JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AUSTRALIA KUTUNGA SHERIA YA KUONESHA UTAMBULISHO WA WATUMIAJI WA MITANDAO

Imepanga kutunga Sheria hiyo kuiwajibisha Mitandao ya Kijamii kwa maudhui yanayochapishwa na watumiaji

Serikali yasema Uhuru wa kutoa maoni unapaswa kuendana na Uwajibikaji

Soma - https://jamii.app/WasiojulikanaMitandaoni
WHO YAHIMIZA KUTOFUNGIA MATAIFA KWA HOFU YA KIRUSI CHA OMICRON

Shirika la Afya Duniani limesisitiza kufuata Kanuni za Kisayansi za Kimataifa za 2005

Limesema Afrika Kusini na Botswana ni za kupongezwa kwa kuwa na uwazi kuhusu #Omicron

Soma - https://jamii.app/SABotswana
#UVIKO3
Wizara ya Mambo ya nje ya #Morocco imesitisha Safari za Ndege za kuingia Nchini humo kwa muda wa wiki 2 kutokana na aina mpya ya Kirusi cha #Omicron

Asilimia 66 ya Watu wa Taifa hilo tayari wamepokea walau dozi moja ya Chanjo ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/MoroccoFlightsBan
#UVIKO3
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwasababu 55% ya mafuta yanaagizwa kutoka nje

Athari za #COVID19 zimefanya uzalishaji kuwa finyu. Sababu nyingine ya bei kupanda ni gharama za usafirishaji

Soma - https://jamii.app/MafutaKupikia

#JFLeo
Sheria zinazolinda na kuzuia #UkatiliWaKijinsia Mitandaoni ni pamoja na Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni (OCR) 2020 ambayo inakataza kurusha Maudhui ya Udhalilishaji ikiwamo Picha/Video za Utupu

Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni unazidi kukithiri kutokana na Uelewa mdogo wa Watumiaji, Utamaduni wa Jamii kukaa kimya badala ya kukemea pale unapoona Vitendo vya Ukatili

Soma - https://jamii.app/SheriaUkatiliOnline

#16DaysofActivism
HOJA: Mdau wa JamiiForums anasema mahari si zawadi kwani zawadi haipangwi. Anadai Mahari ni kumuuza Mwanamke na ndiyo sababu isipolipwa Mtu hunyimwa Mke

Pia, inaondoa nafasi ya Mwanamke katika Ndoa kwa kumfanya Mwanaume awe na uwezo wa kumnyanyasa kwasababu amemlipia Mahari

Nini maoni yako?

Msome - https://jamii.app/KulipaMahari

#StoriesOfChange
WHO: OMICRON NI TISHIO, CHANJO NI MUHIMU

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Kirusi kipya cha Corona cha #Omicron ni hatari na kuna uwezekano maambukizi duniani kote yakaongezeka

Mataifa yahimizwa kusaidia chanjo Nchi masikini

Soma - https://jamii.app/Omicron

#UVIKO3
CHAD: Serikali ya Kijeshi imetoa msamaha kwa takriban Waasi 300 na Wapinzani kutokana na shinikizo kutoka upinzani

Msamaha unahusisha waliokuwa wamezuiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kutoa maoni, ugaidi na kuhujumu Serikali

Soma - https://jamii.app/PrisonersFreedChad
#Democracy
👍1
KILIMANJARO: Serikali imefungia uzalishaji wa pombe aina ya Simba kutokana na Pombe hiyo kuwa na kiwango kikubwa cha Asidi kisichofaa kwa matumizi ya Binadamu

> Pia, TBS imeagizwa kuchunguza viwanda vinavyozalisha pombe zinazotokana na Ndizi

Soma https://jamii.app/PombeSimba
Ukatili unajitokeza katika sura mbalimbali kama vile vipigo, Ukeketaji, Ubakaji, Mauaji ya Wanawake na Watoto wa Kike, kurithi Wajane, Udhalilishaji wa Wanawake Mitandaoni au kwenye Siasa, na rushwa ya ngono

Ukatili una athari mbaya kwa Wanawake na Watoto wa Kike, kwani huathiri Afya zao Kimwili na Kisaikolojia na hupelekea kudidimiza Maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

#JamiiForums #GenderBasedViolence #16DaysofActivism2021
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
RWANDA: WAZEE WAANZA KUPATIWA DOZI YA TATU YA CHANJO YA CORONA

Walio na umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye maradhi wataanza kupokea dozi kuanzia leo, Novemba 30

Watumishi wa Afya wametajwa katika kundi la kupokea dozi hiyo dhidi ya #COVID19

Soma https://jamii.app/WazeeChanjo
#UVIKO3
TABORA: Wauguzi 2 wa Hospitali ya Kaliua wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu

Mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na Daktari aliye katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa Mimba

Soma - https://jamii.app/NursesFiredSex
#JFLeo
CHANJO ZA COVID-19 ZIMEPITIA HATUA ZA KIUSALAMA

Wataalamu wa Afya wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins wanasema utengenezwaji wa haraka haumaanishi hatua zilirukwa

Teknolojia zimekuwa zikiandaliwa kupambana na milipuko ya Virusi vya kuambukiza

Soma https://jamii.app/ChanjoUsalama

#UVIKO3
CHINA YAIAHIDI AFRIKA DOZI BILIONI 1 ZA CHANJO

Rais Xi Jinping ameahidi kuipa Afrika Dozi Bilioni 1 za Chanjo dhidi ya #COVID19

Katika dozi hizo, Milioni 600 zitatoka #China moja kwa moja na Milioni 400 zitatoka kwa vyanzo vingine

Soma - https://jamii.app/ChinaChanjo

#UVIKO3
Mradi wa Uzalishaji wa Sukari Mbigiri ambao unamilikiwa na Kampuni tanzu ya Mkulazi Wilayani Kilosa ulilenga kuzalisha Sukari tani 50,000 kwa Mwaka

CAG alibaini Kampuni ya Mkulazi kushindwa kusimika mtambo wa kuchakata Sukari kwa wakati kinyume na mkataba wa Mwaka 2018

Pia, Kampuni haikuweza kusimamia Utendaji wa Wakulima wanaouzunguka Mradi kwa kuwapatia ushauri wa Kitaalamu

Soma - https://jamii.app/CAGSukariMbigiri
#JFUwajibikaji
MALEZI: UDHALILISHAJI WA MTOTO KWA NJIA YA MANENO

Udhalilishaji kwa njia ya maneno unatokea pale ambapo Mzazi/Mlezi au Mtu aliye karibu na Mtoto anapotumia maneno yenye kumuumiza Mtoto Kihisia

Baadhi ya maneno ni; Kumkemea au kumkaripia mbele ya hadhara ya Watu au Familia/Ndugu. Kumuita Mtoto majina mabaya (Matusi) na majina mengine ikiwemo majina ya Wanyama

Soma - https://jamii.app/AbuseWordsChild
#Malezi #ChildViolence
Novemba 29, 2021, Taasisi ya WAJIBU ilizindua kitabu kiitwacho "Principles of Public Sector Auditing - The Case of SAI Tanzania" Jijini Dar es Salaam
-
Kitabu hicho kilizinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emanuel Tutuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba
-
Kitabu hicho kimeandikwa na CAG mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU, CPA. Ludovick Utouh.

#JamiiForums #JFUwajibikaji