JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AUSTRALIA YAPIGA MARUFUKU RAIA WANAOTOKEA INDIA KUREJEA NCHINI HUMO

- Ni sehemu ya Kanuni zinazolenga kuzuia wasafiri wakati India inapambana na #COVID19

- Ni mara ya kwanza kwa Australia kufanya kitendo cha Raia kurejea nyumbani kuwa kosa la jinai

Soma https://jamii.app/AusBanIndia
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA KUKABILIANA NA KAGERA SUGAR

- Klabu ya Simba ambayo ni bingwa mtetezi wa kombe itakutana na Kagera Sugar majira ya saa 1:00 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mchezo mwingine unaoendelea ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya KMC Fc

- Washindi wa #Michezo ya leo wataungana na Yanga na Mwadui ambazo zimetinga robo fainali ya michuano baada ya Yanga kuifunga Tz Prisons 1-0 na Mwadui kuiadhibu Coastal union goli 2-0

#JamiiForums #Sports
HUAWEI YAJIPANGA KUWA NA KASI YA 6G JULAI 2021

> Wakati Afrika inapambana na teknolojia ya 3G. Kampuni ya Teknolojia ya Huawei inajaribu kwa mara ya pili teknolojia ya 6G

> 6G inatarajiwa kuwa na kasi mara 100 ya kasi ya 5G

Soma https://jamii.app/Huawei6G
#JFTeknolojia
JE, FILAMU ZAKO PENDWA ZA KIVITA NI ZIPI?

> Ziko filamu nyingi za kivita zilizokonga nyoyo za watazamaji kiasi cha Watu kujivisha uhusika wa filamu. Mfano kufunga usongo kama Rambo ili kupigana

> Je, unazikumbuka filamu gani za kivita zilizokukosha?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/FilamuZaKivita
KOMBE LA SHIRIKISHO: SIMBA NA DODOMA JIJI ZATINGA ROBO FAINALI

- Michezo ya hatua 16 bora imemaliza kwa timu za Simba SC na Dodoma Jiji kusonga mbele katika hatua ya robo fainali

- Simba imeibuka kidedea kwa kuifunga Kagera Sugar goli 2-1 huku Dodoma Jiji ikiifunga KMC FC goli 2-0

- Simba na Dodoma Jiji zinaungana na Yanga SC na Mwadui FC katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo

#JamiiForums #JFSports
SOMALIA: BUNGE LAPIGA KURA KUMFUTIA RAIS NYONGEZA YA MUDA

- Ni baada ya hatua hiyo iliyoidhinishwa mwezi Aprili kuibua mvutano mkubwa

- Kuna wasiwasi waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama Nchini humo

Soma > https://jamii.app/BungeSomalia
WADAU WALALAMIKIA HALI YA STENDI YA KAGERA

> Mdau wa JamiiForums ameandika kuwa Stendi Kuu ya Mkoa wa Kagera haiko ktk hali nzuri mbali na kutumiwa na wageni wa nchi jirani

> Mdau amedai bajeti ya Wizara ya OR-TAMISEMI haijaongelea Stendi hiyo

Soma https://jamii.app/StendiKagera
SAMSUNG YAIPIKU APPLE KWENYE MAUZO YA SIMU ROBO YA KWANZA YA MWAKA

- Kampuni hiyo imeteka soko kwa 22%, ikiuza takriban simu Milioni 76.5 ikilinganishwa na Apple iliyouza simu Milioni 52.4 na kuambulia 15% tu ya soko kuanzia Januari hadi Machi 2021

Soma https://jamii.app/SamsungVsApple
MNYIKA: TULIJUA NYALANDU NA SELEMAN WANGEHAMA

> Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema walifahamu Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew wangeondoka kutokana na mienendo waliyokuwa wakiionesha kwa hivi karibuni

Soma https://jamii.app/MnyikaWasaliti
#JFLeo #JamiiForums
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI KENYA

