JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#MAREKANI: ALIYEWAHI KUWA MAKAMU WA RAIS AFARIKI DUNIA

> Walter F. Mondale amefariki akiwa na miaka 93. Alikuwa Makamu wa Rais Jimmy Carter kuanzia 1977-1981

> Alishindwa kupata Urais 1984, lakini aliweka rekodi ya kuwa na Mgombea Mwenza Mwanamke

Soma - https://jamii.app/MakamuMarekani
UTAFITI-MAREKANI: MTU 1 KATI YA 4 ANAFIKIRIA KUACHA KAZI BAADA YA #COVID19

- 80% wataacha kazi kwa sababu wana wasiwasi juu ya maendeleo ya taaluma zao

- Wengine Corona imesababisha wajifunze ujuzi na ustadi mpya ili kupata kazi za aina nyingine

Soma - https://jamii.app/JobQuitCorona
WAZIRI UMMY AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA SENGEREMA

- Waziri wa TAMISEMI amemsimamisha kazi Magesa Boniphace kuanzia leo baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za Ubadhirifu wa fedha za Miradi ya Maendeleo kutoka kwa Wananchi na Mbunge wa Jimbo

Soma - https://jamii.app/DEDSengeremaOut
KENYA: WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE WALALA NJE KUTOKANA NA ZUIO LA KUTEMBEA USIKU

> Wanafunzi waliotakiwa kurudi kwao wamelazimika kulala ktk Viwanja vya Uhuru vilivyopo Nairobi

> Muda wa kutotoka nje uliwakuta wakiwa hawajapata usafiri

Soma https://jamii.app/CurfewNairobi
KAJALA NA PAULA WAHOJIWA KUHUSU TUHUMA ZA KUSAMBAZA PICHA ZA UTUPU ZA HARMONIZE

> Kajala Masanja na mwanaye walikamatwa na Polisi Aprili 19 jioni walipowasili nchini wakitokea Dubai na walihojiwa kwa saa kadhaa. Wameachiwa kwa dhamana

Soma https://jamii.app/KajalaPaula
#JFBurudani
MHASIBU WA TPA KIGOMA AKAMATWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

> Madaraka Robert aliyekuwa anatafutwa na TAKUKURU tangu Agosti 2020 amekamatwa Nyasaka Mkoani Mwanza

> Anatuhumiwa kukwepa kodi zaidi ya Tsh. Milioni 153.5

Soma https://jamii.app/MhasibuTPAKigoma

#KemeaRushwa
RAIS WA CHAD AFARIKI BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI WA UCHAGUZI

- Jeshi Nchini #Chad limesema Rais Idriss Deby amefariki Dunia kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiwaongoza Wanajeshi wanaopambana na Waasi Kaskazini mwa Nchi hiyo

Soma - https://jamii.app/RIPIdrissDerby
WASHINGTON, USA: MAHAKAMA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA FAMILIA YA VALAMBHIA DHIDI YA TANZANIA

> Familia ya Valambhia ilitaka kulipwa zaidi ya Tsh. bilioni 149 kwa madai ununuzi wa vifaa vya kijeshi kati ya Kampuni ya TEL na Tanzania miaka ya 1980

Soma https://jamii.app/WashngtonDC
KAPUFI: IDADI YA WATU SIO TATIZO BALI KUWA NA WATU WENGI AMBAO NI TEGEMEZI

- Mbunge wa Mpanda amesema "Idadi ya Wazalishaji ikiwa ndogo tutaishia kutamani kujenga Madarasa mengi, kuongeza madawati na kukimbizana kufanya mambo kwa zimamoto"

Tazama - https://youtu.be/fJ4JksrEedU
#JFLeo
UFUGAJI: SABABU ZA KUKU KUPUNGUZA UTAGAJI WA MAYAI (2)

- Upungufu wa virutubisho muhimu katika chakula cha Kuku wa Mayai husababisha kupungua kwa uzalishaji wa mayai

