JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ripoti ya Uwajibikaji ya WAJIBU 2019/20 imeeleza kuwa, upungufu wa Watumishi unaathiri Utendaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kusababisha utoaji duni wa Huduma za Msingi kama Elimu, Afya na Maji salama

Kutowasilisha makato ya kisheria ya mishahara ya Watumishi katika Taasisi husika huwasababishia usumbufu usio wa lazima unapofika wakati wa kustaafu

Soma - https://jamii.app/MikopoMishahara

#JFUwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Milipuko miwili imeripotiwa katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Kampala. Kuna taarifa za kuwepo majeruhi

Inaripotiwa, Maafisa wa Usalama wameamuru kila mtu kuondolewa Bungeni baada ya mlipuko mojawapo kuripotiwa karibu na eneo la Bunge

Soma - https://jamii.app/UGExplosions
#SUDAN: Idadi ya waliouawa tangu Jeshi kuchukua Madaraka imefikia Watu 23 huku Raia wakiendelea kuandamana kuupinga Utawala wa Kijeshi

Zaidi ya majeruhi 200 wamerekodiwa hadi sasa, wakiwemo 10 waliojeruhiwa kwa risasi za Moto

Soma - https://jamii.app/DeathTollsSudan

#HumanRights #JFLeo
DAR: Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake 3 imeahirishwa hadi Novemba 17, 2021

Jaji Joachim Tiganga ameshindwa kutoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na upande wa Utetezi kutokana na wingi wa Hoja

Soma - https://jamii.app/MboweKesiJaji
VIASHIRIA VYA RUSHWA, UDANGANYIFU NA UBADHIRIFU

Taasisi ya WAJIBU imeainisha kiasi ambacho hakikukusanywa au kimetumika na Serikali pasipo kupata tija kimeongezeka kutoka Tsh. bilioni 232.52 Mwaka 2018/19 hadi Tsh. bilioni 1,770.84 Mwaka 2019/20

Mamlaka za Serikali za Mitaa ndizo zimekuwa na ongezeko kubwa zaidi kutoka Tsh. bilioni 103.93 Mwaka 2018/19 hadi Tsh. bilioni 863.85 Mwaka 2019/20 ambapo kasoro nyingi zilionekana eneo la ununuzi wa Umma na usimamizi wa mikataba

Soma - https://jamii.app/UbadhirifuRushwa
#JFUwajibikaji
UPDATE: Polisi Nchini Uganda wamesema Milipuko iliyotokea #Kampala ilitekelezwa na watu 3 waliojitoa mhanga, na walifariki papo hapo

Raia 3 wamefariki dunia na 33 wamejeruhiwa, ikielezwa idadi ya Vifo inaweza kuwa kubwa kuliko inayoripotiwa

Soma - https://jamii.app/KampalaExplosions
KUCHANJA CHANJO YA COVID-19 HUCHUKUA MUDA MFUPI

Wataalamu wa #Afya wanashauri kuwa ni vema kila mmoja kutafuta muda katika ratiba yake ili kupata Chanjo ya #COVID19

Mara nyingi mchakato huo si marefu na hukamilika ndani ya dakika 20

Soma - https://jamii.app/ChanjoMuda

#UVIKO3
DONDOO ZA KIUSALAMA UNAPOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII

1. Rekebisha faragha ya akaunti yako: (Personalize your privacy settings). Pangilia kwa kuchagua nani awe na uwezo wa kuangalia taarifa zako

2. Kabla ya kuweka (post) kitu chochote jiulize endapo kuna ulazima wa kuweka maudhui hayo na Watu watachukuliaje. Maudhui kuhusu masuala yako binafsi yanaweza kuwa mwanya kwa wahalifu

Soma - https://jamii.app/SafetySME

#DigitalSafety
HOJA: KUMCHAPA MTOTO HUMSAIDIA KUBADILIKA?

Kupitia Shindano la #StoriesOfChange, Mdau wa JF anahoji, je tulishachukua muda kujiuliza viboko Watoto wetu vinawasaidia?

Anasema imekuwa kawaida Mtoto kuchapwa anapokosea kidogo tu, lakini athari zake ni kubwa kulinganisha na faida

Nini maoni yako kuhusu hoja hii?

