JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#AUSTRIA: WASIOPATA CHANJO WAWEKWA 'LOCKDOWN' KUDHIBITI MAAMBUKIZI

Kansela asema Serikali haijachukua hatua hiyo kwa wepesi, lakini ni ambayo inahitajika

Wasiochanjwa wataruhusiwa kutoka nyumbani kwa sababu kadhaa ikiwemo kununua chakula

Soma - https://jamii.app/AustriaLockdown

#UVIKO3
ARUSHA: Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Sekondari Suye, Evance Florian (17) ameuawa kwa kipigo huku chanzo ni Deni la Tsh. 3,000

Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi, Ibrahim Shaban (18) kwa madai ya kuhusika

Soma - https://jamii.app/KifoDeniBuku3

#HumanRights
UCHAKAVU NA UCHAFU KATIKA MASOKO YA CHAKULA

Katika ukaguzi, CAG alibaini kuwepo kwa idadi kubwa ya Wafanyabiashara ktk Masoko zaidi ya uwezo wa Masoko hayo ambapo hali hii husababisha uzalishaji mkubwa wa takataka na uchakavu wa Miundombinu

Pia, kulikuwa na udhaifu ktk Usimamizi wa uendeshaji wa masoko ambapo kati ya Halmashauri 10 zilizokaguliwa, Halmashauri 5 hazikuwa na #Sheria ndogondogo za usimamizi wa usafi wa Masoko.

Soma - https://jamii.app/UchafuMasoko

#JFUwajibikaji
CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO WAFANYABIASHARA WA TANZANIA

Mdau wa Shindano la 'Stories Of Change' anasema Sekta ya #Biashara Nchini inakabiliwa na changamoto ambazo zinazorotesha Utendaji na Ufanisi

Anasema tunahitaji kuwa na Kodi ya Mashamba makubwa ya Mazao ya Biashara. Pia, kuondoa riba ama kupunguza kwa asilimia kubwa ili Mwananchi akomboke

Msome - https://jamii.app/ChangamotoBiasharaTZ
#StoriesOfChange
DAR: Mahakama imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Mawakili wa Utetezi katika Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake 3

Jaji Joachim Tiganga amekubaliana na hoja za upande wa Mashtaka, na kukubali barua iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama itolewe kama kielezo na Shahidi namba mbili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi

Soma - https://jamii.app/PingamiziMbowe
DAR: Rais Samia Suluhu amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na tatizo jipya la Usalama (Ugaidi)

Asema, "Mapambano dhidi ya tishio la Ugaidi si suala la Vyombo vya Ulinzi na Usalama peke yenu, bali linahitaji ushirikiano wa Taasisi mbalimbali"

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaLugalo

#JFLeo
MAPUNGUFU KATIKA ULIPAJI MISHAHARA NA MIKOPO

Ripoti ya CAG 2019/20 imeonesha mapungufu kadhaa ikiwemo;

Mamlaka za Serikali za Mitaa 36 kushindwa kulipa madai mbalimbali ya Watumishi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 27.84

Pia, Mamlaka za Serikali za Mitaa 46 kushindwa kuwasilisha makato ya kisheria ya mishahara yenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.08 kwenye Taasisi husika

Soma https://jamii.app/MikopoMishahara

#JFUwajibikaji
WHO: CHANJO ZA COVID-19 HAZINA VIAMBATA HATARI NA SUMU

WHO imesema viambata vya chanjo kwa kawaida ni sawa na vile vinavyopatikana mwilini

Chanjo hupitia majaribio ya kisayansi na michakato ya uidhinishaji kuhakikisha zina ufanisi

Soma - https://jamii.app/ViambataHatari

#UVIKO3
INDIA: HEWA CHAFU YAPELEKEA MAHAKAMA KUAMURU OFISI ZIFUNGWE

Mahakama ya Juu imeelekeza Mamlaka kufunga Ofisi New Delhi na Miji ya karibu

Hii itaruhusu Mamilioni kufanyia kazi nyumbani wakati Maafisa wakitafuta mbinu za kupunguza hewa chafu

Soma - https://jamii.app/PollutionIndia
#SOMALIA: WANAJESHI WA UGANDA WAHUKUMIWA KWA KUUA RAIA

