JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UMOJA WA MATAIFA WAITAKA #UGANDA KUDHIBITI VURUGU

- Wametaka Wapinzani na Wanaharakati waliokamatwa kuondolewa mashtaka

- Pia, wameeleza wasiwasi wao kuhusu Vikosi vya Usalama kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na ongezeko la ukandamizaji

Soma > https://jamii.app/UNElectionsUG
MOI: KUNA ONGEZEKO KUBWA LA WAGONJWA WATOKANAO NA AJALI

> Kwa mwaka, vifo vinavyotokana na ajali ni kati ya 28 na 35, ikiwa ni vifo 2 hadi 3 kwa mwezi

> Nusu ya Wagonjwa wanaofikishwa MOI kutokana na ajali, chanzo chake ni bodaboda

Soma - https://jamii.app/WagonjwaMOI
#HealthCare
KIGOMA: WATOTO WATATU WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ZA MOTO

- Watoto wawili wa Familia moja wamefariki Kasulu na mmoja amepoteza maisha Kijiji cha Mpeta baada ya nyumba kuungua

- Wazazi/Walezi watakiwa kuacha tabia ya kuwaacha Watoto bila uangalizi

Soma > https://jamii.app/MotoVifo3
SERIKALI YAINGIZA TSH. BILIONI 123.6 KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI 2020

- Fedha hizo zimepatikana baada ya washtakiwa kukiri makosa yao na kurejesha fedha wanazodaiwa

- Utaratibu wa kukiri makosa kwa DPP ulitolewa na Rais Magufuli mwaka 2019

Soma https://jamii.app/FedhaUhujumu
TRA YATOA ONYO KWA WAFANYABIASHARA WASIOTUMIA ETS

- Ifikapo Januari 31, 2021, wasiotumia Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) hawataruhusiwa kuingiza bidhaa sokoni

- Bidhaa zilizotajwa ni juisi, maji ya chupa na bidhaa za filamu na Muziki

Soma - https://jamii.app/BidhaaMfumoETS
MDAU: MLEE MTOTO WAKO, USIMFUGE

- Kumfuga Mtoto ni kumlea kwa lengo la kujipatia kipato au faida, wakati lengo la Malezi ni kumuandaa Mtoto kwa yatakayomsaidia kukabiliana na changamoto za maisha yake

- Kumlea Mtoto sio kumpa tu chakula, mavazi na sehemu ya kulala. Ni lazima aambiwe na kufundishwa mambo yanayomhusu, yaliyopita, yaliyopo na yatakayokuja mbele yake

Soma - https://jamii.app/KufugaWatoto
#Malezi
ARGENTINA YAPITISHA MUSWADA WA KUHALALISHA UTOAJI MIMBA

> Muswada huo unawaruhusu Wanawake kutoa mimba kwa muda usiopita wiki 14 tangu kupata ujauzito

> Kati ya visa 370,000 na 520,000 vya utoaji mimba kinyume na Sheria hurekodiwa kila mwaka

Soma https://jamii.app/LegalAbortion
UGANDA: BOBI WINE AKAMATWA NA MAAFISA WA POLISI

> Msemaji wa Chama cha NUP, Joel Senyonyi, amesema Mgombea Urais, Robert Kyagulanyi na msafara wake wa watu 90 wamekamatwa kwenye Visiwa vya Kalangala walikokwenda kwa ajili ya mikutano ya Kampeni

#UGElection #HumanRights
SERIKALI YASITISHA MIKESHA YA USIKU KUCHA KATIKA MAENEO YA UMMA DESEMBA 31

- Utamaduni huo umesitishwa ktk Mikoa yote kutokana na changamoto mbalimbali za kiusalama

- Mikusanyiko ifanyike kwenye nyumba za Ibada na kumalizika saa sita na nusu usiku

Soma https://jamii.app/MkeshaMwakaMpya
KENYA: ZAIDI YA WATU 700 WAMEULIWA NA POLISI TANGU 2007

- Shirika la #HakiZaBinadamu la Missing Voices limesema Watu 144 wameuawa na Polisi mwaka 2020

- 59% ya mauaji hayo yalitokana na Polisi kuwaua watuhumiwa kwa kuwapiga risasi

Soma https://jamii.app/VifoUkatiliPolisi
#PoliceBrutality
MKESHA MWAKA MPYA: POLISI YASEMA KUKAA 'BEACH' MWISHO SAA 12 JIONI