- Kupukutisha Manyoya: Katika kipindi hiki Kuku hupunguza au kusimamisha utagaji kwasababu hutumia Protini nyingi na nguvu kuotesha manyoya mapya

- Mtiririko wa utagaji wa Mayai kwa Kuku unaweza kuathiriwa na Joto katika mazingira. Kwa kawaida Kuku anahitaji Joto lisiwe chini ya 11°C lisiwe zaidi 28°C

Soma - https://jamii.app/MayaiKukuChini
HOJA: ELIMU YA SASA HAISAIDII KUJIAJIRI WALA HAITOI WAHITIMU WENYE SIFA STAHIKI

- Baadhi ya Wadau wanasema Wahitimu wengi hawana uelewa wa kile walichokisomea kutokana na kukariri, Taasisi zinazozalisha Wahitimu kuwa na hali mbaya, Walimu na Mitaala isiyo bora

- Wengine wanasema Wahitimu wenye hali mbaya wengi wao ni waliosoma kozi ambazo hawakuzipenda au walisoma kwa kufuata mkumbo/ushauri wa Watu fulani

- Je, una mtazamo gani kuhusu hili?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/ElimuKujiajiri
UGANDA: MADAKTARI WATAKA CHANJO YA #COVID19 IWE YA HIARI

- Ni baada ya Viongozi kadhaa wa Wilaya kutaka Watumishi wa Afya wapatiwe Chanjo kilazima

- Umoja wa Madaktari umesema Afya ni suala binafsi na kushauri kampeni za kujenga uelewa zifanyike

Soma https://jamii.app/ChanjoUganda
ZANZIBAR: MCHELE TANI 42.5 WATEKETEZWA, UMEONEKANA HAUFAI KUTUMIWA NA BINADAMU

> Mchele huo uliingizwa toka India, umeteketezwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA)

> ZFDA yasema bidhaa zilizoisha muda hupelekea matatizo ya Saratani

Soma https://jamii.app/McheleZnz
YANGA SC YATAMBULISHA KOCHA MPYA KUTOKA TUNISIA

- Uongozi wa Klabu ya Young Africans umemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Mohamed Nasreddine Nabi pamoja na Kocha Msaidizi, Sghir Hammadi kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu

#JFSports
MDAU ASHAURI NJIA ZA KUTUMIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA

> Mdau ameshauri kuacha matumizi yasiyo ya lazima kama kutoa ofa. Pia kutonunua kitu kama haujapanga

> Muhimu kuwa na Bima ya Afya, maisha nk. Pia penda kununua vitu kwa bei ya jumla

Zaidi, soma https://jamii.app/UgumuWaMaisha
CHAD: JESHI LAVUNJA SERIKALI. MTOTO WA DEBY KUONGOZA KIPINDI CHA MPITO

Kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby, Jeshi litaongoza kwa miezi 18 na Baraza litaongozwa na Mahamat Idriss Deby

> Chad itaomboleza kwa siku 14. Mipaka ya anga na ardhi yafungwa

Soma https://jamii.app/ChadRaisMpito
ZUNGU ATAKA KUWEPO KWA KODI KWENYE MITANDAO YA SIMU

- Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, amependekeza kuwepo kwa kodi ya Uzalendo itakayokatwa kila siku kupitia Mitandao ya Simu kwa kila Mtanzania ili kuwa chanzo kipya cha mapato kwa Serikali

Soma - https://jamii.app/ZunguKodiMitandao
NAMNA YA KUTAMBUA MWENZA WAKO ANA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

- Anakuwa Mtu wa kukasirika sana na kukerwa na kila kitu unachofanya. Pia, anaweza kuwa na huzuni wakati mwingi na hii hupelekea Mawasiliano yenu kuanza kudhoofika

- Hutumia muda mwingi kukamilisha kazi ndogo na huwa mzito katika kufanya maamuzi

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
#StressAwarenessMonth