JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KUELEKEA UCHAGUZI 28 OKTOBA 2020: MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU SANDUKU LA KURA

> Sanduku la kura linatakiwa kutengenezwa kwa namna ambayo inamruhusu mpiga kura kuweza kuweka karatasi ya kura bila kuweza kuitoa

Kwa elimu zaidi, soma > https://jamii.app/SandukuKura

#Uchaguzi2020 #TZ2020
#UGANDA: WASAFIRI WAKAMATWA WAKIWA NA VYETI BANDIA VYA #COVID19

> Nchini humo, wasafiri hutakiwa kuwa na vyeti vya kupima #CoronaVirus saa 120 kabla ya safari

> Abiria wanaoingia hutakiwa kuwa na cheti kinachothibitisha wamepimwa ndani ya 72

Soma https://jamii.app/COVID19UGWasafiri
HESLB: ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO BADO HAIJATOKA

> Bodi ya Mikopo imesema mchakato wa uchambuzi wa maombi bado unaendelea na taarifa zinazosambaa mitandaoni zikiwaelekeza waombaji kupakua 'App' ili kuona orodha hiyo sio sahihi

Soma https://jamii.app/OrodhaMikopoHESLB
MAARIFA: JE, WAJUA MARAIS WASTAAFU KUJENGEWA NYUMBA NA SERIKALI NI KWA MUJIBU WA SHERIA?

> Kifungu cha 9.-(1) cha Sheria ya Huduma kwa Wanasiasa Wastaafu ya 1999 inaeleza

> Kupewa nyumba yenye samani zake na itakuwa na vyumba visivyopungua 4, viwili self contained

> Kifungu kidogo (i): Ndani ya nyumba hiyo kuwe na Ofisi ambayo itakuwa na samani zilizokamilika

> (ii) Nyumba ndogo kwa ajili ya msaidizi wa kazi za nyumbani (a servant quarter)

Soma > https://jamii.app/MaraisNyumba
#JamiiTalks
DKT. MAGUFULI: UCHAGUZI HUU UTAAMUA TANZANIA IWE NA VIONGOZI WALINDA UHURU AU VIBARAKA WA MABEBERU

> Pia amesema, Uchaguzi huu utaamua kama tuendelee na Muungano na jitihada za kujenga Taifa linalojitegemea kiuchumi au turudi kuwa tegemezi

Soma https://jamii.app/JPMBagamoyo
#TZ2020
NEC YAWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUZINGATIA SHERIA ILI KUEPUKA MALALAMIKO

> Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Mahera Charles amesema, kuna baadhi ya watu wana chokochoko hivyo kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni na Sheria kutaepusha shari

Soma https://jamii.app/UchaguziChokochoko
#Uchaguzi2020
DKT. MWINYI: MUUNGANO HAUIUMIZI #ZANZIBAR BALI UNAINUFAISHA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM amesema, Muungano unawafanya Wazanzibari kunufaika kibiashara na kiusalama

> Pia, Wazanzibari wanaitegemea #Tanzania Bara ili kupata mazao mengi

Soma https://jamii.app/ZnzDktMwinyi
#TZ2020
LISSU: MAGUFULI ALIINGIA KWA KURA, ATAONDOKA KWA KURA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema, ifikapo Oktoba 28 wananchi wapige kura kufuta machozi ya miaka 5

> Amesema Maandiko Matakatifu yanasema #Haki huinua Taifa, sio pesa wala barabara

Soma https://jamii.app/LissuHai
#TZ2020
THAILAND: WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA UTAWALA WA KIFALME

> Raia wa #Thailand wameandamana kumshinikiza Waziri Mkuu, Prayuth Chan-ocha kujiuzulu na kuukomesha Mfumo wa Kifalme

> Pia, wanadai kuachiliwa kwa waliokamatwa kwasababu za Kisiasa

Soma https://jamii.app/ThailandMaandamano
QUEEN SENDIGA: KAMA KUNA KERO, TUMALIZE HASIRA KWENYE SANDUKU LA KURA

> Mgombea huyo Urais kupitia ADC, amewataka Wananchi kuacha kuingia kwenye ushawishi wa kuchafua Amani na badala yake wenye kero wakamalize hasira kwenye Sanduku la Kura