- Wananchi watakaokusanyika katika fukwe za Bahari na Maziwa wametakiwa kurejea nyumbani ifikapo muda huo

- Pia, uchomaji wa Matairi na Disko Toto wapigwa marufuku

Soma > https://jamii.app/MkeshaPolisi
#UGANDA: MATUKIO YA UCHAGUZI KURIPOTIWA NA WAANDISHI WALIOIDHINISHWA

- Mchakato wa kuidhinishwa ambao ulikuwa wazi kwa Wanahabari wote unamalizika leo

- Polisi wadai hatua hiyo inalenga kusaidia Vikosi vya Usalama kuwatambua Wanahabari watiifu

Soma > https://jamii.app/MediaElectionsUG
RC TANGA: TRA MSIJENGE CHUKI KTK UKUSANYAJI WA KODI

- Martine Shigela, ametoa wito wa kuhakikisha Watumishi TRA na Wafanyabiashara hawajengeani chuki, kwa kudhani Wafanyabiashara wanakwepa kodi au TRA huja na makadirio yasiyokuwa na utaratibu

Soma https://jamii.app/ChukiTRAKodi
WANAODAIWA NA TTCL WAPEWA SIKU 30 KULIPA MADENI

- Waziri Dkt. Faustine Ndugulile amesema zaidi ya Taasisi 20 za Serikali zinadaiwa na TTCL zaidi ya bilioni 30

- Pia, ametoa onyo kwa wanaoiba nyaya za shaba za TTCL na kuuza kama chuma chakavu

Soma https://jamii.app/MadeniTTCL
SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOKWAMISHA UVUVI NA UFUGAJI

- Waziri Mashimba Ndaki amesema, Serikali inatafuta namna ya kuwa na Kituo kimoja cha kulipia tozo zote za mazao ya mifugo na uvuvi na vilevile kuondoa tozo ambazo zinakwamisha sekta hizo

Soma https://jamii.app/SerikaliTozo
SIMIYU: WENYEVITI 8 KUKAMATWA KWA KULA FEDHA ZA UJENZI WA MADARASA

- Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meatu, ameagiza kukamatwa kwa Wenyeviti wa vitongoji 8, ktk Kata ya Itinje wanaodaiwa kula fedha za michango ya ujenzi wa Madarasa

Soma - https://jamii.app/FedhaMadarasa
DODOMA: MKURUGENZI WA CHEMBA ATAKIWA KUJIELEZA KWA KUCHELEWESHA MIRADI

> Waziri Jafo ametoa maagizo hayo kutokana na ujenzi wa vyumba 2 vya Madarasa na Bweni la Shule ya Sekondari ya Chemba kutokamilika mwaka huu

> Pia, taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inaeleza fedha walizopokea ni Bilioni 1.5 badala ya Bilioni 1.8 zilizotolewa na Serikali

Soma - https://jamii.app/MiradiChembaJaffo
ARUSHA: WAFUASI WA CHADEMA WALIOTUHUMIWA KUHUJUMU UCHUMI WAPATA DHAMANA

- Watuhumiwa hao waliokuwa wanashtakiwa kwa mashauri tofauti wanadaiwa kutenda kosa la kuunda genge la uhalifu na kuwashawishi watu kutenda uhalifu eneo la bondeni Anex

Soma https://jamii.app/DhamanaCDM19
DAKTARI ABAINIKA KUTUMIA HOSPITALI YA SERIKALI KWA MANUFAA BINAFSI

> Daktari huyo anadaiwa kutumia Hospitali ya Amana kuwatibu Wagonjwa lakini malipo yote huyapokea binafsi

> Waziri wa Afya ameagiza hatua za kinidhamu zifuatwe kumshughulikia

Soma https://jamii.app/UkaguziAmana
SERIKALI KUANZISHA VITUO VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO DODOMA NA DAR

- Vituo 30 vinajengwa ili Watoto wapate sehemu sahihi ya kulelewa wakati Wazazi/walezi wanapokuwa kazini

- Pia, vitasaidia kuondokana na vitendo vya Ukatili kwa Watoto wadogo

Soma https://jamii.app/VituoMaleziWatoto