUWA NA CHETI CHA CHANJO

Kenya imetangaza hatua kali zinazolenga kuzuia kuenea kwa aina mpya ya #COVID19

Waziri wa #Afya amesema ni lazima kwa wageni kuwa na cheti cha Chanjo kabla ya kuingia Nchini humo

Soma - https://jamii.app/CertVaccineKE
#UVIKO3
MYANMAR: AUNG SAN SUU KYI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 4

Kiongozi huyo aliyetolewa Madarakani na Jeshi akutwa na hatia ya uchochezi na kuvunja Kanuni za Corona

Aung San Suu Kyi yupo kifungo cha nyumbani tangu Februari, na anakabiliwa na Mashtaka 11

Soma https://jamii.app/AungSanSuu4
COVID-19: DALILI AMBAZO HUWAPATA WATU WACHACHE

WHO imetaja dalili hizo ni Kupata maumivu ya kichwa, Kuwashwa kooni, Maumivu mwilini, kuhara, upele au vidole kubadilika rangi na macho kuwa mekundu

Unasisitizwa kwenda Kituo cha Afya ukizipata

Soma https://jamii.app/LessCommon

#UVIKO3
Vitendo vya Rushwa ya Ngono vinaendelea kushamiri kutokana na Uelewa mdogo wa Jamii juu ya #Sheria zinazozuia rushwa hiyo

Pia, Watendewa huogopa kutoa taarifa kwa hofu ya kuachishwa kazi, kunyimwa huduma, kuachishwa masomo au kufelishwa kwa makusudi kwa Wanafunzi hasa wa Vyuo Vikuu

Je, umewahi kuombwa Rushwa ya Ngono au kushuhudia Mtu akiombwa Rushwa ya Ngono?

#16DaysofActivism2021
MDAU: UMUHIMU WA MTU/JAMII KUIFAHAMU AFYA YA AKILI

1. Husaidia kuweza kutambua changamoto ndogondogo zinazoweza kupelekea tatizo la Akili ikiwemo Msongo wa Mawazo ambao usipopatiwa ufumbuzi, hupelekea tatizo la Akili liitwalo Sonona (#Depression)

2. Kuitambua Afya ya Akili kunasaidia kupambana na shida ya kiwewe (Post Traumatic #Stress Problem) inayosababishwa na majanga mbalimbali ikiwemo kufiwa na Mtu wa karibu sana

Msome - https://jamii.app/BenefitsAfyaAkili

#StoriesOfChange
AFRIKA KUSINI: Rais Cyril Ramaphosa anasema Hospitali zinaandaliwa kulaza wagonjwa zaidi, wakati Kirusi cha #Omicron kikiendelea kuenea na kupelekea Wimbi la 4

Amewataka Wananchi kuvaa barakoa na kuepuka misongamano ili kupunguza maambukizi

Soma https://jamii.app/Wave4SA

#UVIKO3
GOBA, DAR: Watu wanne (Wanawake 2 na Wanaume 2) wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 17 wakijeruhiwa baada ya jengo lililokuwa linajengwa eneo la Goba kwa Awadhi Jijini Dar es Salaam kuangukia nyumba za jirani

Soma - https://jamii.app/GobaVifo4

#JFLeo
LUDEWA: AJINYONGA BAADA YA KUTOTAJWA JINA KWENYE MISA

Raban Razalo (48) amejinyonga na waya kwa madai ya kutoridhishwa na kitendo cha Mchungaji kutomtaja jina wakati wa misa ya shukrani iliyofanywa na Mkewe baada ya Mtoto wao kupona mguu

Soma - https://jamii.app/BabaKifoPadri
RIPOTI: WATENGENEZAJI WA SILAHA HAWAJAPATA ANGUKO LA KIUCHUMI

Kampuni 100 za juu zimeshuhudia ongezeko la faida kwa 1.3% licha ya Uchumi wa Dunia kushuka kwa zaidi ya 3%

Marekani inaongoza ktk utengenezaji na mauzo ikiwa na Kampuni 41 kati ya 100

Soma - https://jamii.app/SIPRI2021
ETHIOPIA: Serikali imesema Vikosi vyake vimeidhibiti tena Miji ya Dessie and Kombolcha ambayo ilishikiliwa na wapiganaji wa TPLF

Hofu ya Wapiganaji kuingia Mjini #AddisAbaba imepelekea Nchi kadhaa kuwahimiza Raia wao kuondoka Nchini humo

Soma - https://jamii.app/EthiopiaWaasi
Shirika la Afya Duniani limesema vikwazo ktk Huduma za Afya vilivyotokana na COVID-19 vimepelekea vifo 69,000 zaidi vya Malaria mwaka 2020

