JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VUNJO: MREMA NA TLP WAMPOKEA MAGUFULI

> Pia, Mgombea huyo wa Ubunge wa Jimbo la Vunjo (TLP) na wafuasi wake wamempa Dkt. Magufuli zawadi ya mbuzi na mkungu wa ndizi

> TLP walitangaza mapema kuwa, CCM ikimsimamisha Magufuli watampigia kampeni

Soma https://jamii.app/TLPCCMVunjo
#TZ2020
IGP SIRRO: MAGAIDI ZAIDI YA 300 WALIVAMIA KIJIJI NA KUFANYA UHALIFU

> Magaidi hao kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji

> Amesema baadhi ya watu wamekamatwa, na wengine ni raia wa hapa

Soma - https://jamii.app/MagaidiMtwara
QUEEN SENDIGA AAHIDI KUBORESHA SEKTA BINAFSI ILI KUKUZA UCHUMI

> Amesema kwa sasa Sekta binafsi na Serikali kumekuwa na uadui japo wanacheka kwa nje ila ndani wana maumivu

> Mgombea huyo wa ADC ameomba kupewa kura ili kukuza uchumi wa nchi

Soma https://jamii.app/ADCSingida
#TZ2020
MAJALIWA: NAFASI YA URAIS INAGUSA MAISHA YAKO, SIO JAMBO LA MCHEZO

> Kassim Majaliwa akiwa Wilayani Masasi amesema, Urais wa #Tanzania unataka mtu mwenye uwezo wa kuongoza watu zaidi ya Milioni 60 wenye Dini, Vyama, Makabila na uwezo tofauti

Soma https://jamii.app/MajaliwaMasasi
#TZ2020
UJERUMANI: WAZIRI WA AFYA AKUTWA NA #COVID19

> Waziri wa Afya wa #Ujerumani, Jens Spahn amethibitishwa kukutwa na #CoronaVirus na tayari amejitenga

> Visa 11,287 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita na maambukizi kufikia 391,355 hadi sasa

Soma https://jamii.app/UjerumaniWaziri
NEC: MPIGA KURA ANAWEZA KUOMBA KARATASI NYINGINE AKIKOSEA AU KUBADILI UAMUZI

> Ofisa wa NEC, Flora Mkama amesema, wapiga kura wana haki ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura endapo itatokea kwa bahati mbaya amekosea au amebadili uamuzi

Soma https://jamii.app/KaratasiKuraNEC
#TZ2020
SAUDI ARABIA: MWANAMFALME ADAIWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KHASHOGGI

> Mchumba wa Jamal Khashoggi, Hatice Cengiz anamshtaki Mwanamfalme Mohammed Bin Salman kwa kutoa amri ya kuuawa kwa Jamal

> Jamal alikuwa mkosoaji wa Serikali ya Saudi Arabia

Soma https://jamii.app/CrownPrinceSued
KIGOMA: VIONGOZI 5 WA CHADEMA MBARONI KWA KUKUTWA NA KADI 14 ZA MPIGA KURA

> Waliokamatwa ni Hezron Vicent, Ezekia Samakere, Sheby Kasuka, Helson Miniho na Denis Lubuye

> RPC Manyama amesema walihojiwa lakini majibu yao hayakuwa na mashiko

Soma https://jamii.app/CDMKadiKura
#TZ2020
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAWAASA VIONGOZI WA DINI KUTOFANYA KAMPENI ZA KISIASA

> Imewaasa Viongozi wa Dini kutowaambia Wananchi wamchague Mgombea fulani kwasababu kufanya hivyo ni kinyume na kifungu cha 17(c) cha Sheria ya Jumuiya

Soma https://jamii.app/MOHaViongoziDini
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: NITAKUBALI MATOKEO IKIWA UCHAGUZI UTAKUWA HURU

> Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo amesema atakubali matokeo endapo atashindwa, ikiwa Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

> Pia, hatakuwa na tatizo kumpongeza Dkt. Hussein Mwinyi (CCM)

