JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Yanayojiri katika Mjadala unaoendelea hivi sasa kupitia Clubhouse

Ungana nasi - https://www.clubhouse.com/room/PG4vRR0p

#JFUwajibikaji
Baadhi ya yaliyozungumzwa katika Mjadala wa "Nini kifanyike ili Nchi ipate tija stahiki kutokana na Misaada inayotoka nje ya nchi?" uliofanyika kupitia Clubhouse

#JFUwajibikaji #WAJIBU #JamiiForums
Mapungufu yaliyobainishwa katika utekelezaji wa Miradi kwa utaratibu wa 'Force Account' yamepelekea kuwepo kwa viashiria vya rushwa na udanganyifu katika mchakato wa ununuzi wa Umma

Pia, Kuwepo kwa upotevu wa Fedha za Umma na kukosekana kwa thamani ya fedha katika miradi iliyotekelezwa. Mfano; Majengo kupata nyufa muda mfupi baada ya kukamilika

Soma - https://jamii.app/AthariForceAcc
#JFUwajibikaji
ZANZIBAR: Waziri wa Nchi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrick Soraga amesema watakutana na Wadau ili kujua kama kuna haja ya kutumia Fedha za Mtandao (Cryptocurrency) kwenye miamala

> Wadau hao ni Wizara ya Fedha, Benki Kuu pamoja na Benki nyinginezo

Soma https://jamii.app/CryptocurrencyZnz
👍1
CHANJO ZENYE 'VIRUSI HAI' HAZISABABISHI CORONA

Kituo cha CDC kimesema chanjo zenye 'Virusi Hai' hazisababishi mtu kupata #COVID19

Chanjo hizi hutumia virusi visivyo na madhara kuchochea mfumo wa kinga kupambana na unachodhani ni maambukizi

Soma https://jamii.app/LiveVaccine
#UVIKO3
MICHEZO: Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo itavaana na DR Congo katika Mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia hatua ya Makundi. Katika Mchezo wa awali, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao moja kwa moja Nchini Congo

Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Saa 10 jioni. Taifa Stars inaongoza Kundi J ikiwa na point saba katika michuano hiyo ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022

#JamiiForums #Sports #Michezo
JINSI YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (UTI)

Kunywa Maji mengi kila Siku na kila baada ya haja kubwa ni vizuri kujisafisha kwa kutokea mbele kurudi nyuma

Hakikisha sehemu za siri zipo safi kabla ya kujamiana. Pia, ni vizuri kupata haja ndogo mara baada ya kujamiana

Hakikisha sehemu za Siri zipo kavu, pendelea kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba, zenye kuacha nafasi (loose-fitting)

Soma - https://jamii.app/KingaUTI
#Afya
Utoaji wa Chanjo ya #COVID19 umekuwa ukihamasishwa kona zote za Dunia huku baadhi ya Nchi zikichukua hatua za kuweka Vikwazo kwa Watu ambao hawajapata Chanjo kurudi Maofisini, kusafiri au kushiriki shughuli za kijamii

Wasiochanja wana sababu mbalimbali ambazo zinawapelekea kusitasita katika kufanya Maamuzi.

Ungana na Jamii Forums katika Mjadala na wasiochanja utakaofanyika Ijumaa, Novemba 12, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #UVIKO3
Ripoti ya Wajibu inasema tangu lilipoanza zoezi la utolewaji wa Vitambulisho vya Taifa Mwaka 2012/13, ni Wananchi 5,621,350 tu ndio waliopata Vitambulisho kati ya 21,692,122 walioandikishwa NIDA hadi kufikia Juni, 2020

Mwaka 2016/17 Serikali iliagiza Vitambulisho vya Taifa viwe na Sahihi ya mwenye Kitambulisho, hatua ambayo ilipelekea uwezo wa Mashine katika uzalishaji kushuka kutoka Vitambulisho 3,168,000 hadi 1,584,000 kwa Mwaka

Soma - https://jamii.app/UdhaifuNIDA
#JFUwajibikaji
DAR: Polisi Kanda Maalum wanamshikilia Mtu mmoja mwenye miaka 16 ambaye jina lake linahifadhiwa kwa tuhuma za kumlawiti Mtoto wa miaka 4 mpaka kumsababishia Kifo

Tukio hilo limetokea Novemba 10, 2021 maeneo ya Chamazi Mbande, Temeke

Soma - https://jamii.app/UlawitiMtt4
#UkatiliWatoto
STEVEN GERRARD ATANGAZWA KUWA KOCHA WA ASTON VILLA

- Klabu ya Aston Villa ya England imemtangaza Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard kuwa Kocha wake mpya

- Gerrard aliyekuwa akiinoa Klabu ya Rangers ya Scotland, amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu

#Sports
TANZIA: Rais wa Zamani (mzungu wa mwisho kuiongoza Afrika Kusini), FW de Klerk amefariki dunia nyumbani kwake Cape Town alipokuwa akijiuguza Saratani ya Mesothelioma

> Alikuwa Mkuu wa Afrika Kusini kuanzia Septemba 1989 hadi Mei 1994

Soma https://jamii.app/RaisAfrikaKusini
MWANZA: Mwanafunzi wa Darasa la Nne, Ntogoso Gunya (12) amefariki Dunia baada ya kuliwa na Mamba wakati akioga Kando ya Ziwa Victoria

Tukio hilo limetokea Novemba 10, 2021 saa 11 jioni ambapo juhudi za kuutafuta Mwili zimepata Kichwa pekee

Soma - https://jamii.app/KifoMwnfzMamba
#JFLeo
STARS YACHEZEA 3-0 KWA MKAPA

- #TaifaStars imejikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa goli 3-0 na DR Congo kwenye mchezo wa kufuzu #WC2022

- DR Congo inaongoza Kundi J ikiwa na alama 8. Benin ni ya 2 ikiwa na alama 7 na mchezo 1 mkononi. Stars ni ya 3 ikiwa na alama 7

#JFSports