JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UFUGAJI: SABABU ZA KUKU KUPUNGUZA UTAGAJI WA MAYAI (1)

- Kupungua kwa saa za mwanga: Mwanga husisimua “pituitary gland” kwa Kuku ili kuchochea uzalishaji wa Mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa Mayai huhitaji saa 14 mpaka 16 za mwanga (Jua)

- Msongo wa Mawazo (Stress) na mabadiliko mbalimbali: Ni rahisi kwa Kuku kuathirika na #Stress kwasababu hapendi mabadiliko ikiwemo chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji na kuwahamisha hamisha kila mara

Soma - https://jamii.app/MayaiKukuChini
#JFUfugaji
RAIS SAMIA KULIHUTUBIA BUNGE APRILI 22, 2021

- Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia Bunge la #Tanzania kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi jioni

- Spika Job Ndugai awataka Wabunge wote kuhakikisha wanakuwepo Bungeni wakati huo

Soma - https://jamii.app/SamiaBungeni
MICHEZO: JOSE MOURINHO ATIMULIWA TOTTENHAM HOTSPURS

- Imeripotiwa kuwa Chriss Powell na Ryan Mason wanajiandaa kuifundisha timu hiyo hadi mwisho wa mwezi Juni

- Bodi ya Timu hiyo imeanza mpango wa kupata kocha mpya

Soma > https://jamii.app/MourinhoOut

#Spurs #JamiiForums
JE, NINI KIFANYIKE KUWA NA MIPANGO MIJI MIZURI?

> Mdau wa #JamiiForums anasema hata maeneo mapya katika Miji hujengwa kiholela na kuwa changamoto

> Mbali na kazi nzuri inayofanywa na Wizara, Mdau anahoji njia nzuri za kuwa na Miji iliyopangika

Soma - https://jamii.app/MipangoMiji
DAR: WAZIRI MKUU ATEMBELEA KITUO CHA MAGARI YA MWENDOKASI GEREZANI

> Kassim Majaliwa amebaini mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi kutokana na mgogoro na msambazaji

> Meneja ametakiwa kuongeza magari kwani wakazi wa Kimara hupata shida

Soma https://jamii.app/MabasiYaMwendokasi
SERIKALI KUTOA MAFUNZO YA KUFUNDISHA HISABATI KWA WALIMU

- Serikali itaanza kutoa mafunzo kazini kuanzia Julai Mosi ikiwemo mbinu za ufundishaji

- Prof. Mkumbo asema wamebaini kuna Walimu hawamudu kufundisha baadhi ya mada katika somo hilo

Soma - https://jamii.app/MafunzoHisabati
DAR: MMOJA ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTANGAZAJI WA ITV

- Jeshi la Polisi Kinondoni linamshikilia Mtu mmoja ambaye jina linahifadhiwa kufuatia kifo cha Blandina Sembu ambaye Machi 27, 2021 mwili wake ulikutwa pembezoni mwa barabara

Soma - https://jamii.app/MbaroniKifoBlandina
MALAWI: WAZIRI WA KAZI ATIMULIWA KWA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA COVID19

> Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amewafukuza kazi maafisa wawili na Waziri wa Kazi, Ken Kandodo, kwa ubadhirifu wa Tsh. Bilioni 18 zilizolengwa kupambana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/WaziriMalawi
DR-CONGO YAANZA KUTOA CHANJO YA CORONA

> Taifa hilo limepokea Dozi Milioni 1.7 za Chanjo ya #AstraZeneca na wameanza kutoa kwa hiari kwa raia

> Awali utoaji chanjo hiyo ulisitishwa baada ya mataifa mengine kushuku usalama na ufanisi wake

Soma https://jamii.app/ChanjoDRC
RC CHALAMILA: MNAOMUONGELEA VIBAYA MAGUFULI WAKATI HAYUPO, MNATUCHOSHA AKILI

- Asema kuna Watu wameacha kufanya kazi wanakaa ili kumjadili Hayati Dkt. John Magufuli