Soma https://jamii.app/MaalimMatokeoHaki
#TZ2020
GUINEA: WATU 10 WAUAWA KUTOKANA NA GHASIA BAADA YA UCHAGUZI

> Raia 8 na Polisi 2 wameuawa ktk ghasia za kupinga matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Rais

> #Guinea ilifanya Uchaguzi Oktoba 18 na matokeo yanaonesha Rais Alpha Conde anaongoza

Soma https://jamii.app/GhasiaUchaguziGuinea
CECILIA MMANGA: WAUGUZI WENYE SHAHADA HAWATAKI KWENDA VIJIJINI

> Mgombea Urais kupitia Demokrasia Makini amesema Watawasomesha wasafishaji wa Wodi za Hospitali kozi za Ukunga na wakifuzu watapelekwa Vijijini ili kupunguza vifo vya Wajawazito

Soma https://jamii.app/VifoWajawazito
#TZ2020
#NIGERIA: WATU 12 WAUAWA NA POLISI KATIKA MAANDAMANO

> Shirika la Amnesty International limesema uchunguzi umebaini ushahidi wa vifo 12 huku mamia wakijeruhiwa

> Limewatuhumu Polisi na Wanajeshi kutumia nguvu kupita kiasi

Soma https://jamii.app/12DeadNGR
#EndSARS
RAIS MAGUFULI: TANZANIA INAHITAJI JOZI MILIONI 54 ZA VIATU KWA MWAKA

> Ameyasema hayo alipokuwa anazindua Kiwanda cha bidhaa za Ngozi kilichopo Mkoani #Kilimanjaro

> Kiwanda hicho kitatengeneza ajira milioni 3 na ajira 3000 za moja kwa moja

Soma https://jamii.app/MagufuliViwanda
RAIS MAGUFULI: TANZANIA 'IMETOBOA' KWENYE MAENDELEO YA KWELI

> Amesema Kiuchumi #Tanzania imetoboa kutokana na wingi wa Viwanda vilivyopo

> Ametoa wito kwa Watanzania kununua bidhaa za ndani ili kukuza #Uchumi wa Nchi

Soma https://jamii.app/MagufuliViwanda
MMANGA: VIJANA MSISUBIRI AJIRA, KUWENI KAMA MARASTA

> Mgombea Urais JMT kupitia Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga amewataka Vijana kuacha kusubiri ajira Serikalini

> Asema Serikali yake itakuja na kauli ya 'Kilimo cha kufa na Kupona'

Soma https://jamii.app/DemkorasiaMakiniAjira
#Uchaguzi2020
RAIS MAGUFULI: TANZANIA NYEUPE PEE (HAINA CORONA)

> Amesema, chapisho la Gazeti la New York Times kuhusu hali ya #COVID19 Duniani limeitaja #Tanzania ikiwa nyeupe

> Amesema Virusi hivyo vilikuwa tishio la Maendeleo na vimeondoka kwa maombi

Tazama https://youtu.be/9ajyBdWJEeA
#JPM
RC KUNENGE AWAONYA WANAOPANGA KUFANYA FUJO OKTOBA 28

> Mkuu wa Mkoa wa Dar amesema wamejipanga na amewahakikishia usalama Wapiga kura

> Awataka Wananchi wajitokeze bila wasiwasi kupiga kura kwa kuwa Polisi wamejiandaa kudhibiti vurugu

Tazama https://youtu.be/9uAzHABcDiM
#Uchaguzi2020
DAR: AHUKUMIWA MIAKA 2 JELA KWA KUMUUA MKEWE BILA KUKUSUDIA

> Yusuph Ismail (45) alimuua Magdalena Fabian kwa kumchapa fimbo na kumnyonga kwa madai ya kukosa uaminifu

> Wakati tukio linatokea Novemba 2013, wawili hao walikuwa wamelewa

Soma - https://jamii.app/HukumuMauaji