JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LISSU: MIMI SIO WA KWANZA KUWA NA WAKILI MWINGEREZA

> Tundu Lissu amesema hata Mwl. Nyerere aliwahi kumtumia Wakili kutoka Uingereza

> Amesema hayo alipoulizwa kuhusu kujihusisha na Mataifa ya nje kwani hata Wakili wake ni raia wa Kigeni

Soma https://jamii.app/WakiliMuingereza
#TZ2020
ACT-WAZALENDO WAANDIKA BARUA KWA MSAJILI KUHUSU KUKOMA KIKATIBA KWA UANACHAMA WA ZITTO NA MAALIM

> Wanachama wamesema Maalim Seif na Zitto wamekosa sifa. Katiba yao Ibara ya 13(4) inasema mwanachama atapoteza sifa akiunga mkono chama kingine

Soma https://jamii.app/ZittoVsMaalim
#TZ2020
NEC: MADAI YA UWEPO WA VITUO HEWA NI UZUSHI

> NEC imesema imebaini watu wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao wamejipanga kuharibu taswira ya Uchaguzi

> Imetoa onyo ikisema haitosita kuwachukulia hatua kwasababu wanafanya uchochezi

Soma - https://jamii.app/NECViongoziUzushi

#TZ2020
ARUSHA: ADC YAAHIDI KUJENGA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI NA SOKO

> Queen Sendiga ameahidi kujenga Chumba cha Kuhifadhi maiti ktk Hospitali ya Arumeru endapo atachaguliwa kuwa Rais

> Ameahidi kujenga soko jipya ndani ya miezi 3 ya mwanzo

Soma https://jamii.app/ADCAhadiArumeru
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: ACT WAZALENDO ITAJALI MAKUNDI MAALUM

> Mgombea Urais Zanzibar, Maalim Seif amesema watahakikisha kuna usawa wa kijinsia kwenye ajira

> Walemavu watawekewa mazingira rafiki, Serikali itawalipia Wazee nauli za daladala

Soma https://jamii.app/MakundiMaalum
#Uchaguzi2020
LISSU: NI KWELI NINA TIKETI YA KWENDA UBELGIJI

> Mgombea Urais wa JMT (CHADEMA), Tundu Lissu amesema atakwenda Ubelgiji Desemba 18 ili akaonane na Daktari wake Desemba 20, 2020

> Amesema hayo akijibu hoja ya Dkt. Magufuli kuwa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za kuondoka Nchini baada ya kusababisha fujo

Soma https://jamii.app/LissuTiketiNdege
#TZ2020
RC CHALAMILA: TUMEJIPANGA KUKABILIANA NA VIJANA WALIOANDALIWA KUFANYA VURUGU

> Amedai wanazo taarifa za Vijana 150 kuandaliwa kila Kata na Upinzani

> Amewataka wananchi kupiga kura na kutobaki Vituoni kwani kulinda kura si jukumu lao

Soma - https://jamii.app/UchaguziMby
#TZ2020
LISSU: JARIBIO LOLOTE LA KUVURUGA UCHAGUZI LITASABABISHA WATU WAPELEKWE 'THE HAGUE'

> Asema kuna uchunguzi unaendelea na ipo orodha ya watu wanaoangaliwa

> Yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi anajiingiza ktk orodha hiyo

Soma https://jamii.app/LissuUchaguzi
#TZ2020
MARA YA MWISHO TRENI ILIENDA ARUSHA MWAKA 1986

> TRC wamesema, ni kama Mwl. Nyerere alipoondoka Madarakani aliondoka na huduma ya Reli Kaskazini

> Wamesema ukarabati wa Reli hiyo umegharimu Tsh. Bilioni 14 ambazo zimetolewa na Serikali

Soma https://jamii.app/TreiArusha
POLISI WAMHOJI HALIMA MDEE KWA TUHUMA ZA KUMILIKI VINASA SAUTI

> Mdee alienda kuripoti tukio la watu kumfuatilia, alipofika aliwekwa chini ya ulinzi akiambiwa kuna Jalada lake

> Polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake na kuondoka na kompyuta

Soma https://jamii.app/MdeePolisi
KATIBU MKUU WA ACT-WAZALENDO ASHIKILIWA NA POLISI

> Taarifa ya ACT-Wazalendo inasema, Ado Shaibu anatuhumiwa kuhamasisha Wakulima wa Korosho kugomea Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na kujilinda dhidi ya Tembo wanaovamia Mashamba na Makazi yao

Soma - https://jamii.app/AdoShaibuArrested
#TZ2020
NEC WATOA SABABU YA KUZUIA MKUTANO WA LISSU SOMANGA

> Oktoba 23, 2020 Polisi walitumia mabomu ya machozi kuzuia Mkutano wa Tundu Lissu

> NEC wamesema mkutano huo haukuwa ktk ratiba na ilitakiwa kukubaliana juu ya mabadiliko ya ratiba

Soma https://jamii.app/LissuSomanga
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI AMSIFIA DKT. SLAA KAMA MPINZANI ALIYEKUWA NA MASLAHI YA WATU

> Dkt. John Magufuli amemsifu Dkt. Wilbroad Slaa kuwa mpinzani aliyekuwa na hoja zenye manufaa kwa Taifa

> Asema, alimteua kuwa Balozi wa nchi 9 kutokana na uzalendo wake

Soma https://jamii.app/SlaaVsMagufuli
#TZ2020
TANZIA: MTANGAZAJI WA TBC, ELISHA ELIA AFARIKI DUNIA

- Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Elisha Elia amefariki dunia leo Oktoba 24, 2020

- Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Ayoub Rioba amesema kifo hicho kimetokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa amelazwa kwa matibabu

Soma https://jamii.app/RIPElisha

#Tanzia #JFTanzia
LA LIGA: ZIDANE AENDELEZA UBABE DHIDI YA BARCA

Zinedine Zidane ameendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika Dimba la Nou Camp kama Kocha baada ya Barcelona chini ya Kocha Ronald Koeman kuambulia kichapo cha bao 3 kwa 1 ikiwa nyumbani katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga

Magoli ya Real Madrid yamefungwa na F.Valverde dakika ya 5, na kunako dakika ya 63 S.Ramos akaindikia timu hiyo goli la pili kwa mkwaju wa penati, na goli la tatu kukamilisha ushindi wao likafungwa na L.Modric kunako dakika ya 90, huku goli pekee la Barcelona likifungwa na A.Fati dakika ya 8

Hii ni El Clasico ya kwanza tangu msimu huu kuanza pia ni ya mwisho katika muongo huu, ambapo imeikutanisha miamba hiyo ya La liga Santander wakati ambao timu zote zimepoteza michezo yao ya ligi Juma lililopita
FAHAMU IDADI YA WALEMAVU WANAOTARAJIWA KUPIGA KURA - 2020

> Walemavu wa Macho ni 2,223 na Walemavu wa mikono ni 4,911

> NEC wameeleza kuwa Walemavu wa aina nyingine ni 6,077

> Jumla yao inakadiriwa kuwa wanaweza kufikia 13,211

#Uchaguzi2020 #TZ2020 #JamiiForums #JamiiTalks
PROF. LIPUMBA: CUF ITAHAKIKISHA WANANCHI WANAONDOKANA NA MAAFA YA MAFURIKO

> Akiwa Kilwa Kaskazini amesema, CUF itawekeza katika mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi

> Pia, ameahidi kujenga barabara ya Nangurukuru-Liwale

Soma https://jamii.app/CUFKilwa
#Uchaguzi2020
DC KANONI: HAKUNA KUFANYA SHEREHE OKTOBA 27 NA 28

> Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe, Lauter Kanoni amewaagiza Watendaji wake kuhakikisha Wananchi hawafanyi sherehe Oktoba 27 na 28 ili wajiandae kushiriki Uchaguzi Mkuu

Soma https://jamii.app/NjombeSherehe
#Uchaguzi2020