JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NEC YATAKA USHAHIDI WA VITUO HEWA KWA WANAODAI HIVYO

> Mkurugenzi wa NEC amesema tuhuma hizo zinaweza kuzua taharuki kwa jambo ambalo si la kweli

> Asema vituo ni vingi kwasababu kila kituo wameweka Wapigakura wasiozidi 500

Soma - https://jamii.app/UshahidiVituoHewa
#Uchaguzi2020
NEC YASISITIZA: KAMA HAUPO ULIPOJIANDIKISHA HUTOWEZA KUPIGA KURA

> Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema ruhusa ya kufanya hivyo inatolewa kwa Watendaji ambao wameajiriwa na Tume ila sio kwa Mwananchi

Tazama - https://youtu.be/qwrI--yD_sM

#Uchaguzi2020
CHAMA CHA MAPINDUZI CHAFUNGA KAMPENI ZAKE VISIWANI ZANZIBAR

> Dkt. Hussein Mwinyi amefunga kampeni akisema kuzunguka kumempa fursa ya kutambua uzito wa dhamana ya nafasi ya Urais

> Amesema, dhamira yake ya kuwatumikia Wazanzibari ipo imara

Soma https://jamii.app/CCMKampeniZnz
#TZ2020
MBOWE: LISSU ANAKUWA RAIS, MUNGU AKIPENDA MIMI NITAKUWA WAZIRI MKUU

> Aidha, ameongeza, "Uchaguzi huu sio kati ya CHADEMA na CCM wala Lissu na Magufuli bali ni kati ya wanaopenda uhuru na #haki na waliokandamiza uhuru na #Demokrasia"

Soma - https://jamii.app/MboweWaziriMkuu
#TZ2020
SHINYANGA: WATANO MBARONI KWA VURUGU KATIKA MSAFARA WA CHADEMA NA CCM

> Vurugu zilitokea msafara wa Patrobas Katambi (CCM) na Salome Makamba (CHADEMA) ulipokutana

> Polisi imewataka Wanasiasa na wafuasi kuacha maandamano baada ya kampeni

Soma https://jamii.app/5FujoShinyanga
#TZ2020
MGOMBEA(SAU): KAMA MWENZAKO AMEFANYA KAZI NZURI MPONGEZE

> Muttamwega Mgaywa amesema akiingia Ikulu atamteua Dkt. Magufuli kuwa Waziri Mkuu kutokana na utendaji wake

> Asema, ataanzia alipoishia Magufuli na ataleta ndege 30 ktk Uongozi wake

Soma https://jamii.app/SAUMagufuli
#TZ2020
IGP SIRRO: TUNA TAARIFA ZA VIKUNDI VINAVYOPANGA KUVURUGA UCHAGUZI ARUSHA

> Amewaomba Wananchi kuendelea kuimarisha Amani na Utulivu siku ya Uchaguzi

> Asema, Polisi wapo tayari kulinda Taifa ktk nyanja zote na Wahalifu watawashughulikiwa

Tazama - https://youtu.be/Lx8NLJyZEms
#TZ2020
DKT. BASHIRU: CCM IMEFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU, UPENDO UMETAWALA

> Amesema wamefanya Kampeni ambazo hazikuwa na hasira licha ya umati mkubwa

> Vilevile, amesema watajitahidi ushindi wao uambatane na kudumisha amani na upendo kwa watu wote

Soma https://jamii.app/BashiruCCM
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: SUMAYE NI MWANACCM HALISI AMBAYE ALIKUMBWA NA MAPEPO

> Amesema, “Mungu alipoumba Malaika wengine wakagoma wakatupwa Duniani. Wale ndio wakamgusa Mzee Sumaye akahamia chama ambacho ni cha ajabu, kinachomtukana kila mmoja"

Soma https://jamii.app/SumayeMapepo
#TZ2020
MAGANJA WA NCCR-MAGEUZI AAHIDI KUBADILI SHERIA KANDAMIZI

> Jeremiah Maganja pia amesema, ataboresha uchumi na kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara

> Atafuta Vitambulisho vya Bima ya Afya kwani haviwanufaishi walionavyo

Soma - https://jamii.app/AhadiNCCR
#Uchaguzi2020
MAJALIWA: KAMPIGIE KURA MAGUFULI HATA KAMA UNATOKA UPINZANI