Takriban watu 627,000 duniani (wengi watoto) kutoka Mataifa ya Afrika walifariki kwa Malaria mwaka 2020

Soma https://jamii.app/WHOMalaria
MARUDIO YA MITIHANI YA UTABIBU NTA LEVEL 5 KUFANYIKA KUANZIA DESEMBA 13

Mitihani itafanyika pamoja na Mitihani ya marudio kwa Wanafunzi ambao hawakufanya vizuri Mitihani ya awali

Ratiba za Mitihani kwa kozi zote za #Afya zimetumwa Vyuoni

Soma - https://jamii.app/NTALevel5Dec13

#JFLeo
Ndoa za Utotoni ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu kwa Wasichana. Sheria ya Ndoa bado inaruhusu Mtoto wa Kike kuolewa na umri wa miaka 15

Takwimu za Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS), 2015-2016 zilionesha 36% ya Mabinti wenye miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla hawajatimiza miaka 18

Soma - https://jamii.app/SheriaNdoaWatoto

#16DaysOfActivism2021
MDAU: MFUMO WA ELIMU UBADILISHWE, MIAKA YA KUSOMA IPUNGUZWE

Anasema Jamii ya Watanzania inaamini Mtoto mwadilifu ni yule anayefuata njia sahihi za Masomo. Inamtaka aanze kwa kusoma mpaka Darasa la Saba kisha afaulu hadi Chuo Kikuu

Anaeleza, kutokana na mabadiliko ya teknolojia na jamii kiujumla, ni lazima kuwepo namna ya kubadili Mfumo mzima wa Elimu hasa katika kupunguza idadi ya miaka ambayo Wanafunzi hutumia kwenye masomo

Soma - https://jamii.app/MfumoElimuSOC

#StoriesOfChange
SERIKALI KUFANYA MSAKO KWA WATAKAOFUNDISHA WATOTO WAKATI WA LIKIZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Shule zote za Serikali na Binafsi zitapelekewa Barua kuweka msisitizo wa utekelezaji wa agizo hilo

Asema Maafisa Elimu wamesoma somo la Saikolojia na wanajua umuhimu wa mapumziko katika makuzi ya Mtoto hivyo hawapaswi kufungia Macho vitendo hivi

Soma - https://jamii.app/MsakoShuleLikizo
Wakimbizi wa Rohingya walio Uingereza na Marekani wamefungua Mashtaka dhidi Kampuni ya Meta (Facebook). Wanadai Fidia ya Dola za Marekani Bilioni 150 wakisema Mitandao ya Kampuni hiyo ilichochea ghasia dhidi yao

Soma - https://jamii.app/FBSued
KENYA: POLISI AUA WATU 6 AKIWEMO MKEWE KISHA KUJIUA

Benson Imbatu alienda nyumbani akiwa na AK47 kisha kuanzisha ugomvi na Mkewe, Carol Imbatu

Majirani na Waendesha Pikipiki waliouawa walisogea karibu na nyumbani kwake baada ya kusikia risasi

Soma - https://jamii.app/PolisiAua6
USINYWE POMBE KUPINDUKIA BAADA YA KUPATA CHANJO YA COVID-19

WHO inasema unywaji pombe kistaarabu baada ya Chanjo hauna madhara

Inashauriwa kunywa kistaarabu walau kwa wiki 2 baada ya kupata chanjo ili kuipa nafasi ifanye kazi kwa ufanisi

Soma - https://jamii.app/ChanjoPombeKiasi

#UVIKO3
MDAU: SHULE ZINATUWEKA KATIKA UMASIKINI PASIPO KUJUA

Anasema Shule hazitufundishi kuhusu Maisha. Wanafunzi wanatumia miaka mingi Shuleni bila kufundishwa jinsi ya kupata Fedha, Afya ya Akili, Kodi, usimamizi wa muda n.k

Una maoni gani kuhusu hoja za Mshiriki huyu wa 'Stories Of Change'?

Msome zaidi - https://jamii.app/ShuleUmasikini
#StoriesOfChange
Mapungufu yaliyobainishwa na CAG 2019/20 katika Ukaguzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu yamesababisha athari mbalimbali

Kiasi ambacho hakikurejeshwa na kiasi ambacho hakijatengwa kimefikia Tsh. Bilioni 30.9. Kama kiasi hicho kingekopeshwa kwa vikundi vya watu 10 na kila kikundi kupewa Tsh. Milioni 5, kingeweza kuwasaidia watu 61,800

Soma - https://jamii.app/MfukoUwezeshaji

#JFUwajibikaji