JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBEYA: RUWASA YAPEWA SIKU 14 KUKAMILISHA MIRADI KWENYE VIJIJI 6

- Pia, Mamlaka ya Maji Vijijini imepewa mwezi 1 kukamilisha mradi wa maji wa Vijiji viwili vya Kata ya Igale ambavyo havijawahi kupata maji ya bomba kutokana na Jiografia yake ya milima

Soma https://jamii.app/MiradiMajiMby
MARUFUKU YA KAMPENI UGANDA: MUSEVENI ASEMA TUME IMEMLINGANISHA NA BOBI WINE

- Ameishutumu Tume kwa kumlinganisha na Wagombea wengine akiwemo Bobi Wine, ambao wamekuwa wakifanya mikusanyiko

- Asema yeye hajawahi kuwa na idadi kubwa ya watu

Soma - https://jamii.app/ECMuseveni
RAIS MAGUFULI ATAKA WANAOTOA RISITI ZA UONGO WASHUGHULIKIWE

> Ameeleza kuchukizwa na suala la Wananchi kununua bidhaa bila kupewa risiti

> Asema kuna wanaouza bidhaa ya milioni 2 lakini wanatoa risiti ya elfu 2 na kuitaka TRA kuwashughulikia

Soma https://jamii.app/TRARisitiUongo
AFRIKA YA KATI: VITUO 800 VYA KUPIGIA KURA HAVIKUFUNGULIWA SIKU YA UCHAGUZI

- Tume ya Uchaguzi imesema baadhi ya Wapiga Kura walipigwa na wengine kutishiwa kuuawa

- Ghasia ziliripotiwa wakati wa Kampeni na waasi walilenga kuvuruga Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/VotingCAR
RAIS MWINYI: NITAMSIMAMISHA KAZI KIONGOZI ATAKAYETUHUMIWA KWA RUSHWA

> Rais wa #Zanzibar amesema atamsimamisha kazi Kiongozi atakayetuhumiwa kwa rushwa kupisha uchunguzi, na akikutwa hana hatia, atarejeshwa kazini bila kupoteza stahiki zake

Soma - https://jamii.app/RushwaKaziZbar
VIKWAZO VYA KIUCHUMI: FAHAMU KUHUSU AINA ZA VIKWAZO HIVI (SEHEMU YA 2)

1. Unilateral Sanctions: Huwekwa na Taifa moja, hususani Marekani dhidi ya Taifa lingine, au Shirika lililo ndani ya Taifa fulani, au Wanasiasa wake. Huzuia kusafiri kwa kiongozi au kikundi cha watu (travel ban) au kufilisiwa mali, hususani fedha

2. Multilateral Sanctions: Ni vikwazo vinavyosimikwa na Mataifa mengi au Jumuiya ya Kimataifa. Mara nyingi vinapitia Umoja wa Mataifa hasa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (The UN's Security).

Soma - https://jamii.app/EconomicSanctions
#Economy
TABORA: POLISI WAKAMATA WATUHUMIWA 683 NDANI YA WIKI TATU

- SACP Mihayo Msikhela amesema kati yao, 277 wamefikishwa Mahakamani na kuhukumiwa, kesi 255 bado zinaendelea na 42 wapo ktk uangalizi wa Polisi baada ya kutokuwepo kwa ushahidi

Soma - https://jamii.app/683PolisiTbr
RIPOTI: WAANDISHI 40 KATI 50 WALIOUAWA 2020 WALILENGWA MAKUSUDI

> Ingawa idadi ya Waandishi wanaouawa wakiripoti matukio ya mapigano imepungua, wanaouawa kwa kudhamiriwa imeongezeka

> #Mexico imeshika nafasi ya juu kwa Nchi hatari kwa Waandishi

Soma - https://jamii.app/MauajiWaandishi
WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA WA ARDHI MWANZA

- Kaimu Kamishna wa Ardhi Msadizi Mkoani Mwanza, Biswalo Makwasa Musesa amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kukiuka maadili ya kazi zinazomkabili

Soma - https://jamii.app/KamishnaMwz
TAKUKURU YAREJESHA VIFAA GHAFI VYA BILIONI 1.2 TANESCO

- Vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh. 1,216,840,360 vilipotea kwa mbinu mbalimbali