- Asema kama wanaongea yenye maana ilifaa wafikishe ujumbe wakati akiwa hai

Soma https://jamii.app/ChalamilaSemaMagu
TIGO NA ZANTEL ZAUZWA KWA KAMPUNI YA MADAGASCAR

> Millicom International inayomiliki Tigo na Zantel, imetia saini ya kuuza biashara zake kwa Kampuni ya Axian Group

> Wateja wamehakikishiwa hakutakuwa na mabadiliko katika utoaji huduma

Soma - https://jamii.app/MilicomYauzaKampuni
RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI DIT, NACTE, COSTECH, DMI, TLSB, TAEC, TAFORI NA BODI YA MAABARA

- Dkt. Richard Masika anakuwa M/kiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia(DIT)

- Prof. Joseph Msambichaka ni M/kiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)

Soma - https://jamii.app/UteuziDIT
KENYA: WATU MILIONI 1.4 WAKABILIWA NA NJAA

> Shirika la Msalaba Mwekundu limebainisha Watoto 400,000 wasio na lishe bora wanahitaji msaada wa dharura

> Hali ya njaa inaweza kusababisha mapigano kugombea rasilimali finyu zilizopo

Soma - https://jamii.app/NjaaaKenya
MDAU ASHAURI WANAUME KUTOKUWA NA BAADHI YA TABIA

> Mdau ameshauri Mwanaume kutotumia maneno kama ‘Xaxa’, 'Jomoni' au kutumia emoji za kuona aibu kwa Mwanaume mwenzako

> Je, ni vitu gani zaidi Mwanaume asifanye kwa Mwanaume mwenzake?

Soma https://jamii.app/TabiaZaKiume
BURUDANI: MUIGIZAJI GANI HUCHOKI KUANGALIA FILAMU ZAKE?

> Muigizaji nyota anaweza kutoa filamu mbovu na isiyofanya vizuri sokoni lakini bado watakuwepo watakaoifurahia

> Je unampenda muigizaji gani ambaye utaangalia filamu yake hata kama ni mbaya?

Soma https://jamii.app/FavoriteActors
URUSI YAMPELEKA ALEXEI HOSPITALI BAADA YA MASHINIKIZO

- Kiongozi Mkuu wa Upinzani Nchini Urusi, Alexei Navalny amepelekwa Hospitali ya Wafungwa siku ya 20 tangu alipogoma kula

- Wafuasi wake wamepanga maandamano siku ya kesho (Aprili 21)

Soma - https://jamii.app/AlexeiHospital
TANGA: WALIMU WANNE WANAISHI NYUMBA MOJA KUTOKANA NA NYUMBA KUEZULIWA NA UPEPO

> Shule ya Msingi Mandera iliyopo Mswaha, Wilayani Korogwe ina uchakavu mkubwa Vyumba vya Madarasa na Nyumba za Walimu hali inayowatia hofu walimu

Soma https://jamii.app/ChakavuMandera
WAFUGAJI WATAHADHARISHWA KUHUSU DAWA FEKI YA MIFUGO

> Ni Dawa ya Alben Blue 2.5% toleo Na. 019394 lililotengenezwa Novemba 2019 na mwisho wa matumizi Oktoba mwaka 2022

> TMDA imesema Dawa hiyo ya Mifugo imebainika haina viambata hai

Soma - https://jamii.app/MifugoDawa
#MAREKANI: ALIYEWAHI KUWA MAKAMU WA RAIS AFARIKI DUNIA

> Walter F. Mondale amefariki akiwa na miaka 93. Alikuwa Makamu wa Rais Jimmy Carter kuanzia 1977-1981

> Alishindwa kupata Urais 1984, lakini aliweka rekodi ya kuwa na Mgombea Mwenza Mwanamke

Soma - https://jamii.app/MakamuMarekani
UTAFITI-MAREKANI: MTU 1 KATI YA 4 ANAFIKIRIA KUACHA KAZI BAADA YA #COVID19

- 80% wataacha kazi kwa sababu wana wasiwasi juu ya maendeleo ya taaluma zao

- Wengine Corona imesababisha wajifunze ujuzi na ustadi mpya ili kupata kazi za aina nyingine

Soma - https://jamii.app/JobQuitCorona