JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#GHANA: RAIS ADDO ASHINDA UCHAGUZI MKUU

> Rais Nana Akufo-Addo amepata 51.6% ya kura zote huku mpinzani wake, John Mahama akipata 47.4%

> Mahama ambaye alikuwa Rais kuanzia 2012-2017 bado hajatoa kauli yoyote kuhusu kukubali matokeo

Soma - https://jamii.app/AddoWinsGH
KUONGEZEKA KWA JOTO NYAKATI ZA USIKU KTK MIKOA 13 NA ZANZIBAR

> TMA imesema kutakuwa na hali ya joto kutokana na kiwango kikubwa cha unyevu angani kinachofikia zaidi ya 80%

> Joto litaongezeka Februari 2021 na kupungua kuelekea Machi 2021

Soma - https://jamii.app/JotoUsiku
ETHIOPIA: UPINZANI WATAKA VIONGOZI WAO KUACHIWA HURU

> Chama Kikuu cha Upinzani kimesema ni ngumu kujiandaa na Uchaguzi bila Viongozi hao waliokamatwa Julai kufuatia vurugu baada ya kifo cha Mwanamuziki/Mwanaharakati, Hachalu Hundessa

Soma - https://jamii.app/UpinzaniET
BAGONZA: MARA ZOTE MSEMA KWELI LAZIMA ACHUKIWE

> Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amesema, ni lazima kila mtu awe tayari kusimamia ukweli na kukubali gharama

> Asema, kuna dalili za kuliangamiza Taifa kwa sababu watu wanaamini uongo

Soma - https://jamii.app/BagonzaUkweli
#Siasa
MAREKANI: YOUTUBE KUFUTA MAUDHUI YANAYODAI UCHAGUZI ULIKUWA NA UDANGANYIFU

- Mabadiliko yatafanyika kwa video mpya, zikiwemo zinazotoka kwa Rais Trump

- #YouTube imesema Majimbo mengi yameshathibitisha matokeo ya Uchaguzi kuamua Rais Mteule

Soma https://jamii.app/VoterFraudVideos
DESEMBA 10: SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI ZA BINADAMU

- Iliasisiwa na Umoja wa Mataifa 1950 ili Watu watambue umuhimu wa #HakiZaBinadamu na utunzaji wake

- Dunia inatakiwa kulinda haki za makundi maalum na kuzuia ubaguzi na umasikini

Soma - https://jamii.app/HumanRights2020
#HumanRightsDay
WIZARA YA MALIASILI: MAINI NA MAFUTA YA TEMBO SIO DAWA YA KANSA

- Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Kijazi amesema, hakuna utafiti wa Kisayansi unaoonesha mafuta na maini ya Tembo ni Dawa ya Kansa, na Majangili wanawadanganya Wananchi

Soma - https://jamii.app/TemboDawaKansa
DUNIA YATAHADHARISHWA KUHUSU ONGEZEKO LA JOTO

- Mpango wa Mazingira wa UN (UNEP) umesema Joto la Dunia linaelekea kuongezeka kwa zaidi ya digrii 3

- Shirika la Hali ya Hewa Duniani limesema 2020 ungekuwa mwaka wa Joto wa 3 baada ya 2016 na 2019

Soma https://jamii.app/RiseHeatEarth
GODBLESS LEMA APATA HIFADHI CANADA

- Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA) amepata hifadhi ya kisiasa nchini #Canada

- Kwa mujibu wa Wakili wake, George Luchiri Wajackoyah, Lema pamoja na Familia yake wameondoka Kenya jana

Soma https://jamii.app/LemaCanada
FACEBOOK YAKABILIWA NA KESI YA KUTAKA KUUA KAMPUNI PINZANI

- Kampuni ya #Facebook Inc inaweza kulazimishwa kuuza mali zake ikiwemo #WhatsApp na #Instagram baada ya Tume ya Biashara ya Marekani kufungua kesi ikisema iliwarubuni washindani wake

Soma https://jamii.app/FBLawSuits
#COVID19: AFRIKA KUSINI YAKUMBWA NA WIMBI LA PILI LA MAAMBUKIZI