- Pia, Taasisi hiyo imewataka Wakandarasi 16 waliopewa Notisi tangu 2017 kurejesha vifaa ndani ya siku 14

Soma - https://jamii.app/VifaaTANESCO
RIPOTI YA POLISI PWANI: MAKOSA YA JINAI YAPUNGUA KWA MWAKA 2020

- Yameripotiwa makosa ya jinai 1,791 kufikia Desemba 2020 ikilinganishwa na makosa 2,189 ya 2019

- Makosa hayo ni mauaji, kubaka, wizi wa Watoto, usafirishaji haramu wa binadamu

Soma https://jamii.app/UhalifuPwani
DAR: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSAMBAZA PICHA ZA NGONO WHATSAPP

- Faraji Omary amefikishwa Kisutu kujibu mashtaka 4 likiwemo la kusambaza picha za ngono na machapisho yenye ujumbe mchafu

- Amekana mashtaka na kesi imeahirishwa hadi Januari 11, 2021

Soma https://jamii.app/KisutuMashtaka4
ULAYA: UDHALILISHAJI WATOTO MTANDAONI WAONGEZEKA KIPINDI CHA #COVID19

- Ripoti ya Taasisi ya Polisi ya Umoja wa Ulaya (Europol) inasema watuhumiwa wengi huwasiliana na Watoto wanaotumia muda mrefu mitandaoni hasa wakati huu wanavyobaki nyumbani

Soma - https://jamii.app/ChildAbuseEuropol
#ChildAbuse
SERIKALI YATAKA SHIRIKA LA POSTA KUENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

- Dkt. Ndugulile aagiza Sera na Sheria ya Posta kupitiwa ili ziweze kuendana na mabadiliko ya Teknolojia Duniani

- Ametoa siku 90 kwa Shirika hilo kuboresha utendaji kazi

Soma https://jamii.app/TPCHuduma
AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA YARIPOTIWA MAREKANI

- Kirusi hicho kimeripotiwa ktk mji wa #Colorado kwa kijana (20) ambaye hana historia ya kusafiri

- Kirusi cha B.1.1.7 tayari kimeripotiwa #Canada, Italia, India, Falme za Kiarabu na Chile

Soma - https://jamii.app/NewCoronaUS
MISRI: MWANAFUNZI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 KWA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

- Ahmed Bassem Zaki (22) amekutwa na hatia ya kuwanyanyasa kijinsia Wanawake wawili Mtandaoni

- Mashtaka dhidi yake yalichochea kwa kiasi kikubwa Kampeni ya #MeToo

Soma https://jamii.app/JailAbuseEgypt
NEPAL: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA UAMUZI WA WAZIRI MKUU KUVUNJA BUNGE

- Wanamtaka K.P. Sharma Oli kubatilisha uamuzi wake wa kuvunja Bunge na kuitisha Uchaguzi Mkuu wa mapema

- Wasema uamuzi huo uliofanywa Desemba 20 upo kinyume na #Katiba

Soma https://jamii.app/NepalProtestOli
AFRIKA KUSINI: MIGAHAWA YAONYWA KUHUSU MAUZO YA VILEVI

- Serikali imesema watakaokiuka marufuku hiyo inayolenga kudhibiti janga la #COVID19 watashtakiwa

- Migahawa yatakiwa kutoweka pombe kwenye chupa za chai au zile zilizoandikwa hakuna kilevi

Soma > https://jamii.app/AlcoholSaleSA
WATUMISHI WANAOHUSIKA KWENYE UPOTEVU WA DAWA KUCHUKULIWA HATUA

- Naibu Waziri wa Afya asema, kuna mtandao mkubwa wa dawa zinazoibiwa kidogo kidogo

- Amesema kuna shida kubwa kwenye usimamizi kuanzia Hospitali za Taifa mpaka Vituo vya Afya

Soma > https://jamii.app/UpotevuDawa
#COVID19: CHANJO YA ASTRAZENECA YAIDHINISHWA UINGEREZA

- Itaanza kutolewa kwa Umma Januari 04, na dozi Milioni 100 ambazo zinatosha kutolewa kwa watu Milioni 50 zimeagizwa

- Ni Chanjo ya pili kuidhinishwa baada ya ile kutoka Pfizer-BioNTech

Soma https://jamii.app/AstraZenecaUK