Soma - https://jamii.app/HojaViboko

#Malezi
Taarifa binafsi ni taarifa yoyote inayokutambulisha, iwe inahusiana na Maisha yako binafsi, Kitaaluma, au ya umma (Mfano: Majina, Namba za Simu, Anwani n.k)

Ni mara ngapi umeshakutana na taarifa za Watu wengine katika Mazingira ambayo hukupaswa kukutana nazo? Kama ni mara nyingi, basi huenda hata taarifa zako zinazagaa bila wewe kujua

Ungana nasi katika Mjadala wa Haki ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi kupitia Clubhouse ya JamiiForums Novemba 18, 2021

#JamiiForums #dataprivacy
DKT. ELISHA OSATI: CHANJO ZA COVID-19 HAZISABABISHI DAMU KUGANDA

Tafiti zilizofanyika zimebaini Watu waliokumbwa na shida hiyo walikuwa na matatizo mengine kiafya

Huweza kusababishwa na Shinikizo la Damu, unene kupita kiasi au Kisukari

Soma - https://jamii.app/ChanjoMaswaliMajibu

#UVIKO3
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeyataka Mataifa kuchukua hatua zaidi kudhibiti uraibu wa Tumbaku inayokadiriwa kuua zaidi ya Watu Milioni 8 kila mwaka

Ripoti imebainisha Watu Bilioni 1.3 Ulimwenguni walikuwa wanatumia Tumbaku mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/TumbakuWHO

#JFLeo
👍1
DAR ES SALAAM: Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Wakuu wa Wilaya zote kuchunguza Hospitali, Vituo vya #Afya na Zahanati ili kubaini Watumishi wa Afya wanaowatoza Wajawazito kati ya Tsh. 2,000 hadi 5,000 Fedha za Kadi za Kliniki

Soma - https://jamii.app/KadiKlinikiHela

#JFLeo
Mshiriki wa Shindano la 'Stories Of Change' anasema jambo linaloongeza Ukosefu wa Ajira Nchini ni Mfumo wa utoaji Elimu ambao hulenga zaidi kuwaandaa Wanafunzi kuwa tegemezi

Anasema Mfumo huu umeua vipaji vingi vya Vijana wetu ambavyo vingeweza kuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wengine. Tunahitaji Wanafunzi wafundishwe Elimu halisi ya Maisha ya kujituma na kutambua fursa

Msome - https://jamii.app/UtegemeziElimu
#StoriesOfChange
👍1
ETHIOPIA: Umoja wa Mataifa (UN) umesema takriban watu 1,000 (wengi kutoka Tigray) wanashikiliwa katika Miji mbalimbali Nchini humo tangu Hali ya Dharura ilipotangazwa Novemba 02, 2021

Maelfu ya Watu Nchini humo wanakabiliwa na njaa

Soma - https://jamii.app/EthiopiaUN1K
UGANDA: Rais Yoweri Museveni amesema Magaidi wamejidhihirisha kipindi ambacho miundombinu ya usalama ya Nchini humo imeimarika

Amesema waliojilipua Mjini Kampala ni "Bazzukulu" (inayomaanisha Wajukuu) waliodanganywa na kuchanganyikiwa

Soma https://jamii.app/MuseveniTerrorists
Kila Novemba 17, Siku ya Mtoto Njiti huadhimishwa Duniani ili kuongeza uelewa na kupaza sauti kuhusu changamoto zinazohusiana na suala hilo

Kuzaliwa kabla ya wakati ni pale Mtoto anapozaliwa kabla ya wiki ya 37 ya Ujauzito. Kwa mujibu wa WHO takriban Watoto Milioni 15 wanazaliwa kabla ya wakati kila mwaka

Soma - https://jamii.app/PrematurityDay

#WorldPrematurityDay
Serikali imeshauriwa iendelee kutenga fedha kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madai ya Watumishi na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa Halmashauri zilizoshindwa kupeleka Makato ya Mishahara ya Watumishi katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

> Hii ni kwa mujibu wa Taasisi ya Wajibu ktk uchambuzi wa Ripoti ya CAG 2019/20

Soma - https://jamii.app/MikopoMishahara
#JFUwajibikaji
CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MTOTO NJITI

Mtoto njiti anaweza kuwa na changamoto ya kupumua hivyo punde tu baada ya kuzaliwa, anatakiwa kupatiwa huduma ya kwanza

Hawezi kuhimili baridi hivyo lazima azaliwe kwenye chumba chenye joto la kutosha

Wana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwasababu kinga yao ya mwili haijakomaa

Soma - https://jamii.app/WatotoNjiti

#WorldPrematurityDay