> Rais wa #Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini #Kenya

> Anatarajia kufanya ziara hiyo kuanzia Mei 4, 2021 ambapo atapokelewa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Soma https://jamii.app/ZiaraKenya
INTER MILAN YAWA BINGWA WA β€˜SERIE A’

- Inter chini ya Kocha Antonio Conte imekuwa Bingwa baada ya Sassuolo kutoka sare ya goli 1-1 na Atalanta iliyo nafasi ya 2

- Ushindi huu tangu ishinde taji hilo 2009/10 umemaliza utawala wa miaka 9 wa Juventus kushinda taji hilo

#JFSports
MECHI YA MANCHESTER UNITED DHIDI YA LIVERPOOL YAAHIRISHWA

- Ni baada ya mashabiki takriban 200 wa Man. Utd kuvamia Old Trafford kupinga Umiliki wa familia ya Glazer katika Klabu hiyo

- Man. Utd imesema EPL itapanga upya tarehe ya mchuano huo muhimu kwa Ligi Kuu

#JFSports
TUANZE WIKI KWA ARI YA KAZI

> Habari yako Mdau wa JamiiForums. Tunakutakia kila la kheri kwenye kazi zote njema utakazozifanya wiki hii

> Tunashukuru kwa kuwa nasi na kukusihi kuendelea kutufuatilia ili kupata taarifa na maarifa mbalimbali

#JFLeo
JUKUMU LA KULINDA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SIO LA SERIKALI PEKEE

> Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na Maadhimisho yanafanyika Jijini Arusha

> Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, asisitiza kuweka maslahi ya Taifa mbele

Soma - https://jamii.app/FreePress
#MediaRights
NIGERIA YAPIGA MARUFUKU WASAFIRI KUTOKA INDIA, BRAZIL NA UTURUKI

- Watu wenye Hati za Kusafiria zisizo za Nigeria na waliozuru Mataifa yaliotajwa siku 14 kabla ya kwenda #Nigeria, watanyimwa ruhusa ya kuingia kuanzia Mei 4 kutokana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/NigeriaBanIndia
WAZIRI UMMY: NI MARUFUKU SHULE KUWADAI CHETI WANAOANZA DARASA LA KWANZA

- Amesema "Bado hatujafanya vizuri ktk kuongeza 'access' ya Watoto kuanza Elimu ya Awali. Haileti mantiki kusema kila Mtoto aanze Darasa la 1 akiwa na Certificate ya Awali"

Soma > https://jamii.app/ShuleCheti1
LSF: KUPATA TAARIFA NI HAKI YA MSINGI YA KILA MTU

- Mkurugenzi wa Shirika la Legal Services Facility (LSF) Lulu Ng’wanakilala amesema ili kuwa na Jamii yenye maendeleo nyanja zote ni muhimu kuwa na taarifa sahihi zitakazowawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi

- Amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari ambayo kilele chake kinafanyika Arusha

- Ameeleza, "Tunapoadhimisha Siku hii ya #UhuruWaHabari napenda kusisitiza kuwa kupata taarifa ni Haki ya msingi ya kila mtu"

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation
TEF: MWAKABIBI AMEKUWA AKIKAMATA WAANDISHI, TUNAPONGEZA HATUA ZILIZOCHUKULIWA

- Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri Temeke, Lusabilo Mwakabibi amekuwa akikamata waandishi na kuwaweka ndani na wanaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua ya kumsimamisha kupisha uchunguzi

- Amesema Kumekuwa na wimbi la Watendaji wa Serikali na baadhi ya Askari kuwanyang’anya Wanahabari vitendea kazi na kuwashikilia bila sababu za msingi na wanakemea matukio hayo kama Wanahabari

Soma > https://jamii.app/PressFreedomDay

#WPFD #WorldPressFreedomDay #AccessToInformation
- Wabunge hao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Halima Mdee, walifukuzwa uanachama Novemba 27, 2020 baada kwenda Bungeni kuapishwa kuchukua nafasi za viti maalum

- Akizungumza leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Ndugai amewataka Wabunge hao wachape Kazi kwa kuwa wako mikono salama, huku akionya Vyama viache kuwanyanyasa Wanawake