- Waziri wa Afya asema, kuna ongezeko la maambukizi kwa wenye miaka 15-19 kutokana sherehe nyingi zinazohusisha Vijana

- Visa vimefikia 828,598, vifo 22,574 na 754,658 wamepona

Soma - https://jamii.app/2ndWaveSA
PICHA YA DIEGO MARADONA YAPENDEKEZWA KUCHAPISHWA KWENYE PESA YA #ARGENTINA

> Seneta Norma Durango amewasilisha Muswada Bungeni unaopendekezwa uso wa #Maradona na picha ya moja ya mabao yake kuwekwa kwenye noti kubwa zaidi ya Nchi hiyo

Soma https://jamii.app/MaradonaCurrency
#JFLeo #Sports
PINDA: WATUMISHI WANAPASWA KUWA MSAADA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

- Waziri Mkuu Mstaafu ametoa wito kwa Watumishi kujitathmini ikiwa wanazingatia miongozo ya kazi

- Pia, amewataka Viongozi kuhakikisha wanasimamia ahadi na viapo vya uadilifu

Soma - https://jamii.app/PindaKeroWananchi
MSUMBIJI: SERIKALI YAPINGA RAIA KUPEWA SILAHA ILI KUDHIBITI MASHAMBULIZI

- Waziri Mkuu amesema ni hatari na silaha zinapaswa kumilikiwa na watu sahihi

- Wakazi wa Cabo Delgado wamekuwa wakiomba kupatiwa silaha wasaidie kupambana na Wanamgambo

Soma - https://jamii.app/SilahaWananchiMZ
MAJALIWA: TUSIKUBALI KUSHAWISHIWA NA ANAYETUMIWA NA WATU WENYE LENGO LA KUTUTAWALA

- Amewataka Vijana wasikubali kurubuniwa na Watu wasioipenda #Tanzania

- Asema #Uzalendo ni muhimu ktk kujenga umoja na Vijana ni zaidi ya 60% ya Watanzania

Soma - https://jamii.app/MajaliwaUzalendo
DAR: MFANYABIASHARA AJIUA KWA MSONGO WA MAWAZO

- Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesema tukio limetokea Ubungo Kibangu na Marehemu alijipiga risasi akitumia bastola ya Revolver

- Ktk tukio lingine, Polisi wamethibitisha kuuawa kwa jambazi 1

Soma https://jamii.app/TaarifaPolisi
MAALIM SEIF: ACT-WAZALENDO IPO NA ITAENDELEA KUWEPO

- Asema, nguvu ya Chama hicho si silaha wala mabomu bali ni Umoja na mshikamano uliopo

- Ameeleza kuwa, ana jukumu la kutekeleza yaliyoamuliwa kwenye Vikao vya Kitaifa na atasimamia hilo

Soma - https://jamii.app/ACTMaalimSeif
SIKU YA HAKI ZA BINADAMU: WANAHABARI 42 WAMEUAWA 2020 WAKIWA KAZINI

- Ripoti mpya ya IFJ inasema #Mexico inaongoza kwa idadi ya Waandishi wanaouawa ikifuatiwa na #Pakistan

- Mataifa mengine ni #Afghanistan, India, Iraq na Nigeria

Soma - https://jamii.app/IFJJournalistsDeath
#HumanRights
UJASIRIAMALI: FAHAMU FALSAFA YA BIASHARA ILI KUPATA MAFANIKIO

- Mdau anasema, Falsafa ya #Biashara ni seti ya Kanuni, Taratibu na Mienendo ambayo Mfanyabiashara au Kampuni inaiamini na hutumia kuamua jinsi ya kushughulikia maeneo ya utendaji

- Falsafa ya biashara inaelezea kusudi la biashara na malengo yake. Inaweza kuorodhesha maadili maalum ambayo ni muhimu kwa Wafanyakazi, Watendaji au mipaka, ambayo husaidia kukua kwa biashara

Soma zaidi - https://jamii.app/FalsafaBiashara
#Biashara