JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Maoni ya wadau mbalimbali katika Mjadala wa "Wanafunzi kuendelea na Masomo wakati wa Likizo" unaoendelea Clubhouse

#JamiiForums
Baadhi ya masuala aliyozungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu katika Mjadala uliofanyika kupitia Clubhouse

#JamiiForums
MALEZI: ULINZI NI MUHIMU KWA WATOTO

Familia ndicho chanzo cha kwanza cha Ulinzi wa Mtoto. Wazazi/Walezi wana jukumu la kutengeneza mazingira ya Nyumbani ambayo ni salama na yenye upendo

Shule na Jamii zina jukumu la kutengeneza mazingira ya nje ya Nyumbani ambayo ni salama na rafiki kwa Mtoto

Soma - https://jamii.app/UlinziWatoto
#ChildSafety
GAVI YATOA DOLA MILIONI 115.7 KWA AJILI YA CHANJO YA MALARIA AFRIKA

Muungano wa Chanjo Ulimwenguni, Gavi umeidhinisha Fedha hizo kwa utoaji Chanjo kwa Watoto Kusini mwa Jangwa la Sahara

Chanjo ya kwanza ya Malaria iliidhinishwa na WHO Oktoba 2021

Soma - https://jamii.app/MalariaChanjo
MAENEO HATARISHI KWA RUSHWA YA NGONO

1. Sehemu za Kazi: Rushwa ya Ngono kazini ni pamoja na waajiri kutoa ajira kwa Wanawake na faida nyingine kama vile kupandishwa cheo, nyongeza ya mshahara, siku za kupumzika kwa kubalishana na Ngono

2. Ofisi za Umma: Ofisi zinazotoa huduma mbalimbali za Usajili wa Vyeti, utoaji wa Leseni, Vitambulisho, Pasi za Kusafiria nk. Baadhi ya watumishi wanaweza kuomba Rushwa ya Ngono kwa kubadilishana na upatikanaji wa haraka wa nyaraka hizo

Soma - https://jamii.app/HatariRushwaNgono

#16DaysofActivism2021
UJERUMANI: Ili kupambana na aina mpya ya Kirusi cha #Omicron, Kansela Angela Merkel amesema watakaoruhusiwa kuingia katika migahawa na maeneo ya starehe ni waliopata Chanjo tu

Amesema Chanjo zinaweza kuwa lazima ifikapo Februari 2022

Soma - https://jamii.app/ChanjoLazima

#UVIKO3
KAGERA: MTOTO WA SIKU MBILI ATUPWA CHOONI

Jeshi la Polisi linachunguza kumbaini Mama wa Mtoto wa Kiume aliyeokotwa eneo la Lukajage, Kata ya Bugene Wilayani Karagwe ili achukuliwe hatua

Mtoto yupo Hospitali ya Kayanga akiendelea na matibabu

Soma - https://jamii.app/KichangaChooni
SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI

Inakadiriwa katika Watu Bilioni 1 wenye Ulemavu Duniani, asilimia 80 wanaishi kwenye Nchi zinazoendelea. Watu wenye Ulemavu ni miongoni mwa makundi yaliyoathiriwa zaidi na #COVID19

Takriban asilimia 46 ya Wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea wana Ulemavu. Mwanamke 1 kati ya 5 Duniani ana uwezekano wa kupata Ulemavu, na Mtoto 1 kati ya 10 ana Ulemavu.

#JamiiForums #DisabilitiesDay #InternationalDayOfPeopleWithDisability
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA KILIMO CHA BIASHARA

1. Utayari wa kuingia kwenye Kilimo: Maamuzi yako yatokane na uchaguzi wako baada ya kuona Kilimo kitaboresha kipato chako

2. Uchaguzi wa Kilimo kinachokufaa: Chagua kitu ambacho utakuwa tayari kukifanya bila kupata pingamizi la utayari

3. Panga Bajeti kabla ya kuanza Kilimo: Yakupasa ufanye utafiti na kutafuta ushauri wa gharama za Kilimo ulichokichagua

Soma - https://jamii.app/KilimoBiashara
#JFLeo
RAIS SAMIA AKEMEA URASIMU KWENYE KUTOA VIBALI VYA UWEKEZAJI

Asema kuna kasumba ya Kituo Cha Uwekezaji (TIC) kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa nje na kuweka urasimu mwingi kwa wawekezaji wa ndani, hali inayochelewesha Ajira na Kodi ya Serikali

Soma - https://jamii.app/UrasimuTIC
HOJA: VITUO VYA AFYA VILIVYO KARIBU NA MAKAZI YA WATU VIDHIBITIWE

Mshiriki wa #StoriesOfChange amezungumzia utupaji taka holela na uwepo wa matanuri duni ya kuteketeza taka hatarishi, hali anayosema inaleta athari kwa wakazi wa maeneo jirani

Ashauri kuwepo Mwongozo wa kudhibiti taka Pia kuwe na mafunzo ya mara kwa mara kwa Watumishi wa Afya

Soma zaidi - https://jamii.app/VituoVyaAfya
TANZANIA KUPOKEA DOZI 115,200 ZA JOHNSON & JOHNSON KUTOKA UBELGIJI

Chanjo hizo zinatarajiwa kupokelewa Desemba 03, 2021

Ubelgiji iliahidi kusambaza angalau Chanjo Milioni 4 kwa Nchi za kipato cha kati na chini kufikia mwisho wa mwaka 2021

Soma https://jamii.app/JnJ115200

#UVIKO3
Katika ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Mashirika ya Umma, baadhi ya mapungufu yaliyopelekea upotevu wa Tsh. Bilioni 35.96 ni kama;

1) Upotevu wa Tsh. Bilioni 20.17 kutokana na kufutwa kwa madeni ya wakopaji pasipo kuwa na idhini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara ya Fedha na Mipango

2) Upotevu wa makusanyo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 7.23 yaliyokusanywa nje ya mfumo wa malipo ya Serikali GePG na hayakupelekwa Benki

Soma - https://jamii.app/CAGMashirikaUmma

#JFUwajibikaji
KENYA: BABA AMSHTAKI MTOTO AKITAKA AKATWE 20% YA MSHAHARA NA KUPEWA YEYE

Gideon Kisira Cherowo (73) amemfungulia kesi Mtoto wake, Washington Chepkombe akitaka akatwe mshahara ili apewe yeye kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Familia

Cherowo ana Watoto 4 lakini mwenye kazi ni Washington pekee

Soma - https://jamii.app/BabakesiMtoto
TANZANIA YAOMBA KUANDAA KOMBE LA DUNIA

Waziri wa Michezo, Innocent Bashungwa aomba Shirikisho la Soka la Afrika kwa Watu Wenye Ulemavu(FAAF) kuifikiria Tanzania kuandaa Kombe la Dunia

Asema kuna mazingira wezeshi ya kuendesha mashindano makubwa

Soma - https://jamii.app/KombeFAAF