Wanajeshi 5 wa #Uganda wanaofanya Kazi na Vikosi vya AU Nchini Somalia wamekutwa na hatia ya kuwaua raia 7

Wawili wamehukumiwa kifo, watatu kifungo cha miaka 39 kila mmoja

Soma - https://jamii.app/JeshiUgandaKifo

#HumanRights #JFLeo
MDAU: MASOMO YA BIASHARA YAENDANE NA MAZINGIRA YA KITANZANIA

Mshiriki wa Shindano la Stories Of Change anasema bado tunafundishwa jinsi ya kutunza na kuhesabu Fedha lakini Dunia ya leo imebadilika

Anasema Serikali inakubali Teknolojia inazidi kukua lakini bado imeshindwa kufumua Mfumo uliopo ili kuendana na Soko la Ajira

Soma Makala yake - https://jamii.app/MasomoBiashara

#StoriesOfChange
SERIKALI YA MAREKANI KUTOA TSH. BILIONI 437 KWA SEKTA YA AFYA

Waziri Dorothy Gwajima amesema, "Serikali ya Marekani inatarajia kutoa fedha hizo kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia mwaka kesho na zitatumika kuboresha utoaji Huduma za Afya"

Soma - https://jamii.app/MarekaniAfyaTZ
WAZIRI LUKUVI: MARUFUKU MADALALI KULAZIMISHA KULIPWA POSHO YA MWEZI 1

Asema "Baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

Soma https://jamii.app/DalaliPosho1
MISRI: Marufuku ya Wafanyakazi wa Sekta ya Umma kuingia Ofisini ikiwa hawajachanjwa na kupimwa #COVID19 imeanza kutekelezwa

Zaidi ya watu Milioni 14 Nchini humo wamepata Dozi 2. Serikali inalenga kuchanja 40% ya Raia kufikia mwisho wa mwaka

Soma - https://jamii.app/MarufukuMisri

#UVIKO3 #JFLeo
Wizara ya Mambo ya Ndani imesema itazifutia leseni Jumuiya na Taasisi ambazo zitashindwa kuwasilisha Vyeti, Katiba na Kanuni za Uendeshaji kwa Msajili ndani ya Siku 15

Mikoa ya Mbeya na Songwe yatajwa vinara wa Jumuiya nyingi ambazo hazijasajiliwa

Soma - https://jamii.app/JumuiyaMsajili15
DRC: Mahakama ya Katiba imesema haina uwezo wa kumhukumu aliyekuwa Waziri Mkuu, Seneta Augustin Matata Ponyo anayeshutumiwa kwa Ubadhirifu wa Fedha za ujenzi wa Bustani ya Kilimo

Serikali imetakiwa kutafuta Mahakama itakayopewa Mamlaka ya kuhukumu

Soma - https://jamii.app/PonyoFailedCase
Ripoti ya Uwajibikaji ya WAJIBU 2019/20 imeeleza kuwa, upungufu wa Watumishi unaathiri Utendaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kusababisha utoaji duni wa Huduma za Msingi kama Elimu, Afya na Maji salama

Kutowasilisha makato ya kisheria ya mishahara ya Watumishi katika Taasisi husika huwasababishia usumbufu usio wa lazima unapofika wakati wa kustaafu

Soma - https://jamii.app/MikopoMishahara

#JFUwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UGANDA: Milipuko miwili imeripotiwa katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Kampala. Kuna taarifa za kuwepo majeruhi

Inaripotiwa, Maafisa wa Usalama wameamuru kila mtu kuondolewa Bungeni baada ya mlipuko mojawapo kuripotiwa karibu na eneo la Bunge

Soma - https://jamii.app/UGExplosions
#SUDAN: Idadi ya waliouawa tangu Jeshi kuchukua Madaraka imefikia Watu 23 huku Raia wakiendelea kuandamana kuupinga Utawala wa Kijeshi

Zaidi ya majeruhi 200 wamerekodiwa hadi sasa, wakiwemo 10 waliojeruhiwa kwa risasi za Moto

Soma - https://jamii.app/DeathTollsSudan

#HumanRights #JFLeo
DAR: Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake 3 imeahirishwa hadi Novemba 17, 2021

Jaji Joachim Tiganga ameshindwa kutoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na upande wa Utetezi kutokana na wingi wa Hoja

Soma - https://jamii.app/MboweKesiJaji