JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MAHAKAMA YA JUU YAZUIA MAPENDEKEZO YA KUBADILISHA KATIBA

Mahakama imesema mpango wa BBI ni hatua binafsi ya Rais Kenyatta ambaye hana Mamlaka ya Kisheria kuanzisha mchakato wa mabadiliko yoyote ya #Katiba

Mpango huo unapendekeza mgawanyo wa Madaraka baina ya Makabila hasimu ili kuzuia ghasia zinazotokea kila baada ya Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/CourtBBIKE
TAFITI: #COVID19 INAWEZA KUPELEKEA UHANITHI

Watafiti wameandika ktk Jarida la Afya ya Wanaume kuwa Corona huathiri mishipa ya Damu hivyo huweza kupelekea uhanithi

> Wameona haja ya Wanaume kuangaliwa zaidi katika Chanjo ili kuepuka tatizo hilo

Soma https://jamii.app/UhanithCorona
MAREKANI: KAMPUNI YA MAFUTA YADAIWA KULIPA DOLA MILIONI 5 KWA WADUKUZI

Usafirishaji wa Mafuta ktk Bomba la Colonial Pipeline, linalobeba zaidi ya galoni Milioni 100 ulisitishwa Mei 7 kwasababu ya shambulio la Kimtandao ila shughuli zilirejea Mei 13

Soma https://jamii.app/ColonialPipelineBack
CHINA YAFANIKIWA KUPELEKA KIFAA KATIKA SAYARI YA 'MARS'

China imekuwa nchi ya pili ktk historia kufanikiwa kufikisha kifaa ktk Sayari Nyekundu au 'Mars' kwa Kiswahili inaitwa 'Mirihi'

Kifaa hicho kimetua, Mei 15, 2021 Asubuhi kitatafiti uwepo wa maisha kwa miezi 3

Soma https://jamii.app/MarsChina
KINONDONI: WALIMU 1,333 KUPANDISHWA VYEO

> Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kinondoni ipo hatua za mwisho za kukamilisha zoezi la kupandisha vyeo/madaraja Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni wenye sifa

Soma https://jamii.app/WalimuVyeo
MAAMBUKIZI YA #COVID19 YARIPOTIWA KUPUNGUA INDIA

Mji wa #Delhi umeshuhudia visa 8,506 vya maambukizi ndani ya saa 24 zilizopita

Katika Mji wa kibiashara wa #Mumbai, maambukizi yameshuka kufikia visa pungufu ya 2,000 kutoka 11,000 kwa siku

Soma - https://jamii.app/FallCoronaIndia
ABOUBAKARI KUNENGE ATEULIWA RC PWANI

Rais Samia Suluhu amemteua Aboubakari Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani

Kabla ya uteuzi Kunenge alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye amestaafu

#JFLeo
RC HAPI NA RC CHALAMILA WAHAMISHWA MIKOA

- Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza

- Aidha, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora

#JFLeo #Uteuzi
DPP MPYA NI SYLVESTER ANTHONY MWAKITALU

Rais Samia Suluhu amemteua Bw. Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka

> Anachukua nafasi ya Biswalo Mganga aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu

#JFLeo #Uteuzi
QUEEN SENDIGA ATEULIWA KUWA RC IRINGA

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Queen Cuthbert Sendiga, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa

> Anachukua nafasi ya Ally Hapi aliyeteuliwa kuwa RC Tabora

#JFLeo
RAIS SAMIA AMTEUA DAVID KAFULILA KUWA RC ARUSHA

- Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. David Zacharia Kafulila kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha. Kafulila anachukua nafasi ya Bw. Idd Hassan Kimanta ambaye amestaafu

#JFLeo #Uteuzi
AMOS MAKALLA AWA RC DAR ES SALAAM

- Rais Samia Suluhu amemteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akichukua nafasi ya Aboubakar Kunenge ambaye amekuwa RC Pwani

- Pia, amemteua Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

#JFLeo
MAKONGORO NYERERE AWA MKUU WA MKOA MANYARA

- Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere ameteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Mkirikiti

- Mkirikiti amepelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

#JFLeo #Uteuzi
RAIS SAMIA AMTEUA ADAM MALIMA KUWA RC WA TANGA

> Kabla ya Uteuzi huu, Adam Kigoma Malima alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

> Pia, amemteua Bi. Rosemary Staki Senyamule kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita

#JFLeo #Uteuzi
SALUM HAMDUNI AWA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

> Hamduni aliyepandishwa cheo na Rais Samia Suluhu kutoka ACP hadi Kamishna wa Polisi (CP) amechukua nafasi ya Brig. Jen. Mbungo atakayepangiwa majukumu mengine

#JFLeo #Uteuzi
RAIS SAMIA AMTEUA STEPHEN KAGAIGAI KUWA RC KILIMANJARO

- Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanzania, Stephen Kagaigai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Anna Mghwira aliyestaafu

#JFLeo #Uteuzi
GAGUTI RC MPYA MTWARA, BYAKANWA KUPANGIWA MAJUKUMU MENGINE

- Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Gelasius Gasper Byakanwa atapangiwa majukumu mengine

#JFLeo #Uteuzi
RUVUMA: WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA WATUHUMIWA KUJIMILIKISHA MADUKA YA KITUO KIKUU CHA MABASI

> Wananchi wamelalamika kwa DC Pololet Mgema kuwa, Watumishi wamejimilikisha maduka na hawayatumii kwa nia ya kuwapatia wafanyabiashara kwa bei kubwa

Soma https://jamii.app/MadukaSongea
YANGA NA NAMUNGO ZATOKA SULUHU

Namungo ya Lindi imetoka suluhu na Yanga SC kwa kutofungana katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

> Mchezo ulichezwa Uwanja wa Majaliwa ulio mkoani Lindi

#JamiiForums #JFMichezo