JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Je, umewahi kujiuliza nini kitatokea endapo utashindwa kutumia Uwezo ulio nao?

1. Utashindwa kufanya maamuzi sahihi juu ya Maisha yako. Mtu asiyeweza kugundua na kuendeleza Uwezo wake huwa ktk hatari ya kukosa mwelekeo

2. Kukosa kutambua Uwezo wako (potential) kutakufanya uwe mtumwa na utatumika kuendeleza kusudi la Mtu mwingine

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema kiwango cha Elimu siyo sababu ya kushindwa kuendeleza Uwezo ulio nao

Soma zaidi - https://jamii.app/TumiaPotential
#StoriesOfChange
Rwanda imesitisha safari zake za Ndege kwenda Afrika Kusini, #Zambia na Zimbabwe pamoja na kurejesha Karantini ya siku 7 kwa wote wanaotoka kwenye Nchi hizo

Wasafiri watatakiwa kukaa Karantini ya saa 24 kwa gharama zao ili kufanyiwa Vipimo

Soma - https://jamii.app/RWBanFlightsSA
#UVIKO3
Kutokana na udhaifu katika mifumo ya ukusanyaji wa mapato, kuna uwezekano mkubwa wa Serikali kupoteza Tsh. Bilioni 265.85 kutokana na vitendo vya Rushwa, Udanganyifu na Ubadhirifu

Katika Serikali Kuu, kumekuwa na ongezeko la upotevu wa mapato kutoka Tsh. Bilioni 7.7 kwa 2018/19 mpaka Tsh. Bilioni 38.7 kwa Mwaka 2019/20

Soma - https://jamii.app/UpotevuFedha
#JFUwajibikaji
AUSTRALIA KUTUNGA SHERIA YA KUONESHA UTAMBULISHO WA WATUMIAJI WA MITANDAO

Imepanga kutunga Sheria hiyo kuiwajibisha Mitandao ya Kijamii kwa maudhui yanayochapishwa na watumiaji

Serikali yasema Uhuru wa kutoa maoni unapaswa kuendana na Uwajibikaji

Soma - https://jamii.app/WasiojulikanaMitandaoni
WHO YAHIMIZA KUTOFUNGIA MATAIFA KWA HOFU YA KIRUSI CHA OMICRON

Shirika la Afya Duniani limesisitiza kufuata Kanuni za Kisayansi za Kimataifa za 2005

Limesema Afrika Kusini na Botswana ni za kupongezwa kwa kuwa na uwazi kuhusu #Omicron

Soma - https://jamii.app/SABotswana
#UVIKO3
Wizara ya Mambo ya nje ya #Morocco imesitisha Safari za Ndege za kuingia Nchini humo kwa muda wa wiki 2 kutokana na aina mpya ya Kirusi cha #Omicron

Asilimia 66 ya Watu wa Taifa hilo tayari wamepokea walau dozi moja ya Chanjo ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/MoroccoFlightsBan
#UVIKO3
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema bei za mafuta ya kupikia zimepanda kwasababu 55% ya mafuta yanaagizwa kutoka nje

Athari za #COVID19 zimefanya uzalishaji kuwa finyu. Sababu nyingine ya bei kupanda ni gharama za usafirishaji

Soma - https://jamii.app/MafutaKupikia

#JFLeo
Sheria zinazolinda na kuzuia #UkatiliWaKijinsia Mitandaoni ni pamoja na Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni (OCR) 2020 ambayo inakataza kurusha Maudhui ya Udhalilishaji ikiwamo Picha/Video za Utupu

Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni unazidi kukithiri kutokana na Uelewa mdogo wa Watumiaji, Utamaduni wa Jamii kukaa kimya badala ya kukemea pale unapoona Vitendo vya Ukatili

Soma - https://jamii.app/SheriaUkatiliOnline

#16DaysofActivism
HOJA: Mdau wa JamiiForums anasema mahari si zawadi kwani zawadi haipangwi. Anadai Mahari ni kumuuza Mwanamke na ndiyo sababu isipolipwa Mtu hunyimwa Mke

Pia, inaondoa nafasi ya Mwanamke katika Ndoa kwa kumfanya Mwanaume awe na uwezo wa kumnyanyasa kwasababu amemlipia Mahari

Nini maoni yako?

Msome - https://jamii.app/KulipaMahari

#StoriesOfChange
WHO: OMICRON NI TISHIO, CHANJO NI MUHIMU

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Kirusi kipya cha Corona cha #Omicron ni hatari na kuna uwezekano maambukizi duniani kote yakaongezeka

Mataifa yahimizwa kusaidia chanjo Nchi masikini

Soma - https://jamii.app/Omicron

#UVIKO3
CHAD: Serikali ya Kijeshi imetoa msamaha kwa takriban Waasi 300 na Wapinzani kutokana na shinikizo kutoka upinzani

Msamaha unahusisha waliokuwa wamezuiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kutoa maoni, ugaidi na kuhujumu Serikali

Soma - https://jamii.app/PrisonersFreedChad
#Democracy
👍1
KILIMANJARO: Serikali imefungia uzalishaji wa pombe aina ya Simba kutokana na Pombe hiyo kuwa na kiwango kikubwa cha Asidi kisichofaa kwa matumizi ya Binadamu

> Pia, TBS imeagizwa kuchunguza viwanda vinavyozalisha pombe zinazotokana na Ndizi

Soma https://jamii.app/PombeSimba
Ukatili unajitokeza katika sura mbalimbali kama vile vipigo, Ukeketaji, Ubakaji, Mauaji ya Wanawake na Watoto wa Kike, kurithi Wajane, Udhalilishaji wa Wanawake Mitandaoni au kwenye Siasa, na rushwa ya ngono

Ukatili una athari mbaya kwa Wanawake na Watoto wa Kike, kwani huathiri Afya zao Kimwili na Kisaikolojia na hupelekea kudidimiza Maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

#JamiiForums #GenderBasedViolence #16DaysofActivism2021
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
RWANDA: WAZEE WAANZA KUPATIWA DOZI YA TATU YA CHANJO YA CORONA

Walio na umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye maradhi wataanza kupokea dozi kuanzia leo, Novemba 30

Watumishi wa Afya wametajwa katika kundi la kupokea dozi hiyo dhidi ya #COVID19

Soma https://jamii.app/WazeeChanjo
#UVIKO3
TABORA: Wauguzi 2 wa Hospitali ya Kaliua wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu

Mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na Daktari aliye katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa Mimba

Soma - https://jamii.app/NursesFiredSex
#JFLeo
CHANJO ZA COVID-19 ZIMEPITIA HATUA ZA KIUSALAMA

Wataalamu wa Afya wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins wanasema utengenezwaji wa haraka haumaanishi hatua zilirukwa

Teknolojia zimekuwa zikiandaliwa kupambana na milipuko ya Virusi vya kuambukiza

Soma https://jamii.app/ChanjoUsalama

#UVIKO3
CHINA YAIAHIDI AFRIKA DOZI BILIONI 1 ZA CHANJO

Rais Xi Jinping ameahidi kuipa Afrika Dozi Bilioni 1 za Chanjo dhidi ya #COVID19

Katika dozi hizo, Milioni 600 zitatoka #China moja kwa moja na Milioni 400 zitatoka kwa vyanzo vingine

Soma - https://jamii.app/ChinaChanjo

#UVIKO3