JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GUINEA: WATU 10 WAUAWA KUTOKANA NA GHASIA BAADA YA UCHAGUZI

> Raia 8 na Polisi 2 wameuawa ktk ghasia za kupinga matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Rais

> #Guinea ilifanya Uchaguzi Oktoba 18 na matokeo yanaonesha Rais Alpha Conde anaongoza

Soma https://jamii.app/GhasiaUchaguziGuinea
CECILIA MMANGA: WAUGUZI WENYE SHAHADA HAWATAKI KWENDA VIJIJINI

> Mgombea Urais kupitia Demokrasia Makini amesema Watawasomesha wasafishaji wa Wodi za Hospitali kozi za Ukunga na wakifuzu watapelekwa Vijijini ili kupunguza vifo vya Wajawazito

Soma https://jamii.app/VifoWajawazito
#TZ2020
#NIGERIA: WATU 12 WAUAWA NA POLISI KATIKA MAANDAMANO

> Shirika la Amnesty International limesema uchunguzi umebaini ushahidi wa vifo 12 huku mamia wakijeruhiwa

> Limewatuhumu Polisi na Wanajeshi kutumia nguvu kupita kiasi

Soma https://jamii.app/12DeadNGR
#EndSARS
RAIS MAGUFULI: TANZANIA INAHITAJI JOZI MILIONI 54 ZA VIATU KWA MWAKA

> Ameyasema hayo alipokuwa anazindua Kiwanda cha bidhaa za Ngozi kilichopo Mkoani #Kilimanjaro

> Kiwanda hicho kitatengeneza ajira milioni 3 na ajira 3000 za moja kwa moja

Soma https://jamii.app/MagufuliViwanda
RAIS MAGUFULI: TANZANIA 'IMETOBOA' KWENYE MAENDELEO YA KWELI

> Amesema Kiuchumi #Tanzania imetoboa kutokana na wingi wa Viwanda vilivyopo

> Ametoa wito kwa Watanzania kununua bidhaa za ndani ili kukuza #Uchumi wa Nchi

Soma https://jamii.app/MagufuliViwanda
MMANGA: VIJANA MSISUBIRI AJIRA, KUWENI KAMA MARASTA

> Mgombea Urais JMT kupitia Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga amewataka Vijana kuacha kusubiri ajira Serikalini

> Asema Serikali yake itakuja na kauli ya 'Kilimo cha kufa na Kupona'

Soma https://jamii.app/DemkorasiaMakiniAjira
#Uchaguzi2020
RAIS MAGUFULI: TANZANIA NYEUPE PEE (HAINA CORONA)

> Amesema, chapisho la Gazeti la New York Times kuhusu hali ya #COVID19 Duniani limeitaja #Tanzania ikiwa nyeupe

> Amesema Virusi hivyo vilikuwa tishio la Maendeleo na vimeondoka kwa maombi

Tazama https://youtu.be/9ajyBdWJEeA
#JPM
RC KUNENGE AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA FUJO OKTOBA 28

> Mkuu wa Mkoa wa Dar amesema wamejipanga na amewahakikishia usalama Wapiga kura

> Awataka Wananchi wajitokeze bila wasiwasi kupiga kura kwa kuwa Polisi wamejiandaa kudhibiti vurugu

Tazama https://youtu.be/9uAzHABcDiM
#Uchaguzi2020
DAR: AHUKUMIWA MIAKA 2 JELA KWA KUMUUA MKEWE BILA KUKUSUDIA

> Yusuph Ismail (45) alimuua Magdalena Fabian kwa kumchapa fimbo na kumnyonga kwa madai ya kukosa uaminifu

> Wakati tukio linatokea Novemba 2013, wawili hao walikuwa wamelewa

Soma - https://jamii.app/HukumuMauaji
LISSU: VIONGOZI KAMA MAALIM SEIF HAWAZALIWI KILA SIKU