> Akiwa Mkoani Lindi, amewataka wakazi wa eneo hilo kumshukuru Dkt. Magufuli kwa mazuri aliyowafanyia kwa kumpa kura nyingi za kishindo siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MajaliwaLindi
#Uchaguzi2020
LISSU: MADARASA MIJINI YAMEFURIKA WANAFUNZI, TUTAJENGA SHULE MPYA

> Amesema ujenzi wa miundombinu umekuwa duni ukilinganisha na ongezeko la Wanafunzi

> Atafanya mabadiliko kwa kuhakikisha Shule, Vyoo na Nyumba za Walimu mpya zinajengwa

Soma - https://jamii.app/LissuElimu
#TZ2020
NEC: JINA LA LISSU NI LA MWISHO KWENYE KARATASI KWASABABU ALIKUWA WA MWISHO KURUDISHA FOMU

> Ofisa Elimu kwa Umma wa NEC amesema, kigezo kilichotumika ni urejeshwaji fomu

> Amesema, hii sio sababu ya Mpiga Kura kutompigia Mgombea anayemtaka

Soma https://jamii.app/NECMajinaWagombea
#TZ2020
SIMIYU: MINADA NA MAGULIO YASITISHWA KUPISHA UCHAGUZI

> RC Anthony Mtaka amesitisha magulio na minada yote siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 28

> Hatua hiyo inalenga kuwapa nafasi wananchi kupiga kura kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani

Soma - https://jamii.app/MinadaOkt28
#Uchaguzi2020
MEMBE KUFUNGA KAMPENI ZAKE KESHO MKOANI LINDI

> Amesema, Oktoba 28 ni siku ya kupiga kura ya kurejesha Uhuru uliopotea na kuchagua mtu mwenye uchungu na maendeleo ya Nchi

> Awataka Wananchi kupuuza watu wanaosema amejiondoa kugombea Urais

Soma - https://jamii.app/MembeKampeni
#TZ2020
CHEMBA, DODOMA: DKT. MAGUFULI AAHIDI KUTATUA TATIZO LA MAJI

> Mgombea huyo wa Urais (CCM) amesema, "Hatuwezi tukawa na Wilaya jirani na Makao Makuu halafu haina maji"

> Amesema, tumeweza Treni ya Umeme na Bwawa la Nyerere, hatusindwi maji

Soma https://jamii.app/JPMChemba
#TZ2020
SHEIKH MWAIPOPO: LISSU ANAWATUMIA MASHEIKH WA GEREZANI KUOMBA KURA

> Amesema, wakati Masheikh wanakamatwa, Tundu Lissu alikuwa Mwanasheria ila hajawahi kuwatetea

> Amwomba Dkt. Magufuli awaonee huruma Masheikh hao ingawa yeye hakuwakamata

Soma - https://jamii.app/MasheikhLissu
#TZ2020
FAHAMU WATU WANAORUHUSIWA KUWEPO WAKATI WA KUHESABU KURA

> Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Taifa Kifungu cha 72(1)

> a) Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi

> b) Msaidizi wa Msimamizi wa Kituo

> c) Wakala wa Mgombea au mbadala wake

Soma > https://jamii.app/WahusikaVituo
#Uchaguzi2020
TUMIA HAKI YAKO YA KIKATIBA KUCHAGUA VIONGOZI. NENDA KAPIGE KURA OKTOBA 28

> Kura inampa nafasi Mwananchi ya kutimiza #haki yake kwa kushiriki ktk ujenzi wa maendeleo ya nchi

> Kura inatoa nafasi ya kidemokrasia kwa Mwananchi kukabidhi Madaraka na Mamlaka ya Kikatiba aliyonayo kwa Serikali kupitia wawakilishi

#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: HUU NI MWAKA WA MABADILIKO, HAKUNA LA KUTUZUIA

> Amesema, watasimama kwa pamoja kulinda ushindi wao

> Viongozi wa ACT-Wazalendo wameuhakikishia Umma watakuwa pamoja na Wananchi kuvishinda vitimbi vya ZEC na Vyombo vya Dola

Soma - https://jamii.app/MaalimUchaguziZnz
#TZ2020