JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rais Samia: Kamati ya kuchunguza #CoronaVirus imeshaundwa na hivi karibuni nitakaa nayo kujua namna tunavyokwenda

> Niwaombe viongozi wa dini, muwaombe waumini wenu wafuate hatua zote za kujikinga na #COVID19 kama kunawa mikono n.k
MAREKANI: WANAOJITOKEZA KUPATA CHANJO YA CORONA WAPUNGUA

> Mamlaka za #Marekani zimesema wanaojitokeza kupata Chanjo ya #COVID19 wamepungua sababu ikitajwa kuwa wengi wanasubiri kuona madhara ya chanjo hizo kwa ambao wameshapata

Soma https://jamii.app/ChanjoMarekani
TABORA: JELA MIAKA 21 KWA KUVUNJA NYUMBA NA KUIBA

> Hamisi Jilala Kwabi na Mohamedi Kassim wamehukumiwa kutumikia kifungo baada ya kukiri makosa 3 ya kuvunja na kuiba

> Ktk tukio mojawapo waliiba televisheni yenye thamani ya Tsh 1,100,000

Soma - https://jamii.app/JelaWizi
JE, NI SAHIHI KUFURAHIA MAHUSIANO YA VIJANA WADOGO?

> Mdau ameandika wazazi wengi hufurahia watoto wa kiume wakijihusisha na mapenzi wakiwa hata Shule ya Msingi na huonekana ni kawaida wakati huo huo wakichukizwa hali hiyo inapokuwa kwa watoto wao wa kike

> Je, ni kweli wazazi wako hivyo. Je unadhani ni sahihi?

Soma https://jamii.app/MaleziMahusiao
MSONGO WA MAWAZO (STRESS) NA DALILI ZAKE

- Dalili zinaweza kuanza kwa kujihisi mgonjwa, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa na kushindwa kutuliza akili. Iwapo upo kwenye Ndoa, unaweza kukosa kabisa hamu na mwenzako

- Kuwa na hasira bila sababu ya msingi, huzuni kila wakati, kuchoka bila hata kufanya kazi, hamu ya kula kuongezeka kwa kiasi kikubwa ama kutoweka kabisa

Soma - https://jamii.app/MawazoHuzuni
#StressAwarenessMonth
#UJERUMANI: MAKUBALIANO YA MRITHI WA KANSELA MERKEL YAKWAMA

- Vyama vya CDU na CSU vimeshindwa kufikia makubaliano ya atakayechukua nafasi ya Kansela Angela Merkel

- Wajumbe wenye nguvu wanawashinikiza Wagombea wakuu kumaliza tofauti zao

Soma - https://jamii.app/MkwamoMrithiMarkel
UFUGAJI: SABABU ZA KUKU KUPUNGUZA UTAGAJI WA MAYAI (1)

- Kupungua kwa saa za mwanga: Mwanga husisimua β€œpituitary gland” kwa Kuku ili kuchochea uzalishaji wa Mayai. Mtiririko mzuri wa utagaji wa Mayai huhitaji saa 14 mpaka 16 za mwanga (Jua)

- Msongo wa Mawazo (Stress) na mabadiliko mbalimbali: Ni rahisi kwa Kuku kuathirika na #Stress kwasababu hapendi mabadiliko ikiwemo chakula, mpangilio wa vyombo vya chakula na maji na kuwahamisha hamisha kila mara

Soma - https://jamii.app/MayaiKukuChini
#JFUfugaji
RAIS SAMIA KULIHUTUBIA BUNGE APRILI 22, 2021

- Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia Bunge la #Tanzania kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi jioni

- Spika Job Ndugai awataka Wabunge wote kuhakikisha wanakuwepo Bungeni wakati huo

Soma - https://jamii.app/SamiaBungeni
MICHEZO: JOSE MOURINHO ATIMULIWA TOTTENHAM HOTSPURS

- Imeripotiwa kuwa Chriss Powell na Ryan Mason wanajiandaa kuifundisha timu hiyo hadi mwisho wa mwezi Juni

- Bodi ya Timu hiyo imeanza mpango wa kupata kocha mpya

Soma > https://jamii.app/MourinhoOut

#Spurs #JamiiForums
JE, NINI KIFANYIKE KUWA NA MIPANGO MIJI MIZURI?