Tazama https://www.youtube.com/watch?v=DDFNDcdlVAs&feature=youtu.be
#TZ2020
ASKOFU GWAJIMA: NINA JINA LA KIISLAM, NINAITWA RASHID

> Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe(CCM) amesema alipata jina hilo baada ya kutelekezwa Msikitini

> Suala hilo lilimpa sababu ya kuusaidia Uislamu ikiwemo kujenga Visima vya Maji Dar

Tazama https://youtu.be/ieu6HWyR910
#Uchaguzi2020
DKT. BASHIRU: WAGOMBEA WA CCM KUTOENGULIWA NI SUALA LA KUTII SHERIA

> Amesema wana vitengo vya Sheria ambavyo haviruhusu Wagombea kujaza fomu bila kuhakikiwa

> Amesema, kwao suala la kukosea haliwezekani kwasababu CCM ni Chama cha Kitaasisi

Soma https://jamii.app/CCMWagombeaSheria
#TZ2020
ARGENTINA: VISA VYA #CORONAVIRUS VYAFIKIA MILIONI 1

> #Argentina imerekodi visa 1,002,662, ikiwa ni nchi ndogo zaidi kurekodi visa zaidi ya Milioni 1

> Inakuwa nchi ya tano kuathirika zaidi duniani nyuma ya Marekani, India, Brazil na Urusi

Soma - https://jamii.app/COVID-Arg
QUALITY GROUP LIMITED YAAMRIWA KUWALIPA TSH. MILIONI 232 WAANDISHI WAKE

> Mahakama ya Mwanzo ya Migogoro ya Kazi imeamuru Kampuni inayomilikiwa na Yusufu Manji, kuwalipa waliokuwa Waandishi wake kwa kuvunja Mikataba nao bila sababu maalumu

Soma https://jamii.app/ManjiWaandishi
#JFLeo
#NIGERIA: SHULE ZA LAGOS ZAFUNGWA KUTOKANA NA MAANDAMANO

> Kamishna wa Elimu Mjini humo amesema hakuna uhakika wa usalama kwa Wanafunzi na Watumishi

> Maandamano ya kupinga ukatili wa Polisi yanaendelea maeneo mbalimbali nchini humo

Soma - https://jamii.app/SchoolClosureNGR
MOROGORO: MBARONI KWA KUCHANA MABANGO YA WAGOMBEA WA CCM

>Isihaka Exavery (20) anashikiliwa kwa tuhuma za kuchana picha za Mgombea Urais, Dkt. Magufuli na za Mgombea Udiwani, Seif Zahoro Chomoka

> Upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/MoroPichaMagufuli
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: JINA LANGU LIPO NAMBA MOJA, USIHANGAIKE KUANGALIA KWINGINE

> Amewaambia Wananchi wasihangaike kuangalia kwingine kwasababu wale hawawahusu

> Asema, Uchaguzi ni wakati wa kuamua kama wanataka maendeleo au 'blah blah'

Soma - https://jamii.app/JPMKorogwe
#Uchaguzi2020
MAALIM SEIF: TULIKUBALIANA KUMUUNGA MKONO LISSU NA MEMBE AKIWEPO

> Baada ya kuona Kampeni zao zinasuasua, Kamati ya Uongozi ilikutana na Bernard Membe akiwepo

> Membe alitoa tarehe akisema ikifika hajaanza kampeni, ni bora kumuunga Lissu

Soma - https://jamii.app/MaalimMembeLissu
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: NI WAKATI WA KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

> Amesema "Miaka 5 iliyopita tumeimarisha uchumi, sasa 5 ijayo tutakuwa na jukumu la kuongeza mishahara. Huwezi kupandisha mishahara wakati huna uchumi, wengine wanazungumza tu"

Soma https://jamii.app/MaslahiWafanyakazi
#TZ2020
MAALIM SEIF: WAZANZIBARI WAMECHOKA, WAMEDHAMIRIA KULINDA DEMOKRASIA

> Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo amesema wanakwenda tarehe 27 na 28 wakiwa tayari kwa lolote litakalotokea kulinda #Demokrasia na #Haki ya watu kumchagua Rais wanayemtaka

Soma - https://jamii.app/MaalimHakiZnz
#TZ2020