> Akiwa Pemba ktk Mkutano wa kufunga Kampeni za ACT- Wazalendo, amewakata Wazanzibari kumpa kura Maalim ili akamilishe ndoto ya Wazanzibari ya kuwa Taifa lililokuwa kabla ya Muungano

Soma - https://jamii.app/LissuPemba
#TZ2020
MAALIM SEIF: WALIMU WA MADRASA WATAINGIA KWENYE 'PAYROLL' YA SERIKALI

> Mgombea Urais #Zanzibar amesema, ni muhimu kwa Walimu wa Madrasa kuingia kwenye malipo ya Serikali kwasababu wanafanya kazi kubwa katika kuwaandaa watoto kiroho

Soma https://jamii.app/MaalimMadrassaWalimu
#Uchaguzi2020
JOSHUA NASSARI AOMBA RADHI KWA DKT. MAGUFULI

> Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nassari aomba radhi kwa machukizo aliyofanya alipokuwa upinzani

> Nassari alihamia CCM akitokea CHADEMA mwezi Julai 2020

Soma https://jamii.app/NassariVsMagufuli
#Uchaguzi2020
ZEC: MAKOSA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA YAMECHANGIWA NA WAPIGA KURA WENYEWE

> Ni kwasababu ya kushindwa kufanya uhakiki wa taarifa wakati zoezi hilo lilipofanyika

> ZEC itatoa msimamo kuhusu Wapiga Kura hao baada ya Kikao cha Uongozi

Soma - https://jamii.app/DaftariWapigaKura
#TZ2020
#CORONAVIRUS: KENYA YAREKODI VISA ZAIDI YA 1,000 NDANI YA SAA 24

> Maambukizi mapya 1,068 yamerekodiwa huku mgonjwa mdogo zaidi akiwa mtoto wa miezi 6

> Idadi ya visa imefikia 47,212, vifo 870 na wagonjwa waliopona hadi sasa ni 33,050

Soma - https://jamii.app/CovidKE
MMANGA: NITAVUNJA UONGOZI WA TFF NA KUINUA SOKA LA WANAWAKE

> Mgombea Urais kupitia Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga amesema TFF ni chanzo cha Migogoro kwenye Mpira

> Pia, watafufua #Michezo mingine ikiwemo kufundisha Watoto Bao

Soma https://jamii.app/MmangaTFF
#Uchaguzi2020
SERIKALI YAKOPA TSH BILIONI 136.85 KUKARABATI VIWANJA VYA NDEGE

> Serikali imezindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya Shinyanga, Tabora, Sumbawanga na Kigoma ili viwe vya Kimataifa

> Mkopo umetolewa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya

Soma https://jamii.app/MkopoNdege136b
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: WEZI SUGU 30 WAKAMATWA NA POLISI

> Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni limekamata wezi hao wakiwa na mali mbalimbali

> Watu wote waliopotelewa/kuibiwa na vitu wametakiwa kufika kituoni na risiti kubaini vitu hivyo kama ni vyao

Soma https://jamii.app/Wizi30Polisi

#JFLeo
PROF. LIPUMBA: TUTAJENGA UCHUMI WENYE USHINDANI KITAIFA NA KIMATAIFA

> Amesema, ukuaji wa uchumi unahitaji uongozi imara, utawala makini na mipango

> CUF itaweka misingi itakayohakikisha uchumi unakua kwa 8%–10% kila mwaka kwa miaka 10 ijayo

Soma https://jamii.app/LipumbaLindi
#TZ2020
AAFP: TUTAKUSANYA ILANI ZA VYAMA VYOTE NA KUUNDA SERIKALI YENYE SERA JUMUISHI

> Mgombea Urais, Seif Maalim Seif amesema dhana ya Chama kitakachoshinda kuchukua kila kitu ni kama ulaghai kwani Watanzania wamegawanyika katika nadharia tofauti

Soma https://jamii.app/SeifMaalimAAFP
#TZ2020