> Mdau wa #JamiiForums anasema hata maeneo mapya katika Miji hujengwa kiholela na kuwa changamoto

> Mbali na kazi nzuri inayofanywa na Wizara, Mdau anahoji njia nzuri za kuwa na Miji iliyopangika

Soma - https://jamii.app/MipangoMiji
DAR: WAZIRI MKUU ATEMBELEA KITUO CHA MAGARI YA MWENDOKASI GEREZANI

> Kassim Majaliwa amebaini mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi kutokana na mgogoro na msambazaji

> Meneja ametakiwa kuongeza magari kwani wakazi wa Kimara hupata shida

Soma https://jamii.app/MabasiYaMwendokasi
SERIKALI KUTOA MAFUNZO YA KUFUNDISHA HISABATI KWA WALIMU

- Serikali itaanza kutoa mafunzo kazini kuanzia Julai Mosi ikiwemo mbinu za ufundishaji

- Prof. Mkumbo asema wamebaini kuna Walimu hawamudu kufundisha baadhi ya mada katika somo hilo

Soma - https://jamii.app/MafunzoHisabati
DAR: MMOJA ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTANGAZAJI WA ITV

- Jeshi la Polisi Kinondoni linamshikilia Mtu mmoja ambaye jina linahifadhiwa kufuatia kifo cha Blandina Sembu ambaye Machi 27, 2021 mwili wake ulikutwa pembezoni mwa barabara

Soma - https://jamii.app/MbaroniKifoBlandina
MALAWI: WAZIRI WA KAZI ATIMULIWA KWA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA COVID19

> Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amewafukuza kazi maafisa wawili na Waziri wa Kazi, Ken Kandodo, kwa ubadhirifu wa Tsh. Bilioni 18 zilizolengwa kupambana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/WaziriMalawi
DR-CONGO YAANZA KUTOA CHANJO YA CORONA

> Taifa hilo limepokea Dozi Milioni 1.7 za Chanjo ya #AstraZeneca na wameanza kutoa kwa hiari kwa raia

> Awali utoaji chanjo hiyo ulisitishwa baada ya mataifa mengine kushuku usalama na ufanisi wake

Soma https://jamii.app/ChanjoDRC
RC CHALAMILA: MNAOMUONGELEA VIBAYA MAGUFULI WAKATI HAYUPO, MNATUCHOSHA AKILI

- Asema kuna Watu wameacha kufanya kazi wanakaa ili kumjadili Hayati Dkt. John Magufuli

- Asema kama wanaongea yenye maana ilifaa wafikishe ujumbe wakati akiwa hai

Soma https://jamii.app/ChalamilaSemaMagu
TIGO NA ZANTEL ZAUZWA KWA KAMPUNI YA MADAGASCAR

> Millicom International inayomiliki Tigo na Zantel, imetia saini ya kuuza biashara zake kwa Kampuni ya Axian Group

> Wateja wamehakikishiwa hakutakuwa na mabadiliko katika utoaji huduma

Soma - https://jamii.app/MilicomYauzaKampuni
RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI DIT, NACTE, COSTECH, DMI, TLSB, TAEC, TAFORI NA BODI YA MAABARA

- Dkt. Richard Masika anakuwa M/kiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia(DIT)

- Prof. Joseph Msambichaka ni M/kiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)

Soma - https://jamii.app/UteuziDIT
KENYA: WATU MILIONI 1.4 WAKABILIWA NA NJAA

> Shirika la Msalaba Mwekundu limebainisha Watoto 400,000 wasio na lishe bora wanahitaji msaada wa dharura

> Hali ya njaa inaweza kusababisha mapigano kugombea rasilimali finyu zilizopo

Soma - https://jamii.app/NjaaaKenya
MDAU ASHAURI WANAUME KUTOKUWA NA BAADHI YA TABIA

> Mdau ameshauri Mwanaume kutotumia maneno kama β€˜Xaxa’, 'Jomoni' au kutumia emoji za kuona aibu kwa Mwanaume mwenzako

> Je, ni vitu gani zaidi Mwanaume asifanye kwa Mwanaume mwenzake?

Soma https://jamii.app/TabiaZaKiume