JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA: MIAKA MITANO IJAYO KUNAHITAJIKA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA ZA UZALISHAJI ZINAZOTOA AJIRA KWA WINGI

> Rais Samia amesema Uchumi ulikuwa unakuwa kwa 6.9% lakini #COVID19 imefanya ukue kwa 4.7%. Wataboresha Mazingira ya Uwekezaji ili kuleta ajira

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA: TUTABORESHA ILI MASHIRIKA YA UMMA YAJIENDESHE KWA FAIDA

> Rais Samia amesema Mashirika ya Umma yanajiendesha kwa kusuasua hali inayopelekea Viongozi kuwa na hofu wakati wa kutoa gawio

> Ameahidi kufanya kazi vizuri na Mashirika binafsi

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA AWAONYA WANAOPOTOSHA KUHUSU KIFO CHA RAIS MAGUFULI

> Rais Samia amesema kuna wanaotumia mitandao ya kijami kupotosha kuhusu kifo cha Rais Magufuli kwa kudai kuwa amepewa sumu

> Amesema kama wana ushahidi waupeleke Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA: HATUTAKUBALI KUONA ATCL INAPATA HASARA

> Rais Samia amesema Serikali italilea Shirika la Ndege la ATCL kimkakati ili liweze kujiendesha kwa ufanisi ikiwemo kulipa unafuu wa kodi na kuliondolea madeni

> Pia, Serikali itahakikisha wanaoliendesha ni watu wenye weledi na uwezo

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA AWAAMBIA WABUNGE WAIKOSOE SERIKALI KWA LUGHA YA KIBUNGE

> Rais Samia ameliomba Bunge kuisimamia Serikali katika kutekeleza yaliyoahidiwa na wakosoe kwa staha inapobidi

> Amesema Bunge ni sauti ya Wananchi hategemei lijadili yasiyohusika

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA: TUTATOA KIPAUMBELE KUENDELEZA MAKAO MAKUU YA SERIKALI JIJINI DODOMA

> Katika hatua hii, Rais Samia ameahidi kuendeleza hatua za kuifanya Dodoma kuwa Mji Mkuu na Ofisi za Serikali kuwa zinapatikana huko

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
RAIS SAMIA: ULINZI WA AFYA YAKO UNAANZA NA WEWE MWENYEWE

> Rais Samia amewataka watanzania kuendelea kufauta hatua zote za kujikinga na maambukizi ya #COVID19

> Amesema hadi sasa hakuna dawa iliyogundulika hivyo ni lazima kuchukua tahadhari

Soma https://jamii.app/22HotubaSamia
SHINYANGA: TAKUKURU YASHAURI MACHINJIO YANAYOENDESHWA KIENYEJI KUFUNGIWA

> TAKUKURU wilayani Kahama imebaini nguruwe huchinjwa wakiwa wamekufa na kutokaguliwa na Maafisa Mifugo

> Aidha, nyama zinazozikwa hufukuliwa na kuuzwa

Soma https://jamii.app/NguruweKahama
#JFLeo
#NIGERIA: WATU 50 WAUAWA NA WATU WALIOJIHAMI NA SILAHA

> Watu waliokuwa na pikipiki wameshambulia Vijiji vya Jimbo la Zamfara na kusababisha vifo, wengine hawajulikani walipo

> Baadhi ya walioshambuliwa ni waliosambaratishwa na mashambulio ya awali

Soma https://jamii.app/NigeriaMauaji
TMA: KIMBUNGA JOBO CHAZIDI KUSOGELEA TANZANIA

> Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha kuwa kimbunga cha JOBO kipo umbali wa Kilometa 400 kikizidi kusogea kwa kasi ya Km 20 kwa saa

Soma https://jamii.app/KimbungaLindi
NANI ADUI WA VIJANA KATIKA KUJIAJIRI?

- Ajira zisizo rasmi zimekuwa ni changamoto kwasababu zinatoa riziki ya mkono kwa mdomo tu (hand to mouth) na hivyo kutozingatia mahitaji mengine

- Vijana wengi wenye taaluma mbalimbali wamejikuta Mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato

Je, adui wa vijana ni Uthubutu, Serikali, Malezi au Mazingira?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/VikwazoKujiajiri
TAHADHARI ZA KUCHUKUA KUKABILIANA NA KIMBUNGA JOBO

> Kaa karibu na nyumbani. Ingiza vitu hatarishi ndani ili usidhurike upepo ukivuma

> Vifaa vya umeme viwe na chaji muda wote. Weka vitu muhimu ktk begi iwe rahisi kuhama itakapolazimika

Soma - https://jamii.app/TahadhariJOBO
DAVID KAFULILA: TUTUMIE MITANDAO VIZURI, RAIS ANASOMA MAONI YETU

> Kafulila atoa wito kwa Watanzania kutumia vizuri mitandao ili Rais Samia aweze kuvutiwa kusoma mawazo

> Asema matusi yanaweza kumfanya aache kutumia kama alivyofanya Rais wa Kenya

Soma https://jamii.app/TumieniMitandao
NJOMBE: WATOTO CHINI YA MIAKA 5 WATOZWA TSH.4000 KUMUONA DAKTARI

> Mamlaka za Kituo cha Afya Makambako zimesema Watoto hulipa kumuona Daktari, vipimo na Dawa ni bure

> Pia wajawazito wenye matatizo yasiyohusiana na ujauzito hulipia matibabu yote

Soma https://jamii.app/MalipoWatoto
MSONGO WA MAWAZO WAKATI WA UJAUZITO

- Kiwango cha juu cha Msongo wa Mawazo huweza kusababisha shida za kiafya kama Shinikizo la Damu na Magonjwa ya Moyo. Wakati wa ujauzito, Msongo wa Mawazo unaweza kuongeza nafasi ya kupata Mtoto Njiti au aliye na uzani mdogo

- Sababu za Msongo wa Mawazo kwa Wajawazito ni 'Morning sickness', Uchovu, maumivu ya Mgongo, kubadilika kwa Homoni na wasiwasi juu ya kujifungua au jinsi ya kumtunza Mtoto

Soma https://jamii.app/MawazoHuzuni
#StressAwarenessMonth
👍1